Sakata Mkataba wa Bandari: Wakili Mwabukusi asema asiyetaka kukosolewa aondoke kwenye ofisi za Umma

Asilimia kubwa ya wanaopinga mkataba (IGA) Hawapingi mkataba (IGA) wa bandari, kwakua ili kupinga mkataba, ni lazima uanze na sheria zitakazo ongoza mkataba kwanza, kabla ya yaliyomo, kwakua yaliyomo ni lazima yafuate sheria. Hii ni kama tu unataka kupinga kwa nia njema ya taifa. Usipofanya hivyo nisawa na kuchukua maneno, na mistari miwili kwenye vitabu vitakatifu ili iendane na haja zako. Waingereza wanaita hali kama hiyo “ulterior motives”

Kuna msukumo mkubwa kwa wanaopinga lengo Lao kuu ni wanapinga Jamhuri ya Muungano ya Tanzania 🇹🇿 kuwa HURU kimapato kwa mara ya kwanza. Usione ajabu, Kaskazini wanakua na mtazamo tofauti wa mambo na sio dhambi. Hata Mangi Mkuu Mangi Marialle alipingana na Mwl kuhusu Tz kupata uhuru 09 Dec 1961, aliona muda haijafika kwanza, hatuna uwezo wa kujiongoza Bado.

Lakini Uhuru uliletwa na TANU, ambayo leo inaitwa CCM, baada ya kuugana na Afro Shirazi (ambacho likua na wapini Znz) 1977, na Kila mtu amefaidika kutokana na hilo.

unaweza kuiangalia South Africa 🇿🇦 Kijuju ukadhania bora tungechelewa kidogo kupata uhuru kama ulivyokua mtazamo wa Mangi Mkuu Mangi Marialle, japo alikua hapatani na mmoja wa mangi wadogo, mangi Shangali.
Laking Uhuru ni sasa, alisisitiza Mwl, na njia aliyofanikisha kutupitisha ndio tunaendelea nayo Leo.

Hili Jambo ni kubwa kiasi kwamba haliwezi kuwa na mkataba (IGA) mmoja wenye kurasa 38 tu, lazima iwepo mengine, pia ya kupenda na na makubaliano kati ya Tanzania 🇹🇿 na Dubai. Kuku, mbuzi, nguruwe, ngombe, ni nyama, kama vile IGA, HGA, na PA(s) yote ni mikataba, lakini nyama zote ziko Sawa? Mikataba yote iko Sawa?
Watu wanajua tofauti Za nyama, ila kutokana na shughuli zao Za Kila siku sio wote wanajua tofauti ya tofauti ya IGA, HGA, na PA(s).
Kutokua kwao usikutumie kwa faida yako kama wewe ni kiongozi wa kweli.

ukiiangalia kipengele cha 21, kipengele pekee pekee kinachoelezea sheria zitakazo ongoza mkataba, kwakua yaliyomo yote lazima yaendane na sheria.

Kimsingi tafsiri ya mkataba ni makubaliano yanayoweza kulazimishwa na sheria.

Sheria gani sasa zinaweza kulazimisha hayo makubaliano?

Jibu liko kipengele cha 21, kwamba IGA itafuata sheria Za uingereza ambazo tunazifuata tayari, zinafanana na Sheria zetu, kwakua tumezirithi kutoka serikali iliyokuwepo kabla ya 09 Dec 1961. Kipengele cha 21 pia kinasema HGA na makubaliano ya mradi yatafuata sheria Za Jamhuri ya muungano ya Tanzania. Na sheria Za Tanzania tunaweza kuzibadilisha tunavyotaka bila na mkataba (IGA) inatambua hilo, na kukiri hilo. Hii inakua muhimu kwenye mapato. Ndio maana mapato hayamo kwenye IGA, yatakuwepo kwenye HGA ili yafuate sheria Za Tanzania, na hapo ndipo Prof Mbarawa, wanalinda maslahi, ya wa Tanzania, kwamba mapato yangekuwepo kwenye IGA, tusingekua na control nayo. Badala ya kufurahia hilo wanaliruka, hakuna anayepinga anaweza kukataa ukweli huu.
 
Subiri maana ww ni mzee, na wazee wengi wa CCM bado mko kwenye usingizi wa mwenge wa uhuru. Kizazi kimebadilika hiki mzee.
Mimi na uhakika mtoto mdogo sana na uhakika nachosema kamwe hakuna wakuiondoa CCM kama wakuiondoa CCM basi wa humu humu ndani ya CCM hatatoka nje. uwezo wenu mdogo sana.
 
Kaka utakuwa na shida si kidogo mbona unafurahia mateso ya wenzako. Mfano Lisu kupigwa risasi zote zile bado huwezi kumhurumia. Kinyume chake unamkebehi. Ila kumbuka hujafa hujaumbika.
Nimuhurumie wa nini? mimi katika watu niliona vibaya sana alipopigwa na nilikuwa naona JPM katumia nguvu kuliko inavyotakiwa lakini ukiona mtu anaombea nchi hii machafuko huyo mtu hapana hatakiwi wala siwezi kumuonea huruma. wala sina roho mbaya ila kuna watu wanaitakia mabaya nchi hii na huyu ni mmoja wapo. Kila akisimama jukwaani kuhubiri chuki tu haji na policy mbadala tumuelewe.
 
