Sala au maombi gani ambayo uliwahi kusali yakaleta matokeo tushirikishe

Kama wewe ni Mkristo mkatoliki ni sala, Novena, Rozali au uliwahi funga kuombea kitu na kikafanikiwa?
Mfano kwenye kuomba kazi, mke au mume au masomo n.k tushirikishe

Pia madhehebu mengine karibuni kushuhudia kulingana na MUNGU alivyokutendea.
Baada ya miaka miwili ya ugonjwa wa korona. Niliudhurua mkutano wa Mwalim MWAKASEGE. Nikapata kazi inayoitaji mtu mwenye uzoefu wa miaka 12. Mim nilikuwa chini ya hapo. Sikutuma maombi walinitafuta linkedin wakanipigia simu kutoka nje ya bara la africa wananihitaji. ๐Ÿ™
 
Sala ni nyingi sana, Mungu wetu hajawahi kuchelewa wala kuwahi, wakati wa Mungu ni wakati sahihi.
 
Sijaso ma ila yote uliyoandika ni uongo mtupu
 
Kama wewe ni Mkristo mkatoliki ni sala, Novena, Rozali au uliwahi funga kuombea kitu na kikafanikiwa?
Mfano kwenye kuomba kazi, mke au mume au masomo n.k tushirikishe

Pia madhehebu mengine karibuni kushuhudia kulingana na MUNGU alivyokutendea.
Sala yoyote ya kimya na penye utulivu ukiwa pekeyako chumbani ama popote huleta majibu ya haraka
 
NYAKATI AMBAZO DUA HUJUBIWA.
1.Theluthi ya mwisho ya usiku. Huu ni usiku wa manane usiku mkubwa. Muda huu mweye kuomba dua katu haiwezi kurudi kama anavyosimulia Abuuhurairah ุฑุถู‰ุงู„ู„ู‡ ุนู†ู‡ kuwa Mtume ุตู„ู‘ูŠ ุงู„ู„ู‡ ุนู„ูŠู‡ ูˆุณู„ู‘ู… amesema "โ€ ูŠูŽู†ู’ุฒูู„ู ุฑูŽุจู‘ูู†ูŽุง ูƒูู„ู‘ูŽ ู„ูŽูŠู’ู„ูŽุฉู ุฅูู„ูŽู‰ ุงู„ุณู‘ูŽู…ูŽุงุกู ุงู„ุฏู‘ูู†ู’ูŠูŽุง ุญููŠู†ูŽ ูŠูŽุจู’ู‚ูŽู‰ ุซูู„ูุซู ุงู„ู„ู‘ูŽูŠู’ู„ู ุงู„ุขุฎูุฑู ููŽูŠูŽู‚ููˆู„ู ู…ูŽู†ู’ ูŠูŽุฏู’ุนููˆู†ููŠ ููŽุฃูŽุณู’ุชูŽุฌููŠุจูŽ ู„ูŽู‡ู ูˆูŽู…ูŽู†ู’ ูŠูŽุณู’ุฃูŽู„ูู†ููŠ ููŽุฃูุนู’ุทููŠูŽู‡ู ูˆูŽู…ูŽู†ู’ ูŠูŽุณู’ุชูŽุบู’ููุฑูู†ููŠ ููŽุฃูŽุบู’ููุฑูŽ ู„ูŽู‡ู โ€" โ€œanashuka Mola wetu aliye tukuka kuja mbingu ya dunia kila usiku pindi inapobaki theluthi ya usiku ya mwisho kisha husema โ€˜nani ataniomba nimjibu maombi yake, nani antaniomba nimpe na nani ataniomba msamaha nimsameheโ€. (amepokea Bukahari, muslim na wengine).

