Logical non sequitur fallacy.
Mtu ambaye hana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote akishindwa kujidhihirisha hakuna cha ajabu hapo, hakuna kitu ambacho hakina logical consistency.
Huyu mtu hana uwezo wote, hana ujuzi wote, hana upendo wote, inawezekana kashindwa kujidhihirisha kwa sababu hana uwezo wa kujidhihirisha tu, hajasema ana uwezo wote.
Mnaposema kuna Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, Mungu huyo hana excuse ya kutojidhihirisha.
Kwa maana mnasema ana uwezo wote, ana ujuzi wote, ana upendo wote.
Kwa nini hajajidhihirisha kuwa yupo kwa njia ambayo kila mtu atajua bila shaka atumalizie hii mijadala ya kila siku na vita za kidini zisizoisha?