Salamu kwenu Atheist wa Jamii Forums

Salamu kwenu Atheist wa Jamii Forums

Nikishaona mtu hajui tofauti ya "ajidhihirishe" na "hajidhihirishe" tu nakosa nguvu ya kuendelea kujadiliana naye kimantiki.

Huyu ni mtu ambaye hata kuandika herufi za Kiswahili tu ni mgogoro.

Sasa huyu kweli naweza kumpa link ya essays za Bertrand Russell tujadili falsafa ya dini kimantiki na kupangua logical fallacies?
Binafsi sijadiliani na machizi hivyo ulivyoviandika ni mawazo ya Machizi waliopita kabla yako.
 
Kupumua kwangu kuna husiana vipi na huyo Mungu?

Kwanza thibitisha uwepo wa huyo Mungu, yeye kama yeye.

Sio kurukia kusema mifumo yangu na kupumua kwangu ni Mungu.

Hakuna Mungu anaye nifanya nipumue.

Mungu hajawahi kuwepo, hayupo na hatakaa awepo.

Nikisha sadiki yeye inamsaidia nini?

Huyo Mungu kama yupo ajitokeze hadharani mwenyewe ajidhihirishe yupo kama ana huo uwezo.
Yaani huko kupumua tuu ni Mungu anakupa maana,huwanyeshea mvua wazuri na wabaya,Huyo Mungu!
 
Logical non sequitur fallacy.

Mtu ambaye hana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote akishindwa kujidhihirisha hakuna cha ajabu hapo, hakuna kitu ambacho hakina logical consistency.

Huyu mtu hana uwezo wote, hana ujuzi wote, hana upendo wote, inawezekana kashindwa kujidhihirisha kwa sababu hana uwezo wa kujidhihirisha tu, hajasema ana uwezo wote.

Mnaposema kuna Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, Mungu huyo hana excuse ya kutojidhihirisha.

Kwa maana mnasema ana uwezo wote, ana ujuzi wote, ana upendo wote.

Kwa nini hajajidhihirisha kuwa yupo kwa njia ambayo kila mtu atajua bila shaka atumalizie hii mijadala ya kila siku na vita za kidini zisizoisha?
Hili ni tatizo la Akili.Suruhisho la yote uliyaandika yanatatulika na Akili ya kawaida ya kibinadamu kwangu maneno yako yanadhidi kunithibitishia kwamba kichwa chako ni Box.
 
Hujaelewa vizuri sijasema Elon ni Mtheologia.

Na pia Atheists wengi ninao wazungumzia ni hawa wa Tanzania
na Afrika ambao wameacha kumuamini Mungu kisa wamesoma,

wamepata exposure na wengine wamefanikiwa kidogo kiuchumi.

Ndio nikauliza nyie ni zaidi ya Elon Musk ambaye ni mwana
sayansi na tajiri vitu ambavyo vingem tempt kusema hakuna
Mungu. Yeye nimemtumia kama mfano tuu wapo wengine wengi
Elon Musk ni irrelevant kwenye mazungumzo ya Mungu kuwapo au kutokuwapo.

Kwa sababu hana utaalamu wowote wa kipekee kwenye mazungumzo hayo.

Sema Watanzania mtu akishakuwa na pesa tu mnamshobokea kuwa anajua kila kitu.

Hilo ndilo tatizo lako.
 
Kumbuka mnaamini kwamba Mungu ni muweza wa vyote na mwenye kujua yote tangu mwanzo na hata milele.

Sasa huyo Mungu muweza wa vyote, Alishindwaje kuumba binadamu wema tu watakao mtii na kumwamini siku zote?

Mungu mwenye kujua yote tangu mwanzo na hata milele, Je HAKUJUA kwamba kuna binadamu watakuja kutokumwamini, Awadhibiti na kuwazuia mapema?
Hebu wewe tupe jibu
 
Hili ni tatizo la Akili.Suruhisho la yote uliyaandika yanatatulika na Akili ya kawaida ya kibinadamu kwangu maneno yako yanadhidi kunithibitishia kwamba kichwa chako ni Box.
Sijadiliani na mtu asiyejua tofauti ya "suruhisho" na "suluhisho".

