Salary slip ya mwajiriwa fulani serikalini. Umejifunza nini kutoka kwa huyu kamanda?

Salary slip ya mwajiriwa fulani serikalini. Umejifunza nini kutoka kwa huyu kamanda?

Wa hivi ndio wanatusumbua kwenye ajira zao
Kutwa kuomba rushwa hata ukimuuliza kalamu ujaze fomu
Mikopo yao inabidi walipiwe na wengine

Hivi utakuwa na raha gani kama ulizimaliza kwa kununua vitu vya anasa

Na kama alifanyia cha maana well and good ila riba haram
 
Kukopa ni kuzuri kama uliplan kupata faida ya zaidi (au sawa na riba) ya riba unayolipa. Kama mtu alijenga nyumba, apangishe, na mapato kutoka kwenye kodi ya pango atakayolipwa yawe sawa au kuzidi makato ya mkopo anaorejesha kila mwezi (principal + interest), ili kumaintain positive cash flow.
Najaribu tu kuwaza hapa. Anakatwa around 451K kwa mwezi. Nyumba gani hiyo kwa mkopo wa 24M unaweza kuijenga ukapangisha halafu pesa ya pango ulipwe Tsh 451K ? Labda kama ana vyanzo vingine vya pesa Mkuu. Ila kwa huo mkopo haiwezekani.
 
Naomba uchukuwe huu utafiti uchwara niliofanya mie mkuu.

Matokeo ya utafiti wangu uchwara ni kuwa karibia 95% ya watumishi wanaokopa kwa ajili ya biashara, hizo biashara zao hazifanikiwi.

Kama huyo ndugu yupo kwenye hiyo 5% basi ana bahati sana na amshukuru sana Mungu kwa hiyo neema.

Wengi hawafanikiwi. Hizi biashara ni ngumu mtu asikwambie. Halafu weka sasa hawa watumishi biashara zao ni za kuagiza. Hafanyi yeye.
Nakubaliana na wewe kwa Asilimia ndogo kidogo.

Ishu ni ku invest kwenye biashara ambayo yeye mwenyewe hayupo humo. Ndio maana hawatoboi.

Kuna mdau hapo juu, amesema anapata 1.2M kama faida kila mwezi kwenye Biashara aliyowekeza.

Nikamshauri ili afanikiwe zaidi aachane na hiyo ajira ili ajiajiri kabisa, hapo ndio atatoboa.
 
Kukopa ni kuzuri kama uliplan kupata faida ya zaidi (au sawa na riba) ya riba unayolipa. Kama mtu alijenga nyumba, apangishe, na mapato kutoka kwenye kodi ya pango atakayolipwa yawe sawa au kuzidi makato ya mkopo anaorejesha kila mwezi (principal + interest), ili kumaintain positive cash flow.
Hivi inawezekana ?
 
Infwakiti ukikopa benki za tanzagiza 25Million tegemea kulipa 40+ million au zaidi ya 50million kutegemea na duration ya mkopo hasa pale mkopo ukiwa wa muda mrefu. Yaaan interest rate yake ni karibia 100%.
Twafaaaaaaaaaaaaaaa
Aisee shida sana kwa kweli.
 
Nimejifunzaa ukiwa serekali na mshahara kuazia laki tisaa kupanda unaweza kuchukua mkopo kuazia milioni 40,binafsi nikipata huu mkopo nimeanga ufukaraaa,kwa jinsi nilivyo sota kwenye ujasiriamali nazani itazaa Mara 2
Kumbuka principal amount aliokopeshwa sio 42M hiyo 42M ni jumla ya mkopo aliopewa na riba yake. Hapo jama unaweza kuta kapewa kwenye around 20 hadi 24M
 
Daah Mil 42.

-Chukua Mil 25 peleka UTT utapata zaidi au sawa na ayo makato ya kila mwezi 415k
Kama nimeelewa vizuri, hiyo mil.42 inahusisha principal na interest. Kwa hiyo inawezekana alikopa mil.25. Halafu inawezekana anakatwa kwa mfumo wa straight balance, ambao unaumiza zaidi. Tunapokopa tuulizie na mfumo wa marejesho. Mfumo rafiki wa marejesho ni reducing balance.
 
Nakubaliana na wewe kwa Asilimia ndogo kidogo.

Ishu ni ku invest kwenye biashara ambayo yeye mwenyewe hayupo humo. Ndio maana hawatoboi.

Kuna mdau hapo juu, amesema anapata 1.2M kama faida kila mwezi kwenye Biashara aliyowekeza.

Nikamshauri ili afanikiwe zaidi aachane na hiyo ajira ili ajiajiri kabisa, hapo ndio atatoboa.
Unamshauri ujinga.....ajira aliyonayo ndio imemfanya apate hela ya kuwekeza kwenye hiyo shughuli inayompa 1.2 M,akichanganya na mshahara anaopata "kwa sasa" laki 3 ana 1.5M,hapo bado viposho vya hapa na pale,kumbuka halipi kodi ya nyumba......waza tena mkopo ukiisha maana yake mshahara wake tufanye atakunja 900k na biashara itakua imepiga hatua kutoka 1.2m hadi 1.6m,unadhani atakua na pesa ngapi kwa mwezi? kutoboa sio lazma uache kazi,unaweza kuendelea na kazi na biashara zikasonga pia.
 
Watanzania wapumbavu sana, sasa mpo bize kujadili salary slip ya mtu wakati nyie hamkopesheki hata dukani kwa mangi kwasabab hamna kazi au ni kibarua. Mwenzenu ametimiza malengo yake ila nyie mnataka kutuaminisha amefeli... Na hapo baada ya miaka 3 anaweza kukopa tena... Maisha ni kuchagua... Nilichogundua wanao comment negatively ni watu ambao wana stress za maisha, wameStuck hawawez kwenda mbele na umri unakimbia... Guys mtakufa masikini mkiendelea kujadili maisha ya watu.
 
Back
Top Bottom