Nimesoma hii taarifa na nimejaribu kufatilia je tangu ilipotoka hapa jukwaani kuna mrejesho wowote kutoka kwenye hizi Mamlaka na watu waliotajwa?
Kama haya mambo kwa mujibu wa mleta mada ni kweli, Hii ni zaid ya dhambi hata shetani mwenyewe huenda alikimbia kuogopa ushahidi kwa Mungu.
Mawazir, DC, Maji,Polisi!! yaani wote hawa wanajua hii dhulma? Na wapo Maofisini wanafanya kazi, Za kumtumikia nani? Mwananchi? Hapana...Mungu mwenyewe Kuna matendo haysameheki na ukiyaacha unakua sehemu ya huo Uovu.
Tutafunga kama kwa mikono yetu tumeshindwa kumalizana na hawa Waovu. Na hizi tuhuma kama zina ushahidi kabisa tutazifikisha kwa Mkuu wa nchi ili tujitoe kwenye ghadhabu za Mungu za kufumbia macho dhulma za namna hii.
Wazir, DC, Jaji uliyemtaja, watuhumiwa wa Uovu huo ni Muslims, hii haukubaliki kwenye Imani yetu, hakika kama ni kweli wanastahili kulaaniwa na kila Muislam kwa Uovu huo, nasema kama ni kweli, Sisi tutafunga kumshtakia Mungu kwa wenzetu hawa kutenda kinyume na Imani yetu.
Pole sana kwa hayo, sisi hatujui ila Mungu anajua na analipa hapa hapa.