Salamu kutoka US: Kidogo nivunje kiuno kwa mchezo huu wa vijana

Salamu kutoka US: Kidogo nivunje kiuno kwa mchezo huu wa vijana

Prof Janabi wa JF

Senior Member
Joined
Jul 7, 2023
Posts
165
Reaction score
450
Habari zeni wa-TAMISEMI,

Katika harakati zangu huku kwa Biden nikakutana na vijana wanacheza mchezo wa hiki kidude. Nikaona mtu mweusi hashindwi kitu. Nikaomba na mimi niwaoneshe jinsi wabantu tunafanya.

Hawakuwa na hiyana, wakanipa hicho kidude, nikataka kufanya hizo flips kama wao. Ya kwanza ikagoma nikarudia mara kadhaa ikawa nakaribia kupatia.

Basi ile time napatia kiliondoka kwa speed, nikajisogeza kwa mbele kubalance wapi...

Kuja kukaa sawa kitambi kiko kwenye hicho kidude mdomo upo kwenye sakafu, vidamu kwa mbali... nikasema naam michezo na umri.

Ila nishakinunua hicho kidude naendelea na zoezi maeneo salama.

Muishi salama enyi watamisemi
 
Back
Top Bottom