- Thread starter
- #21
Mkuu, nikumbushe lini upinzani mlimuunga mkono JPM.
Tambua Mama Samia alipoanza alikuwa na uungwaji mkono wote hadi alipokuja kuyakoroga.
JPM alipoanza na kuondosha polisi wala rushwa sehemu mbalimbali haswa traffic aliungwa mkono. Mengi mazuri yalifanyika kipindi cha Kangi Lugora na dhuluma za polisi hasa wa barabarani.
Mkuu JPM tusingeweza kumwunga mkono kwenye:
1. Misimamo yake na ugonjwa wa Corona
2. Kuiingilia mihimili mingine ya utawala
3. Kuendesha na kuratibu magenge ya watu wasiojulikana
4. Ubambikaji wa kesi kwa watu
5. Kutokuzingatia katiba yakiwamo kuzuia mikutano ya siasa
6. Wizi wa chaguzi hasa 2019/20
7. Ununuzi wa wapinzani kwa pesa za umma
8. Upelekaji wa miradi kwao kinyume cha katiba
9. Manunuzi ya madege kinyume cha katiba
10. Kujinasibu kwake hadharani kupeleka miradi kunako wabunge na wakilishi wa CCM tu
11. Kuuwa demokrasia nchini
12. Kujenga chuki baina ya watu kisiasa
13. Kuwa kina Sabaya na kina kondakta Kwamba walikuwa majembe
14. Kuzuia mabinti wanaopata ujauzito kutorudi shule
15. Kutokulipa wastaafu mafao yao kwa wakati
16. Kufilisi watu kwa kuwabambikizia madai ya kodi hewa
17. Nk nk.
Labda utuonyeshe wewe kuwa ulitegemea Tumwunge mkono kwenye lipi zaidi.