2.Baada ya swala za faradhi. Anayetaka kuomba dua basi aombe baada ya kuswali swala ya faradhi, dua yake itajibiwa. ุนูŽู†ู’ ุฃูŽุจููŠ ุฃูู…ูŽุงู…ูŽุฉูŽุŒ ู‚ูŽุงู„ูŽ ู‚ููŠู„ูŽ ูŠูŽุง ุฑูŽุณููˆู„ูŽ ุงู„ู„ู‘ูŽู‡ู ุฃูŽู‰ู‘ู ุงู„ุฏู‘ูุนูŽุงุกู ุฃูŽุณู’ู…ูŽุนู ู‚ูŽุงู„ูŽ โ€"โ€ ุฌูŽูˆู’ูู ุงู„ู„ู‘ูŽูŠู’ู„ู ุงู„ุขุฎูุฑู ูˆูŽุฏูุจูุฑูŽ ุงู„ุตู‘ูŽู„ูŽูˆูŽุงุชู ุงู„ู’ู…ูŽูƒู’ุชููˆุจูŽุงุชู โ€"โ€ Amesimulia Abuu Umama ุฑุถู‰ุงู„ู„ู‡ ุนู†ู‡ kuwa aliulizwa Mtume ุตู„ู‘ูŠ ุงู„ู„ู‡ ุนู„ูŠู‡ ูˆุณู„ู‘ู… โ€˜dua gani husikulizwa (zaidi na Allah? Akasema๐Ÿ™‚ usiku mkubwa (theluthi ya mwisho ya usiku) na baada ya swala za faradhiโ€™โ€. (amepokea tirmith kwa isnad sahihi).

3.Kati ya adhana na iqama. Huu ni muda unaopatikana baada ya kuadhiniwa na mpaka kukimiwa kwa swala. Hapa mwenye kuomba dua itakuwa ni yenye kujibiwa. Amesimulia Anas ุฑุถู‰ุงู„ู„ู‡ ุนู†ู‡ kuwa Mtume ุตู„ู‘ูŠ ุงู„ู„ู‡ ุนู„ูŠู‡ ูˆุณู„ู‘ู… amesema โ€œhairudishi (haiachi kujibiwa dua) kati ya adhana na iqamaโ€. (amepokea Abuu Daud, Nisai na tirmith kwa isnad sahihi).

4.Wakati wa kusujudi. Hii ni dua inayoomwa wakati mtu akiwa amesujudi, dua hii pia ni yenye kujibiwa. Amesimulia Abuuhurairah ุฑุถู‰ุงู„ู„ู‡ ุนู†ู‡ kuwa Mtume ุตู„ู‘ูŠ ุงู„ู„ู‡ ุนู„ูŠู‡ ูˆุณู„ู‘ู… amesema โ€œmuda ambao mja anakuwa karibu zaidi na Mola wake ni pale akiwa amesujudi. Basi zidisheni dua (muda huu) na uweni na uhakika kuwa mtajibiwa. (amepokea Muslim na Daud).

5.Muda wa kukutana majeshi kwenye jihad, muda wa kunyesha kwa mvua, muda wa kukimiwa kwa swala na na muda wa kuiona alkaba. Amepokea Abuu Umamah ุฑุถู‰ุงู„ู„ู‡ ุนู†ู‡ kuwa Mtume ุตู„ู‘ูŠ ุงู„ู„ู‡ ุนู„ูŠู‡ ูˆุณู„ู‘ู… amesema: โ€œhufunguliwa milango ya mbinguni na hujibiwa dua katika maeneo manne (nyakati): muda wa kukutana safu katika jihadi, muda wa kunyesha kwa mvua, muda wa kukimiwa kwa swala na muda wa kuiona alkabaโ€. (amepokea Tabrany).

6.Siku ya ijumaa. Siku ya ijumaa kuna muda ambao dua hujibiwa bila ya tatizo. Muda huu ni mchache sana na hakuna anaoujua. Zipo riwaya nyingi sana zinataja muda huu. Ila kuna riwaya zinaonesha muda huu ni baada ya swala ya al-โ€™asr mpaka magharib. Ila ukweli ni kuwa muda huu ni mchache sana na haujulikani, jambo la msingi ni kujitahidi kumuomba Allah siku ya ijumaa yote huenda muda huo ungeupata.
 
Nina ushubuda wa mambo karibia yote kwenye maisha yangu yanajibiwa kwa maombi, japokuwa mimi ni mmoja kati ya binadamu wenye dhambi nyingi sana hasa hizi ndogo ndogo, lakini lakini nitakuwa shahidi wa kwanza na wa mwisho kuwa Mungu yupo na anajibu maombi. Kwangu mimi maombi huwa yanajibiwa dakika za nyongeza yaani zile dakika ambazo pumzi inakaribia kuniisha then paaah.
 
Mashallah kijana umeivaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