KERO Sakila Chini, Mtaa wa Mbuyuni - Arusha hakuna maji, Hospitali, Shule wala duka la dawa

KERO Sakila Chini, Mtaa wa Mbuyuni - Arusha hakuna maji, Hospitali, Shule wala duka la dawa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kikati.jpg
Kiakti1.jpg
Kikati22.jpg


Kwetu ni Arusha sehemu wanaita Sakila Chini, Mtaa wa Mbuyuni, tangu enzi za bibi zetu hakuna maji hakina shule hakuna hospitali hakuna chochote miaka na miaka naomba tupazie sauti tupate hata maji tu tunanunua maji kwa pikipiki dumu moja mia tano hata barabara hatuna.

Viongozi wana trekta, wanafata maji na trekta sisi wananchi ni punda tunafuata umbali mrefu sana, sehemu ya nauli kwa bodaboda elfu moja mia tano au ulipe boda alete dumu tatu kwa elfu nne hata soko hatuna jamani tusaidieni na sisi tupumzike kidogo

Hiyo pichani ndiyo ofisi ya Kijiji cha Sakila Chini na barabara ndiyo hiyo, hakuna shule hakuna maji hakuna hospitali hakuna hata duka la dawa.

Hospitali tunafuata Kikatiti na shule ni Kikatiti pia maji tunafuata kiwanda kwa boda, dumu nne elfu 5, dumu la liter 20, hospital iKikatiti au Tengeru sehem ya nauli elfu tano kwenda tu.
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Hatari sana tanzania, kutatua tatizo la shule wananchi wa hiko mngeshirikiana kufyatua tofali za udongo, mamlaka zije kuwasaidoa walimu
 
Back
Top Bottom