Salary slip ya mwajiriwa fulani serikalini. Umejifunza nini kutoka kwa huyu kamanda?

Hapo ndo kama ulichukua mkopo, ukajenga nyumba ikaishia kwenye renta sijui wenyewe mnaita😆😆😆, bado utakuwa umepanga na kwa makato hayo kujenga tena subiri miaka 7au mitano deni likipungua. Hapo shughuli ipo, ndo mtu anaanza kuichukia kazi
 
Nilichojifunza:
1. Kama ametumia huo mkopo kujengea nyumba, anailipia Kodi ya 451K na baada ya miaka michache nyumba itakuwa yake.
2. Kama amewekeza kwenye biashara yenye faida zaidi ya 451K kwa mwezi, mapato yake hayajaathirika na baada ya miaka michache atakuwa anajilipa nusu ya mshahara wa serikali.
3. Kama amewekeza kwenye starehe mkopo unamtesa.
 
Dah, kwa kada zetu hizi tofauti na Ewura, BOT, NSSF,PSSSF,BANDARINI,SIASA tena ukiwa super senior emploee/worker kuajiriwa ni utumwa na kujitafutia stress na kifo.
Take home 314k wakati dalali hiyo anapata kwa nusu saa tena kwa kumtembeza mnunuzi au kutangaza biashara ya bosi
 
Kwa haraka haraka huyo ni mwalimu wa daraja E1. Na anaonekana alishamaliza deni la bodi ya mikopo au hakupata kabisa kusomeshwa kwa udhamini wa HESLB kwa hiyo kaenda kajitungua milioni kama 25+ . Yeye ndo anajua kama amekamilisha malengo au bado.
Tukope kwa sababu maalum.
Tukope tukiwa tumeshafanya upembuzi kamili kwa miradi au mradi tunayoifanya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…