Tetesi: Salim Abdallah ‘Try Again’ katika jaribio la kumng’oa Mo Dewj Simba!

Mkuu, SSB akikabidhiwa Simba pale akafanya uwekezaji wa maana zikiwemo sajili makini itakuwa balaa.

Sasa hivi Yanga tunatamba sababu ya uwekezaji aliofanya GSM ikiwemo uongozi makini, ukiviondosha hivyo Yanga sio lolote.
 
Mchakato mpya ukianzishwa tu Mo hana chake pale Simba, hizo janjajanja mwisho wake ni huo mchakato.
 
Washabiki wa simba ndo wajinga
Kipindi kile mzee kilimon alipiga sana kelele ila akaonekana ni mamluki na anayeitakia simba mabaya

Na washabiki wa simba hawakutaka kusikia chochote sababu walikua katika mafanikio
Taratibu za asilimia 49 za wawekezaji wanatakiwa kuwa watatu na sio mmoja tokea mwanzon ilikua inajulikana ila kwa sababu simba walikua kwenye mafanikio hukuwaambia kitu

Hata swala la uwanja wa bunju kuitwa mo arena lililamikiwa na mzee kilomon ila alioneka mamluki
Ila ukweli ni kwamba yule mzee aliona mbali sana

Sasa leo mnaimba nyimbo zile zile mzee kilomoni aliyeziimba miaka sita nyuma na akaonekana hamnazo
 
Mzee Kilomoni anatakiwa kujengewa sanamu ya heshima pale Simba.

Hivi unafikiri mpaka kufikia mtifuano ule Mo alishampa ofa kubwa kiasi gani lakini akaendelea na msimamo wake huku akizishikilia hati?
Kama kuna shabiki mzalendo pale Simba ni Mzee Kilomoni.
 
......sijajua ni ipi nafasi ya mashabiki na wanachama hai wa simba katika kuamua mustakabali wa timu, au wamnachukuliwa kama mazuzu tu means hawana impact, baada ya Ferguson kuondoka na timu kuyumba familia ya Glazer imekuwa kwenye pressure kubwa, na jitihada zao kupambania timu zinaonekana licha ya kwamba bahati haipo upande wao.....
.......mashabiki hawawazi kupata pesa wanataka timu bora, Sasa hiyo battle onaonekana wazi hailengi kusaidia timu na ndo maana ni 'pesa against power' na sio matamanio ya mashabiki, hivyo basi kwa kuwa pesa=power basi yeyote atakaeshinda hapa usitegemee atakaa ashughulikie changamoto za simba sc, hili litapita na matatizo yatabaki palepale.......
 
Hii imekaa sawa
Hii imekaa sawa kama mtoto ndo mmiliki
 
Sasa Mkuu, Kama Mangungu ambaye ndiye Mwenyekiti wa Simba akiwakilisha wanachama hana sauti katika vikao, yeye kazi yake ni kufungua na kufunga vikao unategemea nini?
 
Sasa Mkuu, Kama Mangungu ambaye ndiye Mwenyekiti wa Simba akiwakilisha wanachama hana sauti katika vikao, yeye kazi yake ni kufungua na kufunga vikao unategemea nini?
........huko kukosa kwake sauti ndo kunaongeza tatizo au kuzua maswali zaidi, ina maana hisa za wanachama zinaweza kuwa hewa au tunaweza kuquestion upatikanaji wake kama mwenyekiti, lakini ukiachana na Ngungu boy je wanachama by themselves wanaweza kufanya kitu eg kugomea kwenda uwanjani au hata kutishia kurudisha kadi au kususia jezi za msimu mpya etc, inasemekana mashabiki wa upande wa pili hawanaga mzaha timu ikiwa down,.....
 
Hapana Mkuu, hii sio propaganda ni habari ya ukweli kabisa.
Na huyo mtu ambaye ni chanzo changu ni mwanachama hai wa Simba mwenye access na taarifa za ‘ndani’ huko kwenye klabu yao.
Mulikuwa wapi na Ulimpa nini hadi akupenyezee habari nyeti kama hizo?

".............Delila kwa Samson............"
 
Kuna wakati nilikuwa nikitamani kuona threads za michezo zikiwa zinaandikwa kwa weledi namna hii, bila kujaza unazi na ushabiki.

Hongera sana Nifah, umelipa heshima jukwaa na michezo. Umeandika vizuri sana na kufafanua kwa kina hadi nikasahau kama wewe ni Yanga.

Ni kweli Simba tuko kwenye tatizo la kiuongozi na sioni namna nzuri ya utatuzi, kando ya mbinu nyingi za kukomoana na kuonesha umwamba.

Ova
 
Hicho ndicho kilichofanya serikali iagize kurudiwa upya kwa mchakato baada ya kuonekana Mo amejitwalia madaraka makubwa Simba kuliko wanachama ambao ndio wenye hisa nyingi.

Sisi Yanga huwa hatuna mchezo, si unakumbuka kilichomleta Mzee Mpili town kutokea Ikwiriri ni nini? Alikuja kukiwasha baada ya kuona kuna watu wanafanya mchezo timu haisongi mbele ilhali GSM anaweka pesa.
 
Mulikuwa wapi na Ulimpa nini hadi akupenyezee habari nyeti kama hizo?

".............Delila kwa Samson............"
We ni mgeni kwenye habari ninazozileta hapa? Mbona kanipenyezea nyingi tu?

Nimempa moyo wangu.
 
Mwandishi bora ni yule anayeficha mapenzi yake binafsi katika maandishi yake. Nimejifunza haya kutoka kwa mwalimu bora, bado najifunza vingi kutoka kwenye kapu lake lisokwisha maarifa.

Asante b… hii kutoka kwako ni zaidi ya pongezi.
Nashukuru.
 
Mbona unakwepa kujadili hoja iliyopo, unaweza kufungua uzi mwingine wa hoja yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…