lufthansa01
New Member
- Sep 11, 2024
- 2
- 2
๐๐๐๐๐๐๐Nisiwe muongo. Haipo
๐๐๐๐๐๐๐Nisiwe muongo. Haipo
Great commentgreat job" au " excellent" , paper ilichafuka kwa remark nzuri za mwalimu.
Baada ya miaka miwili ya ugonjwa wa korona. Niliudhurua mkutano wa Mwalim MWAKASEGE. Nikapata kazi inayoitaji mtu mwenye uzoefu wa miaka 12. Mim nilikuwa chini ya hapo. Sikutuma maombi walinitafuta linkedin wakanipigia simu kutoka nje ya bara la africa wananihitaji. ๐Kama wewe ni Mkristo mkatoliki ni sala, Novena, Rozali au uliwahi funga kuombea kitu na kikafanikiwa?
Mfano kwenye kuomba kazi, mke au mume au masomo n.k tushirikishe
Pia madhehebu mengine karibuni kushuhudia kulingana na MUNGU alivyokutendea.
Was matter of time,hizo hekaya zako za maombi ndiyo useme chanzo cha kupata ajira serikali ni uongo uliodhahiriNovena ya mt. Rita nilisaliwa na mke wangu nikapata kazi serikalini.
nielezee kiufupi mimi kila nikiswali sipati majibu yoyote yaleSunna ya dhuha ni komesha
Endelea kuswaliKivip nenielezee kiufupi mimi kila nikiswali sipati majibu yoyote yale
ma ila yote uliyoandika ni uongo mtupuNi nyingi ila nitaelezea moja, Mama alininunulia kile kitabu cha mawaridi ya sala nilivyoanza form one, so nilikua nasali zile sala mara kwa mara, sasa nakumbuka kipindi nipo form three ilipokaribia mitihani ya mwezi wa sita basi nikaweka nia , nikaanza kusali novena ya "mt Anthony" ipo kwenye mawaridi ya sala.
kila siku asubuhi kabla ya kuanza mitihani nasali na jioni nasali ombi langu lilikua "Mungu anisaidie nifaulu vizuri mitihani yangu, anikumbushe yale yote nitakayosoma na awe pamoja na mimi kwenye chumba cha mtihani".nilikua ni mmoja wa wanafunzi wazuri tu kwa darasa langu nilikua najua siwezi kufeli lakini basi tu, niliamua kujiombea,๐.
Basi bwana siku hiyo tukaletewa paper ya physics(lilikua somo langu pendwa pamoja na Maths), yaani ile paper ilikua kama mwalimu anatukomoa hivi, kwa kifupi nilitoka sina matumaini mazuri kabisa, sasa wenzangu wanatoka wanaelezea njia walizofanya, maana tulikua na group discussion naona watu wanatiririka tu jinsi walivyojibu maswali ambayo mimi yalinitatiza, lakini niliyafanya, kwakweli niliona hali yangu ni tete nikifaulu sana basi 60sivuki hapo.
Hatimaye siku zikaenda, sikuhiyo tupo uwanjani ilikua siku ya michezo,tukaja kuitwa form three science wote tunaitwa na mwalimu "Adrian" alikua mkali balaa , kapanga karatasi from the worst to the best na fimbo mbili zimenyooka.
Kwanza kaanza kutupiga beat hapo, kauliza nikifundisha hamuelewi au shida nini? akasema nusu ya darasa wapo below fifty, watu kimyaaa.
kaanza kuita majina unatajiwa na marks zako mbele ya wanafunzi wote then kama upo below fifty unakula fimbo za kutosha halafu unaenda kukaa, halafu kama ni mwanafunzi mzuri lakini sikuhiyo hujafanya vizuri kama kawaida yako unakula fimbo hatakama umepata above fifty.
hapo natetemeka balaa naona karatasi zinaenda tu siitwi, mwisho wakaitwa wote ikabaki ya kwangu akaniambia njoo mbele nikaenda, akaniuliza unahisi umepata ngapi? Nikamwambia 85, maana aliyekua wa pili alikua ana 80%, akaniambia NO una 98% daah!!!! nikaanza kulia๐๐๐ mwalimu anacheka ananiambia ukiendelea kulia nakuchapa ili ulie vizuri๐๐, wanafunzi wenzangu wakapiga makofi meengi , hii moment huwa siisahau na mpaka leo ule mtihani ninao nimeutunza.
Nilianza kukagua yale maswali ambayo nilikua nauhakika sijafanya vizuri nikakuta nilifanya kwa njia ambayo mwalimu hakufundisha nikawa najiuliza hii njia nilitoa wapi?? So kwenye kila swali mwl alikua anasahihisha anaweka comment "great job" au " excellent" , paper ilichafuka kwa remark nzuri za mwalimu.
Hapa ndipo mbegu ya kumtegemea Mungu ilipandwa.
Hata sasa hivi nimeshakua mtu mzima,( mwaka 2019 niliokoka rasmi) nguzo yangu ya kwanza kwenye maisha ni kumtegemea Mungu wakati wote na nyakati zote niwe na raha au shida nipo na Mungu tu.
huwa nikipita kwenye changamoto naona kama sioni mbele, sioni kama nitatoboa basi huwa nakumbuka hiki kipindi hapa nasema Mungu anasikia maombi na anajibu so naendelea kukomaa.Kwa kifupi maisha yangu mpaka hapa nilipo ni Mungu tu na hakuna kitu naogopa kama kumkosa Mungu kwenye maisha yangu.
