Salary slip ya mwajiriwa fulani serikalini. Umejifunza nini kutoka kwa huyu kamanda?

Salary slip ya mwajiriwa fulani serikalini. Umejifunza nini kutoka kwa huyu kamanda?

Nilichojifunza:
1. Kama ametumia huo mkopo kujengea nyumba, anailipia Kodi ya 451K na baada ya miaka michache nyumba itakuwa yake.
2. Kama amewekeza kwenye biashara yenye faida zaidi ya 451K kwa mwezi, mapato yake hayajaathirika na baada ya miaka michache atakuwa anajilipa nusu ya mshahara wa serikali.
3. Kama amewekeza kwenye starehe mkopo unamtesa.
Kama annual increaments na madaraja vingekuwa vinapanda kwa wakati asingeona maumivu ya mkopo
 
Dah, kwa kada zetu hizi tofauti na Ewura, BOT, NSSF,PSSSF,BANDARINI,SIASA tena ukiwa super senior emploee/worker kuajiriwa ni utumwa na kujitafutia stress na kifo.
Take home 314k wakati dalali hiyo anapata kwa nusu saa tena kwa kumtembeza mnunuzi au kutangaza biashara ya bosi
Motivational speakers bana.
 
Mshahara ni mzuri sana tu ttzo lipo kwenye matumizi ili ndo ttZo kubwa la wafanyakaz wanamatumizi fake yasiyoendana na vipato vyao bas
Utakuta iyo lk4 anayokatwa ni mkopo wa gari ya kutembelea tena gar yenyewe ya kijapani haidumu niaka 5 anamaliza mkopo gar imezeeka inabid akope gari ingne
Tujifunze kuishi kulingana na vipato vyetu
 
So udalali unalipa sana
Inategemea unalinganisha na nini. Kwa kulinganisha na huyo mwamba wa TGTS E1 anayeambulia 314 elfu,udalali unalipa.
NB nimechukua mfano wa kazi ya kujiajiri inayodharaulika kwa wengi usichukulie serious kila kitu humu japo kwa salary na takehome hiyo baada ya NMB kufanya yake ni bora kwenda kupiga udalali
 
View attachment 2200989

Basic salary: 940,000
......
Michango/makato yake

Chakuhawata contribution 5000
PSSSF 47,000
PAYE 94,200
Nmb bank loan 42,870,300 (451,266)
NHIF fund employees 28,200
......
NET AMOUNT DUE.. 314,333.68 Tshs
mzigo mzito kuliko uwezo wa kuubeba.Nashauri mshahara wa mbunge upunguzwe waongeze watumishi wa chini kama hawa.
 
Daah Mil 42.

-Chukua Mil 25 peleka UTT utapata zaidi au sawa na ayo makato ya kila mwezi 415k
-Chukua Mil 10 peleka kwenye biashara kama ipo tayari
-Chukua 5 rekebisha nyumbani
-Izo 2 chagua mwenyewe utaipeleka wapi
mzee hiyo 42m ni deni analotakiwa kulipa baada ya kupewa mkopo wake. kwa hiyo net loan aliyopewa inaweeza kua 20-25 m.
 
Hapo ndo kama ulichukua mkopo, ukajenga nyumba ikaishia kwenye renta sijui wenyewe mnaita😆😆😆, bado utakuwa umepanga na kwa makato hayo kujenga tena subiri miaka 7au mitano deni likipungua. Hapo shughuli ipo, ndo mtu anaanza kuichukia kazi
Ukiona hela yako ni ya kuunga unga unatakiwa ufanye hivi
Jenga kijumba kidogo cha kukustri nyuma kwenye kiwanja. Mungu akikujalia ukilipwa mafao ndiyo unajenga nyumba ya mbele na wajukuu wanapata vyumba vyao wakija kusalimia.

Wengine wana bahati wakiwa kwenye vibanda vya uwani mble watoto wao wanamalizia. Si watoto wote wana msaada wengine utawalea mpaka unaingia kaburini.
 
Back
Top Bottom