Tetesi: Salim Abdallah ‘Try Again’ katika jaribio la kumng’oa Mo Dewj Simba!

Kukudanganya vibaya mnooo Mo ndo aliyemteua Try Again hivo akijua anafanya hayo anao uwezo wa kumtoa mda wowote mtu ambae ungesema anafanya zengwe habar yako iwe na maana labda Ngungu boy pole sana aise
Huna unachokijua wewe, huyo Mo sasa hivi analazwa na viatu na Try Again.

Mangungu wameungana na Try Again, sio vita rahisi kwa Mo.
 
binafsi naitaza hivi!


simba wamedisclose some informations ili kuleta gilibu kwenye daby ya kko tarehe20, mean watu wafocus kwenye discussion za Mangunga, na mo wasahau ajenda ya msingi..



hizi wanaita siasa za mpira ni sawa na siasa za nchi tu kama mnajambo fulani so hot! kunatengezwa jambo jingine na vile waandishi wanapenda kudandia kwa mbeleee woote wanahama then mambo yanabalance kuja kurudi mambo yamepita....



cha msingi now tufocus kwenye match ya Deby then tukimalizana huko tuje sasa tujue nani ni nani!? hayo mambo yameanza mda, kwanza alianza msemaji simba, 'ohooo wanaokwenda uwanjani wawe na Roho ngumu', hatujakaa sawa, akaja mshabiki mmoja akasema timu imeachiwa msemaji, viongozi wameenda Dubai, ikatrend kidg ikaonekana imevubaa ikaja kwamba tarehe 20, baada ya match simba hata ikifungwa 1 mashabiki na viongozi wanakikao wakiwa uwanjani, hatujakaa sawa wanakuja na hii tena.....


anyway tujipe mda tarehe 20 c mbali wanasimba wana jambo lao, kwa matokeo yoyote yale tuwe na subra. cha kuzingatia tumalizie match, kwamba simba inatafuta kushinda na yanga inatafuta ubingwa match moja malengo tofauti ....



kwa hyo kwa sasa viongozi wa simba wasiwazubaishe wanachama wala yanga wasizubae kwa taarifa za mitandao na kuwa ajenda ya kila mmoja ibaki kwenye reli baada ya tarehe 20 saa1 jioni sasa tuje tujadili ajenda zote hapo juu


Mr
Bon
 
Try again amesha jiuzuru nyazifa alizonazo simba na mwanamama amerudi

Nazani kikao kilicho fanyika ktk ofisi za mo kilieleza haya

Alipost pia ktk IG yake

Kama kumbukumbu zangu zipo sawa lakini... una weza jirizisha pia kupitia IG ya muwekezaji
 
Ukweli ni kwamba kama sio SSB kupewa Simba basi bado mtaendelea kumuhitaji Dewj pamoja na drama zake zote hizo.
Hili halipingiki ila
SSB tayari ana Azam FC

Lakini kama ni kweli ameweka nia ya kuwepo simba basi kuna mpango anao wa kukwepa hicho kikwazo cha umiliki wa Azam Fc

Kwa mara ya kwanza naomba timu yangu ifungwe ili ilete chachu ya mabadiliko maana tukishinda hapa tena lawama robo fainali ijayo kama tutafika😁👍🏽
 
Hataweza mbele ya serikali? Serikali ndio imetoa agizo hilo, mchakato ukianza anarudishiwa pesa zake aanze upya.
Bakheresa ana miliki timu tayari ambayo ni azam sheria za fifa haziruhusu iko kitu ni kosa

Washabiki na viongozi wa wanajaribu kutumia short cut kutatua changamoto zao kitu ambacho sio sahihi
 
Mo hisa zake kwa hiari yake atauza ila huwezi mlazimisha
Mkuu unaelewa taratibu sana. Ngoja nikufafanulie kwa mara ya mwisho…

Serikali wameagiza kuanza kwa mchakato mpya, kwa maana hiyo mchakato uliompatia hisa 49% Mo ni batili, hivyo endapo mchakato mpya utaanzishwa ni kwamba Mo atarudishiwa fedha zake alizotoa kwa ajili ya kununua hizo hisa zake.

Hapa suala sio la hiyari ya Mo tena endapo mchakato mpya utaanzishwa, ndio maana yeye kwa kulitambua hilo anafanya awezavyo ili kuzuia mchakato kuanza upya. Ndio hii mechi ya Yanga sasa inapokuja…

Kama hujaelewa basi tena, good day.
 
Mmiliki wa Azam ni mtoto
Miliki wa simba muwekezaji ni baba (kama atakuwa) sizani kama kuna shida

Ni kama umiliki wa timu za taasisi
Timu za jkt
Timu za jwtz huko daraja la kwanza zimejaa
Timu za polisi zipo polisi dom, polisi moro, polisi dsm
Magereza pia wanazo mikoani kama magereza musoma

Timu za halmashauri kama ilivyokuwa timu za kurugenzi (wakurugenzi wa halmashauri)

Timu za ujenzi

Timu za shirika moja la relic Yani reli kigoma, reli morogoro

Nazani kwetu ni kawaida

Pia ndg kumiliki timu ni jambo la kawaida, pale Congo dr kuna Katumbi na ndg yake wana miliki timu na zipo Ligi kuu

Salzburg RB, RB reipzig na RB zingine ni mifano ya umiliki wa taasisi moja au shabihishi
 
Hakuna tatizo wewe kuwa na mtazamo tofauti Mkuu, ni sawa kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…