Ben na Azory walikuwa hatari kiasi gani ktk siasa za Tz mpaka uhisi Serikali waliwapoteza!???
Kwann kina Zitto, Mnyika, Mdee, Sugu etc waliokuwa wakimkosoa Magufuli WAZIWAZI wasishughulikiwe badala yake ashughulikiwe Ben asiye na lolote la maana ktk ulingo huu wa kisiasa nchini!?????
Mmemezeshwa na kukaririshwa ujinga tu bila kutumia hata common sense ktk arguments zenu
Vitengo vya kiuchunguzi vya Serikali vikiamua na na kuweka umakini zaidi basi Mbowe ana kesi ya kujibu kuanzia ishu ya skendo ya 'kumzima' Chacha Wangwe mpaka kwa Ben Saanane
Kwani kuna asiyewajua tena watu wasiojulikana?
Kwani hatukuwasikia kina Adamoo, Ling'wenya, Mhina au Mdude wakisimulia?
Hivi sasa tunawajua kwa majina, sura na hata nani alikuwa akiwatuma.
Kwamba? - "Ben na Azory walikuwa hatari kiasi gani ktk siasa za Tz mpaka uhisi Serikali waliwapoteza!???"
Kwani Adamoo, Ling'wenya, Urio, Malema, Lijenje, au Mdude walikuwa hatari kiasi gani ktk siasa za Tz mpaka yeyote kupanga kuwapoteza!???
Kwani nani hata alipata kuyasikia majina yao kabla?
Yaliyowakuta wao bila ya shaka yaliwakuta pia kina Ben, Mawazo, Lissu, Azory, Mdude na hata wale wa kwenye viroba. Bila shaka hata washambulizi wao walikuwa ni wale wale.
Kwamba? - "Kwann si kina Zitto, Mnyika, Mdee, Sugu etc?"
Huu ndiyo utetezi madhubuti sasa wa kujinasua kwenye shutuma za kuwashambulia kina Ben, Azory, Adamoo, Ling'wenya, Urio, Malema, Lissu, Lijenje na tusiowajua kwenye viroba?
Hivi ni kwa kutuona je vile? Kwa hiyo tuseme sasa ndiyo mlikuwa kazi yenu mmeimaliza? Kwani kina Lijenje wako wapi?
Visingizio na vijimaelezo dhoofu kama hivyo hata Chatto na Makunduchi hawawezi kuvikubali!
Wangwe? Una maana Wangwe alinyamazishwa kama Kolimba, Sokoine, Kombe, Shaba, au Mwaikambo?
Kuna na ndege ikitokea Zanzibar kwenye kipindi cha uchaguzi 2020 nayo inasemwa semwa kwenye nyamazishana zenu hizi.
"Mmemezeshwa na kukaririshwa ujinga tu bila kutumia hata common sense ktk arguments zenu!"
Au wewe ndiyo sehemu ya ujinga au kuaminishwa kwenyewe?
Kumbuka hata ichukue muda gani tutarejea ku account kwa kila mmoja mliyempoteza au kumwua wakiwamo kina Lijenje na wale wa kwenye viroba.
Kwenye hilo wala hatutanii.
Habari ndiyo hiyo.