Shin Lim
JF-Expert Member
- Mar 27, 2012
- 7,837
- 14,198
Pale pana supamaketi inaitwa Nkwabi.Huwezi kuamini nimeishi pale na huyo mmiliki nilikuwa namjua ila sasa hivi nimemsahau!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Pale pana supamaketi inaitwa Nkwabi.Huwezi kuamini nimeishi pale na huyo mmiliki nilikuwa namjua ila sasa hivi nimemsahau!
Hahahahaha..mie huwa nasoma nakuacha, ujue niko nao karibu sana baadhi ya walikua viongozi..Simba kwa moto kitambo tu..wkt wa. Uchaguzi nilikua upande fulani hivi hivyo najua upande ule mpk sasa bado haujarudhika wao kuwa mbali na timuEeeeh bwana eeh. Tatizo watu wasiojua mambo wanabisha kiushabiki, huko Simba kumekucha.
Nkwabi au Mkwabi?Pale pana supamaketi inaitwa Nkwabi.
Mtifuano huoView attachment 2966280
Moto unawaka SSC! Ni vita kubwa!
Klabu ya Simba ipo katika kipindi kigumu cha vita inayozidi kukomaa kila uchwao baina ya Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi ya Simba Salim Abdallah Muhene ‘Try Again’ dhidi ya ‘Rais wa heshima’ wa Simba Mohamed ‘Mo’ Dewj.
Wawili hao walianza kukosa maelewano baada ya Mo Dewj kuhamisha makazi yake nchini ambapo taarifa za uhakika ni kwamba anaishi Dubai hadi hivi sasa.
Baada ya Mo Dewj kuhamisha makazi uwekezaji wake Simba ulisuasua, ikitaarifiwa kumuachia mzigo mkubwa wa uendeahaji timu Try Again ambao ulimuelemea!
Try Again alijitahidi kadiri ya uwezo wake baada ya ‘tajiri’ kujitenga ‘kiaiana’, akihaha huku na huko kutafuta namna ya kuinusuru Klabu ya Simba ambayo kwa msimu wa tatu mfululizo imekuwa na matokeo ya kusuasua. Jitihada zake hizo zikizaa matunda kwa kiasi kisichoendana na kipindi ambacho muwekezaji alikuwa ameshikilia usukani.
Try Again adhamiria mapinduzi, amlenga Said Salim Bakhressa!
Baada ya Try again ‘kususiwa’ timu na muwekezaji Mo Dewj, Try Again aliona uwezekano wa kupindua meza, na kama ilivyo ada ya wafanyabiashara wakubwa kuwa na jicho angavu la udhia, S.S Bakhressa hakusita kupenyeza rupia!
Vita kubwa iliyopo hivi sasa ni Try Again aliyeko kwenye mikakati thabiti ya kumpindua Mo Dewj kama muwekezaji kisha nafasi hiyo apewe muwekezaji asiye na ‘mbambamba’ S.S. Bakhressa, huku Mo Dewj nae akiwa katika mipango ya kujidhatiti kushikilia nafasi yake hiyo adhimu ambayo huitumia mara nyingi kama kielelezo cha mali zake (SSC)
Serikali yakoleza vita!
Hivi karibuni, Serikali imetoa agizo la kuanzishwa upya kwa mchakato wa undeshwaji wa kisasa kwa klabu ya Simba. Kama mtakumbuka vyema mchakato huo ulioanza miaka kadhaa nyuma, haukuwahi kukamilika.
Serikali imetoa agizo hilo baada ya kujidhihirisha kuwa mchakato wa awali ulikuwa na makosa mengi, hivyo ulikuwa batili ukikosa uhalali.
Agizo hilo limekuwa chachu kwa Try Again na timu yake, kwani endapo ukifanikiwa kuanza kuna uwezekano mkubwa wa S.S. Bakhressa na wawekezaji wengine kujitokeza na kushika hatamu katika hisa, huku ikielezwa kwamba Mo Dewj atarudishiwa fedha zake alizolipia katika mchakato uliohuishwa ambako alijitwalia hisa 49% za umiliki wa klabu ya Simba.
Mo Dewj atupa shilingi mechi ya Yanga!
Hii ni tahadhari kwa Klabu ya Yanga, Hersi na wenzio kama hamjaipata nawapa hii…
Mo Dewj amejipanga kuitumia mechi ya tarehe 20/04/2024 dhidi ya Yanga kama turufu yake ndani ya Simba.
Mo Dewj ambaye inaarifiwa ametenga fungu ‘nono’ kuhakikisha Simba inashinda mechi hiyo, amejipanga sawia na mkakati wake huo ambao tayari ameshaanza utekelezaji.
Mkakati huu wa Mo ni kwamba endapo Simba ikishinda mechi hiyo, atafanikiwa kurudisha imani na mapenzi kwa mashabiki, hivyo kutumia hilo kama zengwe la kuwang’oa Try Again na Mangungu pale Simba.
Kila mmoja ana mpango kazi!
Try Again ambaye hapo awali alitumia ‘janja janja’ kuwang’oa aliyekuwa CEO wa Klabu bibie Barbara na Rweyemamu ambaye alikuwa meneja wa timu kwa ‘kuwachonganisha’ na muewekezaji Mo Dewj, anahaha kulinda maslahi yake kwani endapo Mo Dewj akishinda vita hii (Kwa Simba kushinda dhidi ya Yanga) amepanga kuwarejesha Barbara, Rweyemamu ambaye hivi sasa yupo Kikosi B na aliyekuwa Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi ambaye alijiengua Nkwabi.
Try Again ambaye wameungana na Mangungu kumuhujumu Mo Dewj, nao hawako nyuma. Wanatumia turufu yao ya ‘ujanja wa mjini’ kuhakikisha Mo Dewj anang’oka Simba kwa namna yoyote!