Wewe ni ngumbaru, hujui hata kuandika Kiswahili, utanipotezea muda tu.

Nakupeleka ignore list, kuanzia hapa sitaona post yako yoyote.
 
Uarabuni mbona kuna mabilionea wengi sana na wote hao wanaamini Mungu?

Ulitoa wapi hiyo bias ya kwamba matajiri hawaamini Mungu?
Kwanza nimezungumzia Atheists wa Tanzania na pia

Kufanikiwa sio utajiri tuu ni pamoja na elimu na ufahamu
wa mambo mengi .
 
Nilishawahi kusema hawa wasiomwamini Mungu wote wana tatizo la Akili kama kuna mtu anataka kupima ninachoongea kama kuna mmoja unamfahamu anza kumfuatilia hapo ulipo.Yaani mwangalie huyu mjinga anatumia nguvu kubwa kutaka yeye athibishe uwepo wa Mungu eti huyo Mungu aje amthibitishie yeye kwamba yupo sasa hiyo ni kwamba Mungu anashida na wewe au una umuhimu sana kwa nani sasa ?Hata huyo Rais Samia ukimvunjia heshima yake hatokuja yeye kukushughulikia na uwenda usimuone kabisa iwe mahakamani au popote pale ila utashughulikiwa ila haiondoi kwamba yeye hana nguvu kisa tu hajajitetea mwenyewe Sisi tupo kwa ajili ya kuwa machawa wa Mungu kwa vile sisi ni Mali yake kama haumini maneno yangu nenda pale magogoni Ikulu pale kamtukane Rais uone atakuja yeye kukujibu au ni nini kitatokea.
Kwa nini unahangaika kumwelezea na kumtetea huyo Mungu?
 
Hivyo ulivyo ndivyo imetakiwa kuwa hivyo ungeumbwa tofauti na hivyo usingeona maana ya maisha kwa sababu hicho unachokifikilia tayari kipo Mungu ameumba Malaika wao wako hivyo unavyotaka wao muda wote wako limited tofauti na wewe unafanya unachotaka Alafu akakupa Akili ikuongoze sasa hicho ndo kitu wewe umekikosa.
Kwanza mimi sijaumbwa ni wewe unafosi na kulazimisha mawazo yako uchwara kwamba nimeumbwa.

Hakuna Mungu Aliyeumba kitu chochote kile.

Huyo Mungu mmemtunga vichwani mwenu tu Na wala huwezi kuthibitisha uwepo wake.

Huyo Mungu ana exist kwenye kichwa chako tu, Hayupo katika uhalisia.
 
Hata Wana wa Israel walimwambia Musa wanataka wamuone Mungu,Mwishowe , wenyewe walimwambia Musa chochote utachoambiwa huko tutakufanyia kazi! Kambi ya jeshi tuu unaogopa.
Hizi ni hekaya za vitabuni tu zisizo na uthibitisho wowote ule.

Huyo Mungu kama yupo kweli na ana uwezo kweli, ajitokeze mwenyewe ajiongelee, ajitetee na kujidhihirisha mwenyewe kama ana huo uwezo.

Huyo Mungu wa Musa ni hadithi za kusadikika tu.

Mungu hajawahi kuwepo, hayupo na hatakaa awepo.
 
Yaani huko kupumua tuu ni Mungu
Hakuna Mungu anaye nifanya nipumue.

Ni wewe tu unafosi imani na mawazo yako uchwara kwamba Mungu ananifanya nipumue.

Hakuna Mungu anayefanya kiumbe chochote kile kipumue.

Huyo Mungu hajawahi kuwepo, hayupo na hatakaa awepo.
anakupa maana,huwanyeshea mvua wazuri na wabaya,Huyo Mungu!
Hakuna Mungu anayefanya mvua inyeshe.

Ni wewe tu, unafosi mawazo yako uchwara kusema kwamba Mungu anafanya mvua inyeshe.
 
Back
Top Bottom