Ahsante mkuu 'Retired', mada ya namna hii niliiwazia muda kitambo. Nashukuru hatimae imewasili.
Sasa nakuomba tuachane na ya uchaguzi ndani ya chama, tuyatazame haya muhimu zaidi yanayo husu nchi yetu.
Sishangai kwamba kwenye orodha hiyo hapo juu hukuweka "Waarabu wa Oman" (wajomba zetu), waliokabidhiwa Gesi ya Ntorya kule Mtwara kimya kimya.
Bila shaka kuna mengi mengine yasiyo julikana kwa sasa, na itakuwa balaa zaidi endapo utawala huu utapata miaka mingine mitano kuendelea kugawa Bandari, kama Bagamoyo na maliasili zetu nyingine kama vichaa!
Kama ulivyo eleza kwa kifupi hapo juu, mada hii itawaingia sana hao walio amua kutunadisha; akina Kafulila na wenzao kwa kupewa tu makombo kwa manufaa yao wenyewe.