Inaarifiwa hata agizo la kuanza upya kwa mchakato wa uendeshaji wa kisasa wa timu umechagizwa na ‘connection’ za Try Again pamoja na S.S.B na mpaka hivi sasa mpango wao ‘umetiki’.
Je, nani ataibuka mshindi katika vita hii? Ni ‘watoto wa mjini’ Salim Abdallah, Try again au tajiri Mo Dewj?
Ni mimi na chanzo changu nyeti,
Nifah.
Ulikuwa team Wakili? 😀😀Hahahahaha..mie huwa nasoma nakuacha, ujue niko nao karibu sana baadhi ya walikua viongozi..Simba kwa moto kitambo tu..wkt wa. Uchaguzi nilikua upande fulani hivi hivyo najua upande ule mpk sasa bado haujarudhika wao kuwa mbali na timu
Katiba yao ndo tatizo inataka waekezaj watatu katika zile asilimia 49 sasa mafahali wawili hawawezi kaa sehemu mojaHebu ngoja tuone huo mchakato mpya itakuwaje, ila ni kama Mo akishindwa hii vita niliyowaletea habari yake.
Akishinda amejipanga kuuzuia.
Hahahaha...mimi huwa nafanyaga nao kazi maalumu,🤣🤣. Kwa wakati maalumuUlikuwa team Wakili? 😀😀
Ni Mkwabi, nilikosea kuandika.Nkwabi au Mkwabi?
Yah ila chamsingi kama atafanikiwa kumng'oa Mo basi ahakikishe Bakhresa anaingia.Vita imepamba moto.
Mkwabi alikuwa mwenyekiti wakuchaguliwa. Ilipokuja suala la mabadiliko yeye akapishana na Tajiri hasa ktk 51% ambayo ndio ya wanachama..Tajiri akamuundia zengwe tena zengwe hasa akajitoa...kipindi chake cha uongozi..Try Again...Mlamu Ng'ambi .dr hasan ..Hans pope , kasim dewj walikua wajumbe wa bodi ...baada ya kupishana na tajiri na kujiondoa ...ukafanyika uchaguzi wa uliomuweka Mangungu..na Tajiri akaamua kuwa rais wa heshima...Mwenyekiti wa bodi akampa try again..wale wajumbe wote wa bodi iliyokua ya Mkwabi wakaondolewa ..Tajiri akateua wajumbe wapya ambao ndio wako mpk sasaLakini mimi mbona nimeelewa tofauti? Kwani Nkwabi alikuwa mwenyekiti kabla ya Mangungu au kabla ya Try Again?
Hivyo ni vyeo viwili tofauti.
Mbona sisi Yanga tumeshakubaliana mchakato ukianza tutakuwa na wawekezaji watatu na tayari Rostam ameshaonesha nia na hili haliwezi kuwa tatizo pale.Katiba yao ndo tatizo inataka waekezaj watatu katika zile asilimia 49 sasa mafahali wawili hawawezi kaa sehemu moja
Hata akija bakharesa machakato bado utakua ni mgumu
Hahahahaha..ni ktk kuweka mambo sawa RafikiSawa Mkuu.
Mi nashukuru umenisaidia kuwatoa tongotongo wadau hapa kwamba habari ni ya kweli.
Ufafanuzi umeshatolewa hapahapa kwenye huu uzi Mkuu, ngoja niitafute hiyo post nikutag.Yah ila chamsingi kama atafanikiwa kumng'oa Mo basi ahakikishe Bakhresa anaingia.
Lakini napata ukakasi kidogo, huyo Bakhresa ni mmiliki wa Azam football club.
Itakuaje hapo kumiliki hisa kwenye timu nyingine???
Au taratibu za soka letu kwenye hilo zinasemaje?
Serekali inakosea hawa matajirk ni maadui huku duniani unalazimishaje wawe wa tatuMbona sisi Yanga tumeshakubaliana mchakato ukianza tutakuwa na wawekezaji watatu na tayari Rostam ameshaonesha nia na hili haliwezi kuwa tatizo pale.
Shida pale Simba Mo hawezi kukubali kugawana zile shares, ndio maana anahaha kukwamisha mchakato mpya.
Na ndio tatizo..kifupi Mo kawageuka wenzie FoS kiasi kwamba akaligawq kundi ili afanikiwe mipango yake..ila watoto wa mjini wanamkazia maana nao wanajua ulaji wa ktk sokaMbona sisi Yanga tumeshakubaliana mchakato ukianza tutakuwa na wawekezaji watatu na tayari Rostam ameshaonesha nia na hili haliwezi kuwa tatizo pale.
Shida pale Simba Mo hawezi kukubali kugawana zile shares, ndio maana anahaha kukwamisha mchakato mpya.
Hivi angekuwepo Hans Pope hii vita ingekuwaje?Mkwabi alikuwa mwenyekiti wakuchaguliwa. Ilipokuja suala la mabadiliko yeye akapishana na Tajiri hasa ktk 51% ambayo ndio ya wanachama..Tajiri akamuundia zengwe tena zengwe hasa akajitoa...kipindi chake cha uongozi..Try Again...Mlamu Ng'ambi .dr hasan ..Hans pope , kasim dewj walikua wajumbe wa bodi ...baada ya kupishana na tajiri na kujiondoa ...ukafanyika uchaguzi wa uliomuweka Mangungu..na Tajiri akaamua kuwa rais wa heshima...Mwenyekiti wa bodi akampa try again..wale wajumbe wote wa bodi iliyokua ya Mkwabi wakaondolewa ..Tajiri akateua wajumbe wapya ambao ndio wako mpk sasa