Jana nilikuwa nataka kujua mishahara ya vyuo vikuu. Kama Alivyojibu
tang'ana niliishasikia kuwa: Tutorial Assistant (Bachelor's Degree) = 1,800,000 Tshs; Assistant Lecturer (Master's degree) = 2,800,000 Tshs, na Lecturer (PhD/Doctoral) = 3,800,000 Tshs. Lakini kulingana na debate kati ya
mbu wa dengue na
Agogwe nimegundua kuna mambo mawili hayaeleweki:
1. Mishahara ya vyuo vikuu haitegemei elimu ya mtu tu bali uzoefu na kupanda madaraja ya kitaaluma. Mtu akiishafikia Phd Level mshahara wake unaanza kupanda kulingana na tafiti anazofanya - anaanza kuwa lecturer, halafu Seniour Lecturer, halafu Associate Professor halafu Full Professor. Hawa wote wana mishahara tofauti. Professor ni PhD holder ndio maana hujitambulisha kwa elimu yao kwa vile siku za nyuma kulikuwa na maprofesa wasio na PhD. Lakini mshahara wa Professor ni mkubwa (sio chini ya 7m) ukilinganisha na wa lecturer japo wote wana elimu sana. Kwa hiyo
mbu wa dengue anakosea kusema "Kumbe PhD si lolote!". Mshahara hautegemei na elimu tu bali uzoefu na ngazi ya taaluma.
2. Kuwa na mshahara mkubwa kuliko wa Lecturer haina maana kwamba yeye si lolote! Hela sio kila kitu! Kwa mfano mwalimu wa International School anaweza kuwa analipwa sawa na lecturer au senior lecturer lakini kuna tofauti mbili kuhusu kubwa kimapato na mchango wa hawa watu wawili katika jamii:
a) Mapato: Mwl wa International School mshahara wake mara nyingi ni inclusive (salary and other allowances ukiondoa health insurance) lakini kwa lectucturer, mbali na mshahara huo anapata hela nyingi ya ziada kama house allowance, travel allowance, examination/assessment allowance, research supervision allowance, na field practice assessment allowance. Hizi zote ni hela nyingi sana. kwa hiyo hata kama mwalimu wa international school anapata let's say 5 m bado income yake ni ndogo kulinganisha na lecturer kwa uhalisia.
b) Mchango kwa jamii: Mwalimu wa International School au mtu mwingine anaweza kudhani kwa vile anapata mshahara mkubwa zaidi ya lecturer basi yeye ni muhimu zaidi kuliko lecturer katika jamii. Ndio maana
mbu wa dengue akasema "Kumbe PhD si lolote"! Sio kweli kabisa. Hawa watu wana mchango mkubwa sana kwa ustawi wa nchi. Kwanza wataalam wote wa nchi hii hutokana na vyuo vikuu - engineers, technicians, nurses, doctors of medicines, teachers, scientists, accountants, IT specialists, economists, lawyers, n.k. wote hawa uandaliwa na walimu wa vyuo vikuu - kwa hiyo ukisema "PhD si lolote"! unakuwa hujatumia muda kidogo kutafakari. Pili wasomi hawa wana mchango mwingine zaidi ya kufundisha. wengi wao hutumika kama consultants serikalini au katika mashirika ya binafsi (NGOs) kusaidia kutatua changamoto mbali mbali za kijamii kama vile maradhi, kuondoa umaskini n.k. na wakifanya hivyo sio tu wanapata hela ya ziada bali pia mchango wao unakuwa wa maana sana kwa maendeleo ya jamii. Kwa hiyo si sawa kusema kuwa: PhD si lolote!