Salaah (Silent Ocean) mrejeshee Kijana uliyetaifisha mali zake, nakupa saa 72

Salaah (Silent Ocean) mrejeshee Kijana uliyetaifisha mali zake, nakupa saa 72

Yule mangi tajiri alikuwa zulumati na muuaji ilikuw ikifika usiku utamuinea huruma.roho zinaanza kumfata.alikuwa na nyumba nyingi lakini usiku inabidi alale juu ya mti.au awaite baa kwake awape bia adi asubui ili asibaki peke Ake
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
JamiiForums324928181.gif


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Humu ndani kumezaliwa mambo Dah

Huo mda ufike tu huyo mwamba aje kupasua hilo jipu

Lakini nadhani mama anafuatilia huu mtanange viedi kabisa

Tafadhali mama okoa hili jahazi kabla mambo hayajaenda harijojo mda unayoyoma hivyoo
najua hili liko ndani ya uwezo wako mama etu kipenzi tafadhali
 
Kwa leo sitaandika mengi.

Najua tambo zako za sasa kuwa katika Serikali hii ya sasa mnaweza fanya lolote na hakuna wa kuwafanya kitu.

Najua ulivyojigeuza Serikali na kutaifisha mali na pesa za kijana huyo na ukaahidi utapiga nae hesabu na kumrejeshea kinachozidi na hujafanya hivyo toka June 14, 2022.

Hata kama mnasema Serikali ya sasa inawabeba basi iheshimuni japo kidogo kwa kutoifedhehesha.

Kumbuka kama ilitokea Serikali ikawafanya kuwa na adabu basi siku hazigandi.

Kumbuka kaka yenu mkubwa alikuwa akifanyia wanadamu wenzie ukatili lakini alimwagiwa tindikali na haohao mnaowaona wanyonge, na sasa anaishi kama panya maana haonekani in Public.

Najua mambo yote kampuni yenu inayofanya hapo kariakoo, hivyo masaa 72 yakipita bila kutafuta suluhu na kumpa huyo kijana Haki yake basi nitaaanika kila kitu hapa hadharani.

Naamini nikishaanika itakuwa aibu kwako na kampuni yako, hata kama Serikali ya sasa haitawachukulia hatua basi dunia itakuwa imejua mnayofanya gizani.

Vilevile mtapoteza heshima mliyonayo kama Silent Ocean kwa watu wasiowajua.

Na taarifa zenu tutamkabidhi Mwenyekiti wa Tume ya Haki Jinai, hata akipelekewa na asichukue hatua kwa kampuni yenu zitakuwa zimeingia kwenye record za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mengi nitaandika baada ya hayo masaa 72 kama utaendelea kuufanya moyo wako mgumu. Naamini juhudi zote za kidiplomasia zimekwishafanyika na umepuuza eti kwa kutamba hivi sasa serikali ni ya kwenu.

Tunakubali na kujua hayo yote brother, ila nikueleze huo unafiki wenu wa kujidai watu wema mbele za wanadamu huku mkiwatendea Watanzania hiyana basi una mwisho wake.
ndugu zangu tayari nimeweka uzi ambao niliahidi, nimeona huenda majini yananilia timing so yanaweza ninyonga kabla ya masaa 72.

Namshukuru Mungu kunipa ujasiri kuyaweka haya machache niyajuayo, hata kama serikali ya sasa itawalinda basi historia hii wataikuta watoto wetu watajifunza na kuweka mifumo mizuri ya kutetea Haki.

 
Back
Top Bottom