" Kwa maana ndani yake tunaishi,tunakwenda na kuwa na uhai wetu"(Mdo 17:28).
Sio MBAMIZWA?Novena kwa Mt Ritha wa kashia
Bikra Maria mkingiwa dhambi ya asili uiombee Tanzania
cc secretarybird mkatumeni mla sadaka DIVISHENI FOO
Shindwa peto ๐๐Sio MBAMIZWA?
Sala yoyote ya kimya na penye utulivu ukiwa pekeyako chumbani ama popote huleta majibu ya harakaKama wewe ni Mkristo mkatoliki ni sala, Novena, Rozali au uliwahi funga kuombea kitu na kikafanikiwa?
Mfano kwenye kuomba kazi, mke au mume au masomo n.k tushirikishe
Pia madhehebu mengine karibuni kushuhudia kulingana na MUNGU alivyokutendea.
okay.Sijaso
ma ila yote uliyoandika ni uongo mtupu
Mashallah kijana umeivaaNYAKATI AMBAZO DUA HUJUBIWA.
1.Theluthi ya mwisho ya usiku. Huu ni usiku wa manane usiku mkubwa. Muda huu mweye kuomba dua katu haiwezi kurudi kama anavyosimulia Abuuhurairah ุฑุถูุงููู ุนูู kuwa Mtume ุตููู ุงููู ุนููู ูุณููู amesema "โ ููููุฒููู ุฑูุจููููุง ููููู ููููููุฉู ุฅูููู ุงูุณููู ูุงุกู ุงูุฏููููููุง ุญูููู ููุจูููู ุซูููุซู ุงูููููููู ุงูุขุฎูุฑู ููููููููู ู ููู ููุฏูุนููููู ููุฃูุณูุชูุฌููุจู ูููู ููู ููู ููุณูุฃูููููู ููุฃูุนูุทููููู ููู ููู ููุณูุชูุบูููุฑูููู ููุฃูุบูููุฑู ูููู โ" โanashuka Mola wetu aliye tukuka kuja mbingu ya dunia kila usiku pindi inapobaki theluthi ya usiku ya mwisho kisha husema โnani ataniomba nimjibu maombi yake, nani antaniomba nimpe na nani ataniomba msamaha nimsameheโ. (amepokea Bukahari, muslim na wengine).
2.Baada ya swala za faradhi. Anayetaka kuomba dua basi aombe baada ya kuswali swala ya faradhi, dua yake itajibiwa. ุนููู ุฃูุจูู ุฃูู ูุงู ูุฉูุ ููุงูู ููููู ููุง ุฑูุณูููู ุงูููููู ุฃูููู ุงูุฏููุนูุงุกู ุฃูุณูู ูุนู ููุงูู โ"โ ุฌููููู ุงูููููููู ุงูุขุฎูุฑู ููุฏูุจูุฑู ุงูุตููููููุงุชู ุงููู ูููุชููุจูุงุชู โ"โ Amesimulia Abuu Umama ุฑุถูุงููู ุนูู kuwa aliulizwa Mtume ุตููู ุงููู ุนููู ูุณููู โdua gani husikulizwa (zaidi na Allah? Akasema๐ usiku mkubwa (theluthi ya mwisho ya usiku) na baada ya swala za faradhiโโ. (amepokea tirmith kwa isnad sahihi).
3.Kati ya adhana na iqama. Huu ni muda unaopatikana baada ya kuadhiniwa na mpaka kukimiwa kwa swala. Hapa mwenye kuomba dua itakuwa ni yenye kujibiwa. Amesimulia Anas ุฑุถูุงููู ุนูู kuwa Mtume ุตููู ุงููู ุนููู ูุณููู amesema โhairudishi (haiachi kujibiwa dua) kati ya adhana na iqamaโ. (amepokea Abuu Daud, Nisai na tirmith kwa isnad sahihi).
4.Wakati wa kusujudi. Hii ni dua inayoomwa wakati mtu akiwa amesujudi, dua hii pia ni yenye kujibiwa. Amesimulia Abuuhurairah ุฑุถูุงููู ุนูู kuwa Mtume ุตููู ุงููู ุนููู ูุณููู amesema โmuda ambao mja anakuwa karibu zaidi na Mola wake ni pale akiwa amesujudi. Basi zidisheni dua (muda huu) na uweni na uhakika kuwa mtajibiwa. (amepokea Muslim na Daud).
5.Muda wa kukutana majeshi kwenye jihad, muda wa kunyesha kwa mvua, muda wa kukimiwa kwa swala na na muda wa kuiona alkaba. Amepokea Abuu Umamah ุฑุถูุงููู ุนูู kuwa Mtume ุตููู ุงููู ุนููู ูุณููู amesema: โhufunguliwa milango ya mbinguni na hujibiwa dua katika maeneo manne (nyakati): muda wa kukutana safu katika jihadi, muda wa kunyesha kwa mvua, muda wa kukimiwa kwa swala na muda wa kuiona alkabaโ. (amepokea Tabrany).
6.Siku ya ijumaa. Siku ya ijumaa kuna muda ambao dua hujibiwa bila ya tatizo. Muda huu ni mchache sana na hakuna anaoujua. Zipo riwaya nyingi sana zinataja muda huu. Ila kuna riwaya zinaonesha muda huu ni baada ya swala ya al-โasr mpaka magharib. Ila ukweli ni kuwa muda huu ni mchache sana na haujulikani, jambo la msingi ni kujitahidi kumuomba Allah siku ya ijumaa yote huenda muda huo ungeupata.