Salary slip ya mwajiriwa fulani serikalini. Umejifunza nini kutoka kwa huyu kamanda?

Salary slip ya mwajiriwa fulani serikalini. Umejifunza nini kutoka kwa huyu kamanda?

Mkuu acha kukariri B.O.T,NSSF,PSSF mshahara hamna anayeanza na mshahara angalau wa 2M.tena bandari ni 1.5M hapo mwenyewe unafuu ni EWURA ambaye degree holder anaanza na 3.5

Na hata kwenye siasa labda use Mbunge au Waziri-vyeo vingine vyote hakuna chochote utafaidika pia jua fika huko kwenye uwaziri na Ubunge risk zake nazo ni kubwa tena sana-na ukitaka kujua jaribu uone.
Huyo anayeanza na 1.5m ndo tumlinganishe na huyu mwamba wa 0.94m tena TGTS E1 akiwa ameitumikia Jamhuri kwa si chini ya miaka 18?
Huoni baada ya miaka 10 mtu anayeanza na 1.5m atakuwa mbali sana kuliko huyu aliyeko mezani?
 
View attachment 2200989

Basic salary: 940,000
......
Michango/makato yake

Chakuhawata contribution 5000
PSSSF 47,000
PAYE 94,200
Nmb bank loan 42,870,300 (451,266)
NHIF fund employees 28,200
......
NET AMOUNT DUE.. 314,333.68 Tshs
Vote code :- 71B7

Tarehe ya kuzaliwa 2041 - 60 = 1981
17/11/1981

Mbona ni rahisi sasa KUMJUA?

#YNWA
 
Hapo ndo kama ulichukua mkopo, ukajenga nyumba ikaishia kwenye renta sijui wenyewe mnaita😆😆😆, bado utakuwa umepanga na kwa makato hayo kujenga tena subiri miaka 7au mitano deni likipungua. Hapo shughuli ipo, ndo mtu anaanza kuichukia kazi
Atakuwa alikamilisha nyumba bhana.., sio ‘Lental’
 
Ile idea ya kununua bonds ikupate uwe na nyumba tatu, moja unaishi na mbili zinakupa laki saba kila mwezi. Ukitoa matengenezo unaweza kuwa na laki tano. Hii pesa na bado uwe unapata interest ya bonds zako BOT na una pension ya kila mwezi. Unaweza kumudu bia mbili kila jioni.
Definitely, unaweza kuishi na mwenza quite comfortably. Sasa wale omba omba ni mtihani.

Nyumba simple za kupangisha hata room moja moja zinaleta hela nyingi monthly. Hata ujenzi wake ni rahisi sana
 
Dah, kwa kada zetu hizi tofauti na Ewura, BOT, NSSF,PSSSF,BANDARINI,SIASA tena ukiwa super senior emploee/worker kuajiriwa ni utumwa na kujitafutia stress na kifo.
Take home 314k wakati dalali hiyo anapata kwa nusu saa tena kwa kumtembeza mnunuzi au kutangaza biashara ya bosi
Hayo ameyasema vizuri sana bwana Robert Kiyosaki kwenye kitabu chake cha Rich Dady's Cash flow Quadrant...
 
Kimsingi kama kawaida ya JF, mtoa Post alileta hoi post kwa lengo la kuponda utumishi wa umma ila majibu ya wadau mazuri na yanamvunja moyo. Yeye alitaka tuishambulie hiyo 300k anayoipata.
Mimi nina chini ya 500K kwa mwezi kama mshahara wangu toka TGS G sikuwa na loan board na nilikopa zaidi ya 40M ambayo inanisaidia kwenye mzunguko wa zaidi ya 1.2M kwa mwezi toka kwenye Kilimo, ufugaji wa ng'ombe wa maziwa, duka la Pembejeo na bodaboda za mkataba. Kumbuka nilishajenga na nipo kwangu hapo.
Hongereni watumishi wa umma, hakika mnaenjoy maisha!
 
Sisi watumishi wa serikali ndo tunaelewa tunaishije,inshort sijui kwa kada za kawaida kama ualimu na udaktari lkn serikalini kwenye mashirika ya umma ns wizarani watu hatuishi kwa mishahara,mishahara ni kwa ajili ya kukopea tu,
Huo mshahara haujainclude ;
-over time ambayo mara nyingi huwa ni kianzia siku 20 kwa mwezi kwa rate ya kuanzia 30,000 kwa ofisa ambayo mtu anakuja 600,000,hiyo haikatwi kodi na ni fixed ipo kwnye standing order ya taasisi,
-kuna posho za vikao ambapo rate ni 100,000 kwa kikao na ofisa haipiti siku ukakosa kikao au kwa uchache walau kwa wiki una vikao vitatu,
-kuna madokezo ya posho,asilimia kubwa ya kzi serikali tunaandikia posho,kazi hiyohiyo niliyolipwa kikao pia naiandikia posho na jina la kwanza ktk dokezo la posho ni la mpitishaji malipo na wahasibu walipaji ambapo rate huwa ni kuanzia laki kwa siku,kama nimeandika kazi imefnyika kwa siku 7 nakunja laki 7 isiyokatwa kodi,etc,
Sijainclude safari,transport allowance,meal allowance etc,
Inshort mtumishi wa umma wa kwenye mashirika mengi na wizara hawaishi kwa mshahara,kwenda leo kazini kurudi na milipn 2 kawaida hapo nje ya rushwa na 10percent!1
 
Konda na dereva wa dala dala ..... 20-30k kwa sikuuu, net take home 900k
Acheni kuwaza juu juu

Unajua konda na dereva wanapata shida gani barabarani
Masaa ya kazi zaidi ya 12 kila siku ila mtumishi akizidisha analipwa

Semina ngapi
Na mambo mengi ambayo kuna taasisi hata mshahara unaweza usiutegemee tena kama kungekua na uwezekano wa kukopea wotee wengine wangekopea
 
Ukute kwenye hiyo 42m loan plus interest mwamba aliambulia 24m tu. Daah maisha sio fare kabisa
 
View attachment 2200989

Basic salary: 940,000
......
Michango/makato yake

Chakuhawata contribution 5000
PSSSF 47,000
PAYE 94,200
Nmb bank loan 42,870,300 (451,266)
NHIF fund employees 28,200
......
NET AMOUNT DUE.. 314,333.68 Tshs
Hiyo 42+M wamemkopeshaje kwanza?
Huku ni kusababishiana mtu kuichukia kazi isee!
 
Kimsingi kama kawaida ya JF, mtoa Post alileta hoi post kwa lengo la kuponda utumishi wa umma ila majibu ya wadau mazuri na yanamvunja moyo. Yeye alitaka tuishambulie hiyo 300k anayoipata.
Mimi nina chini ya 500K kwa mwezi kama mshahara wangu toka TGS G sikuwa na loan board na nilikopa zaidi ya 40M ambayo inanisaidia kwenye mzunguko wa zaidi ya 1.2M kwa mwezi toka kwenye Kilimo, ufugaji wa ng'ombe wa maziwa, duka la Pembejeo na bodaboda za mkataba. Kumbuka nilishajenga na nipo kwangu hapo.
TGS G kuwa na take home ya chini ya laki 5 kisheria haiwezekani mana ni lazima ubakie na 1/3 ambayo sio chini ya laki 5. Hapa utakuwa umetudanganya kidogo Afisa.
 
Back
Top Bottom