Salary slip ya mwajiriwa fulani serikalini. Umejifunza nini kutoka kwa huyu kamanda?

Salary slip ya mwajiriwa fulani serikalini. Umejifunza nini kutoka kwa huyu kamanda?

Dah, kwa kada zetu hizi tofauti na Ewura, BOT, NSSF,PSSSF,BANDARINI,SIASA tena ukiwa super senior emploee/worker kuajiriwa ni utumwa na kujitafutia stress na kifo.
Take home 314k wakati dalali hiyo anapata kwa nusu saa tena kwa kumtembeza mnunuzi au kutangaza biashara ya bosi
Kwa hali hii bora tu kuwa dalali! Maana hakuna namna.
 
Real
Watanzania wapumbavu sana, sasa mpo bize kujadili salary slip ya mtu wakati nyie hamkopesheki hata dukani kwa mangi kwasabab hamna kazi au ni kibarua. Mwenzenu ametimiza malengo yake ila nyie mnataka kutuaminisha amefeli... Na hapo baada ya miaka 3 anaweza kukopa tena... Maisha ni kuchagua... Nilichogundua wanao comment negatively ni watu ambao wana stress za maisha, wameStuck hawawez kwenda mbele na umri unakimbia... Guys mtakufa masikini mkiendelea kujadili maisha ya watu.
 
Kimsingi kama kawaida ya JF, mtoa Post alileta hoi post kwa lengo la kuponda utumishi wa umma ila majibu ya wadau mazuri na yanamvunja moyo. Yeye alitaka tuishambulie hiyo 300k anayoipata.
Mimi nina chini ya 500K kwa mwezi kama mshahara wangu toka TGS G sikuwa na loan board na nilikopa zaidi ya 40M ambayo inanisaidia kwenye mzunguko wa zaidi ya 1.2M kwa mwezi toka kwenye Kilimo, ufugaji wa ng'ombe wa maziwa, duka la Pembejeo na bodaboda za mkataba. Kumbuka nilishajenga na nipo kwangu hapo.
mtoa mada kakurupuka watu wan mahesabu yao mpaka kachukua mkopo hongera san
 
Kila mtu anajua mwenyew life analiendeshaje ,
Maisha yanabaki Siri ya mhusika .

Unaweza ukawa unakuja take home nzima nzima na ukawa na life la stress na huyo mwamba akawa na life la furaha.

Kitu kingine watu wanashindwa kuelewa kuwa Deni la mtumishi ni tofaut na Deni la mfanyabiashara ,mtumishi Ana faida nyingi Sana kwenye mikopo maana hata akikosea mkopo wa kwanza Ana chance ya kujiuliza Tena na kusimama imara huku akiwa na faida ya kukopesheka muda wowote Tena.

Wengi hamjawahi kuona mikopo ya wafanyabiashara wasio watumishi nadhan wengi mnaweza zimia Sasa .

Na wafanyabiashara wengi huku mitaan wanadharirika balaa yaan anaweza poromoka toka 100 had 0 kitu ambacho hakipo kwa mtumishi.

Hapa ilipaswa kuongelea namna ya kuutumia mkopo wako kwa usahihi na sio kutisha watu ,na mleta maada kaileta hiyo slip kwa mlengo wa kutisha watu.

Watumishi hapa walipaswa wapewe elimu konki ,maana walio wengi wanakopa kwa lengo la kushindana ,mfano kununua magari ,kuweka samani ndani za gharama huo ndio ujinga ulipaswa ukemewe hapa ,watu wabadirike watu washindane kwa kupambana kimaisha sio kufurahisha watu.
Take home hata isipokua na makato ni Yale Yale tu na huwez toboa Wala kujenga kwa take home yako ya bila mkopo ,tuamke Sasa kukopa sio dhambi ila tukope kwa manufaa yenye tija.
 
Nilichojifunza ni kuona mfuko wa PSSSF hauna hela, tutateseka sana kupata hela zetu, sio kwa contribution hiyo[emoji3064]
Serikali si inaweka 15% Mtumishi anachangia 5%
 
Mikopo ya aina hii ipo mingi Sana..watu tumekopa na bado maisha yanasonga fresh Wala mkopo siusikii ukiniumiza...na Sion gape...
 
View attachment 2200989

Basic salary: 940,000
......
Michango/makato yake

Chakuhawata contribution 5000
PSSSF 47,000
PAYE 94,200
Nmb bank loan 42,870,300 (451,266)
NHIF fund employees 28,200
......
NET AMOUNT DUE.. 314,333.68 Tshs
Ana Akili kuliko Ww. Unayedhani Madeni ni Dhambi wakati kuna Watu Salary Slip yao wanapata 50000
 
Kama nimeelewa vizuri, hiyo mil.42 inahusisha principal na interest. Kwa hiyo inawezekana alikopa mil.25. Halafu inawezekana anakatwa kwa mfumo wa straight balance, ambao unaumiza zaidi. Tunapokopa tuulizie na mfumo wa marejesho. Mfumo rafiki wa marejesho ni reducing balance.
Haya mambo yanahitaji elimu. Wengi wanaingia kichwa kichwa mwisho wanajikuta wapo kwenye mizigo mikubwa inayochukua muda mpaka kuondokana nayo
 
Dah, kwa kada zetu hizi tofauti na Ewura, BOT, NSSF,PSSSF,BANDARINI,SIASA tena ukiwa super senior emploee/worker kuajiriwa ni utumwa na kujitafutia stress na kifo.
Take home 314k wakati dalali hiyo anapata kwa nusu saa tena kwa kumtembeza mnunuzi au kutangaza biashara ya bosi
Wewe unaangalia take home, huangalii huo mkopo?
 
Ndio maana watumishi wanakuwa na hasira sana kumbe mikopo aisee.
 
Kwakweli najaribu kutafakari ni kipi kimetokea. Maana hata kama kachukuwa mkopo mwezi huu, jumla ya deni ilitakiwa isome kama 37M hivi Kwa mkopo wa 7 years.

Hilo deni linawezekana tu endapo NMB wana mikopo ya kufikia miaka 8. Yaani kama amekopa kwa muda wa miezi 96 (miaka 8) hilo deni liko sawa.
Top up hiyo Mkuu.
 
Kwa 940,000/= unawezaje kupata mkopo wa 42,800,000/=? na ile ⅓ ya nachotakiwa kibaki kwenye mshahara wako kimezingatiwa hapa?..


Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
Hii Salary slip siyo genuine in any way,
  • Huyo mtumishi hawezi ku-qualify hiyo pesa
  • Mfumo wenyewe ungekataa automatically ku-capture hayo marejesho sababu una violate rule ya 1/3 ya basic pay as take home
 
Back
Top Bottom