Tetesi: Salim Abdallah ‘Try Again’ katika jaribio la kumng’oa Mo Dewj Simba!

Eeeeh bwana eeh. Tatizo watu wasiojua mambo wanabisha kiushabiki, huko Simba kumekucha.
Hahahahaha..mie huwa nasoma nakuacha, ujue niko nao karibu sana baadhi ya walikua viongozi..Simba kwa moto kitambo tu..wkt wa. Uchaguzi nilikua upande fulani hivi hivyo najua upande ule mpk sasa bado haujarudhika wao kuwa mbali na timu
 
Mtifuano huo
 
Vita imepamba moto.
Yah ila chamsingi kama atafanikiwa kumng'oa Mo basi ahakikishe Bakhresa anaingia.
Lakini napata ukakasi kidogo, huyo Bakhresa ni mmiliki wa Azam football club.
Itakuaje hapo kumiliki hisa kwenye timu nyingine???
Taratibu za soka letu kwenye hilo zinasemaje?
 
Lakini mimi mbona nimeelewa tofauti? Kwani Nkwabi alikuwa mwenyekiti kabla ya Mangungu au kabla ya Try Again?
Hivyo ni vyeo viwili tofauti.
Mkwabi alikuwa mwenyekiti wakuchaguliwa. Ilipokuja suala la mabadiliko yeye akapishana na Tajiri hasa ktk 51% ambayo ndio ya wanachama..Tajiri akamuundia zengwe tena zengwe hasa akajitoa...kipindi chake cha uongozi..Try Again...Mlamu Ng'ambi .dr hasan ..Hans pope , kasim dewj walikua wajumbe wa bodi ...baada ya kupishana na tajiri na kujiondoa ...ukafanyika uchaguzi wa uliomuweka Mangungu..na Tajiri akaamua kuwa rais wa heshima...Mwenyekiti wa bodi akampa try again..wale wajumbe wote wa bodi iliyokua ya Mkwabi wakaondolewa ..Tajiri akateua wajumbe wapya ambao ndio wako mpk sasa
 
Katiba yao ndo tatizo inataka waekezaj watatu katika zile asilimia 49 sasa mafahali wawili hawawezi kaa sehemu moja

Hata akija bakharesa machakato bado utakua ni mgumu
Mbona sisi Yanga tumeshakubaliana mchakato ukianza tutakuwa na wawekezaji watatu na tayari Rostam ameshaonesha nia na hili haliwezi kuwa tatizo pale.

Shida pale Simba Mo hawezi kukubali kugawana zile shares, ndio maana anahaha kukwamisha mchakato mpya.
 
Ufafanuzi umeshatolewa hapahapa kwenye huu uzi Mkuu, ngoja niitafute hiyo post nikutag.
 
Serekali inakosea hawa matajirk ni maadui huku duniani unalazimishaje wawe wa tatu
Hili ni kosa ile timu apewe mo kwa asilimia 100 kama akitaka hio ndo suluhisho
 
Na ndio tatizo..kifupi Mo kawageuka wenzie FoS kiasi kwamba akaligawq kundi ili afanikiwe mipango yake..ila watoto wa mjini wanamkazia maana nao wanajua ulaji wa ktk soka
 
Hivi angekuwepo Hans Pope hii vita ingekuwaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…