GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Huu ujumbe unamuhusu ye yote mwenye access ya kuingia kwenye mikusanyiko inayowakutanisha watawala wakuu wa Afrika!
Siku watakapokutana, naomba uwazamomee na kuwaambia wanalitia sana aibu bara la Afrika kwa kuendelea kulialia kuwa nchi za Magharibi zinaharibu amani barani Afrika. Waambie kuwa Afrika ina eneo kubwa la ardhi na idadi kubwa ya watu kuzidi Umoja wa Ulaya! Iweje Afrika ishindwe kumdhibiti Mbelgiji au Mfaransa kuzichezea nchi zao?
Siku ukikutana nao, wazomee na kuwaambia kuwa ni aibu bara zima la Afrika kuendelea kuendeshwa kama gari bovu na nchi moja iitwayo Marekani, wakati Marekani ni ndogo kwa idadi ya watu na kieneo kuzidi Afrika! Waambie wasikubali siku nyingine kukusanywa kama kondoo Washington na Rais wa USA! Kama Rais wa USA ana shida nao, wawafuate "nyuma" na siyo wao kwenda kujikombakomba kwake!
Tafadhali sana, wazomee bila aibu! Huenda kwa kufanya hivyo, watakasirika na kuamua kuzikataa fedheha, na hivyo kuifuata aibu ya kilichotokea Libya na Congo DRC!
Waambie na kisha uwazomee bila hiyana!!!
Huenda watabadilika!!!