Salamu kwenu Atheist wa Jamii Forums

Logical non sequitur fallacy.

Mtu ambaye hana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote akishindwa kujidhihirisha hakuna cha ajabu hapo, hakuna kitu ambacho hakina logical consistency.

Huyu mtu hana uwezo wote, hana ujuzi wote, hana upendo wote, inawezekana kashindwa kujidhihirisha kwa sababu hana uwezo wa kujidhihirisha tu, hajasema ana uwezo wote.

Mnaposema kuna Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, Mungu huyo hana excuse ya kutojidhihirisha.

Kwa maana mnasema ana uwezo wote, ana ujuzi wote, ana upendo wote.

Kwa nini hajajidhihirisha kuwa yupo kwa njia ambayo kila mtu atajua bila shaka atumalizie hii mijadala ya kila siku na vita za kidini zisizoisha?
 
Kuna uhusiano mkubwa kati ya kuwa Atheist na kuugua ugonjwa wa akili....
Hata kama hii ni kweli.

Kuugua ugonjwa wa akili ni uthibitisho kuwa Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.

Angekuwepo, asingeruhusu viumbe wake anaowapenda waweze kuumwa ugonjwa wa akili.

Kwa akili yako ndogo unaona unawabagaza atheists hapo, ika kiukweli unawaongezea atgeists hoja zao tu kuwa Mungu hayupo.
 
Nilishawahi kusema hawa wasiomwamini Mungu wote wana tatizo la Akili kama kuna mtu anataka kupima ninachoongea kama kuna mmoja unamfahamu anza kumfuatilia hapo ulipo.Yaani mwangalie huyu mjinga anatumia nguvu kubwa kutaka yeye athibishe uwepo wa Mungu eti huyo Mungu aje amthibitishie yeye kwamba yupo sasa hiyo ni kwamba Mungu anashida na wewe au una umuhimu sana kwa nani sasa ?Hata huyo Rais Samia ukimvunjia heshima yake hatokuja yeye kukushughulikia na uwenda usimuone kabisa iwe mahakamani au popote pale ila utashughulikiwa ila haiondoi kwamba yeye hana nguvu kisa tu hajajitetea mwenyewe Sisi tupo kwa ajili ya kuwa machawa wa Mungu kwa vile sisi ni Mali yake kama haumini maneno yangu nenda pale magogoni Ikulu pale kamtukane Rais uone atakuja yeye kukujibu au ni nini kitatokea.
 
Nikishaona mtu hajui tofauti ya "ajidhihirishe" na "hajidhihirishe" tu nakosa nguvu ya kuendelea kujadiliana naye kimantiki.

Huyu ni mtu ambaye hata kuandika herufi za Kiswahili tu ni mgogoro.

Sasa huyu kweli naweza kumpa link ya essays za Bertrand Russell tujadili falsafa ya dini kimantiki na kupangua logical fallacies?
 
Elon Musk kumkubali Mungu hakuleti ukweli kuwa Mungu yupo. Hiyo inaitwa fallacy (kutumia ulaghai ili hoja ikubalike). Uwepo wa Mungu unategemea sana "correct arguments"!
 
Hujaelewa vizuri sijasema Elon ni Mtheolojia.

Na pia Atheists wengi ninao wazungumzia ni hawa wa Tanzania
na Afrika ambao wameacha kumuamini Mungu kisa wamesoma,

wamepata exposure na wengine wamefanikiwa kidogo kiuchumi.

Ndio nikauliza nyie ni zaidi ya Elon Musk ambaye ni mwana
sayansi na tajiri vitu ambavyo vingem tempt kusema hakuna
Mungu. Yeye nimemtumia kama mfano tuu wapo wengine wengi
 
Huyo Mungu kama yupo, Kwa nini aliumba binadamu wasio mwamini?

Huyo Mungu, Alishindwaje kuumba binadamu wema tu watakao mtii na kumwamini siku zote na wakati wote?

Hivi huyo Mungu ana jielewa kweli?
Hivyo ulivyo ndivyo imetakiwa kuwa hivyo ungeumbwa tofauti na hivyo usingeona maana ya maisha kwa sababu hicho unachokifikilia tayari kipo Mungu ameumba Malaika wao wako hivyo unavyotaka wao muda wote wako limited tofauti na wewe unafanya unachotaka Alafu akakupa Akili ikuongoze sasa hicho ndo kitu wewe umekikosa.
 
Hata Wana wa Israel walimwambia Musa wanataka wamuone Mungu,Mwishowe , wenyewe walimwambia Musa chochote utachoambiwa huko tutakufanyia kazi! Kambi ya jeshi tuu unaogopa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…