Kwa hiyo Lissu kwake ilikuwa muhimu nani apewe sifa sio alilokuwa anagombania linatatuliwa ilikuwa about him sio wananchi kwenye migodi. Basi huyu hafai kama issue lazima atajwe yeye basi ana shida sana.
 
Hebu yijiulize maswali haya;.
1., Kwanini serikali imatumia nguvu kubwa kuzima hoja za wananchi
2., Kwanini wako tayari hata kudhuru watu kisa mkataba

3, Kwanini wanashindwa kuelezea kwa hoja na badala yake ni blah blah
Kwa ufupi mkataba ni maandishi na kinachotakiwa kujengewa hoja za kuzungumza ni huu mkataba na sio hizo blahblah za CCM na watu wake ambao wengine hata mkataba tunahisi hawajasoma ndio maana wanaongea utumbo huko mitaani.
 
Njaa mbaya
 
Huu ndio ukweli.Kwa nini udharau mamlaka,ukidharau mamlaka unadharau wananchi.
 
Nyinyi mshukuru sana Mungu alimchukua JPM mapema angewarudisha kwenye mapango mlikotoka. Mama katukosea sana na huruma zake. Ingepita operation moja kabambe ndio mngeshika adabu mbwa nyie.
Kweli kabisa.Punda hendi bila fimbo.
 
Huyo wakili analishwa na anawalisha wajinga matango pori

Hivi lile bakuri lenu mmefikia wapi mbona hamjatoa mrejesho mmepata bei gani baada ya kugeuka kuwa omba omba?
Wakili ni msomi mwenye akili. Ninyi punguani bakini kama mlivyo. Hakuna namna ya kumfanya punguani kuwa intelligent.
 
Hisia zako hazihitaji uwe na hasira.
Wao wakiwa mbwa sasa ww ni Nani?
Embu acha maneno ya kuudhi na kukebehi.
Sote ni Binadamu.
Huyo Heijah kama anawaona wanadamu wenye akili ni mbwa, basi labda yeye mwenyewe anajiona ni ngiri au fisi.
 
Huu wimbo wa taharabu unaitwaje
 
Nyinyi Chadema sio ndio lugha myaoelewa. Mtu akiwa mstaarabu nyinyi ndio mnaona idhaifu, Rais Samia mpole mnamuona dhaifi mnahitaji watu kama JPM ndio mnakuwa na heshima.
Hivi mwisho wake yeye na Cdm nani anaendeleza harakati zake ?!. Hata wewe chuki zako haziwezi kuiua Cdm. Unateseka bure.

Kinachopingwa ni aina ya mikataba ile ya madini , Gas & mafuta na mbuga za wanyama pori. Mikataba ya win win situation hakuna wa kulalamika.
 
Mimi na uhakika mtoto mdogo sana na uhakika nachosema kamwe hakuna wakuiondoa CCM kama wakuiondoa CCM basi wa humu humu ndani ya CCM hatatoka nje. uwezo wenu mdogo sana.
Hakuna wa ndani ya CCM ataweza kuindoa CCM, maana hakuna mwanaccm anaweza kufanya siasa za nje ya CCM, kwani wote wanategemea mbeleko ya vyombo vya dola. Uwezo wetu mdogo sana maana hatushindani na CCM ya kisiasa tena, bali vyombo vya dola.. ufahamu sisi hatuna silaha. Lakini kwa uhalisia ulivyo, machafuko au mapinduzi pekee ndio yataondoa ccm madarakani, kwani haipo madarakani kwa ridhaa ya wananchi walio wengi tena.
 
ningetaka kuwa mwanasiasa ama WA CCM au chadema nisingeshindwa sababu kote Nina connection na uwezo wa kupenya ila Sina interest na siasa za Tanzania ila kama mzalendo lazima nitetee uwepo wa serikali ya Tanganyika na kulinda rasilimali za nchi kwa mujibu wa katiba.

uwezo wako mdogo wa kufikiri ndio unakufanya uhisi Kila mtu lazima awe chadema au CCM.
 
Sasa unajuwa rasilimali maana yake nini? bandari ni rasilimali, eti na connection ukisikia mtu yoyote anajinado mzalendo ujue mnafaki subiri usifiwe sio kujitapa.
 
Kwa hiyo Lissu kwake ilikuwa muhimu nani apewe sifa sio alilokuwa anagombania linatatuliwa ilikuwa about him sio wananchi kwenye migodi. Basi huyu hafai kama issue lazima atajwe yeye basi ana shida sana.
Kwa Magufuli ilikuwa ni nani apewe sifa. Lakini ukweli ni kuwa Lisu ndio mwenye rekodi ya kupigania migodi na wananchi wa huko. Na hakusubiri hadi awe rais.
 
Machafuko au Mapinduzi? jaribu halafu ndio utajuwa CCM iko mpaka kwenye nyumba unayoishi hiyo hata kivuli chako CCM.
 
Sasa unajuwa rasilimali maana yake nini? bandari ni rasilimali, eti na connection ukisikia mtu yoyote anajinado mzalendo ujue mnafaki subiri usifiwe sio kujitapa.
mbona unatapatapa kwa siasa zetu na sio siasa ukiwa na connection ni rahisi kufika unapotaka ila kwa sababu sitaki kuwa chawa ndio maana nimejiweka mbali na siasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…