Tetesi: Salim Abdallah ‘Try Again’ katika jaribio la kumng’oa Mo Dewj Simba!

Tetesi: Salim Abdallah ‘Try Again’ katika jaribio la kumng’oa Mo Dewj Simba!

Kaburu sio tu anajua fitina pia ana jicho la kusajili alimleya Okwi na miaka 27. Kasim Dewji ni tapeli alidanganya Simba kiwejenga msingi wa ghorofa 7 kumbe ni tatu pia alidanganya Ramadhani Was so anaenda Ubelgiji kumbe anamwuza yanga pia ndiye aliyeuza sehemu ya uwanja wa Simba Msimbazi.
Shida ya Kaburu ni ile tabia ya kuuza mechi, na rafiki yake Aveva. Kassim ni shida sana, kaitafuna sana Simba kwa lile jengo la pembeni pale.

Wakati wake wa mkataba wa jezi alikuwa anawapa Simba kati ya miliono 250 hadi 400 tu kwa msimu mzima. Anasingizia piracy kila siku.

Ova
 
Shida ya Kaburu ni ile tabia ya kuuza mechi, na rafiki yake Aveva. Kassim ni shida sana, kaitafuna sana Simba kwa lile jengo la pembeni pale.

Wakati wake wa mkataba wa jezi alikuwa anawapa Simba kati ya miliono 250 hadi 400 tu kwa msimu mzima. Anasingizia piracy kila siku.

Ova
Kaburu hajawahi kuuza mechi Ila kasim ana tuhuma hizo na ndiyo sababu alikosana na marehemu Sianga
 
Majibu yako yanaonesha wewe ni mcheza miziki ya vigodoro! Unaokoteza habari na kuleta kwenye jukwaa ukidhani watu wote ni wajinga! Na low IQ kama wewe!

Tatizo lako hujawahi kufanya biashara ya maana zaidi ya kuuza madera na mkorogo uko feki uko bongo.

Habari yako aina source wala haina mantiki umetunga mwenyewe upo unakunywa chai na miogo unaona watu wanakuunga mkono kishabiki unaona umeleta habari

Kwa mtu mwenye akili tu atajua wewe ni chenga! Board ya wakurugenzi ya Simba inaundwa na wajumbe kumi na mbili! Na kwa mgawanyo wa wajumbe kutoka simbasc holding company na kutoka kwa mwekezaji!

Mwenyekiti wa boards anachaguliwa na mwekezaji how! Aandae mapinduzi ya boss wake? Inawezekana vipi? Eti dangote na Mzee Salim wanaitaka Simba!

Uongo wa kijinga sana! uyo dangote sidhani hata kama anazijua Simba na yanga!
Ameshindwa kuwekeza kwao ambako ana uwekezaji wa viwanda karibu asilimia 80% aje awekeze Tz ambako wala hana uwekezaji mkubwa zaidi ya kiwanda cha cement!

Yaani unatunga uongo ambao ni vichwa panzi wanaweza kuuamini tu! Dangote kawekeza Arsenal ambako timu ipo kwenye soko la hisa! Tena kwenye nchi ambayo iko proper ambayo uhakika wa pesa yake ipo salama!

Eti aje Simba ambayo hata kwenye soko la hisa haipo! Ambayo hata ligi ya nchi haileweki! Mnafikili dangote ni mfanyabiashara wa ukwaju!

Ingekuwa anataka fame
angedhamini ligi ya uko kwao ambako angepata millege kubwa kwasababu naigeria wana population kubwa ambayo ni faida kwa matangazo.

Kwa faida yako na mbumbumbu wengine hata MO sio mjinga iyo billion 20 kaweka Simba kama deposit kwa kununua Bond za serikali ambayo gawio lake kila mwezi ndio anaipa Simba karibu million 200. Siku akiamua kuondoka Simba anakatisha mkataba na anaondoka na Simba haipati kitu!

MO anaweka hio pesa Simba kama billboard ya matangazo yake nothing else! Hakuna pesa MO anapata kupitia Simba! Zaidi ni billboard! Na anaweza kutumia njia nyingine kufanya matangazo na akaendelea vizuri tu! Kwa wanaojua biashara na watu wa marketing wanaelewa!

Ujiulizi why's gsm hapo yanga ni kit sponsor? Ambae amejigeuza mmiliki kidizaini bila kuweka pesa! Anauza jezi na bidhaa za yanga na kwenye uongozi kamuweka mfanyakazi wake kama chairman? Kwasababu huna akili ya biashara huwezi kuelewa!

Try again Abdala! Ana kampuni ya agency ya clearing and forwarding! unajua kuwa asilimia kubwa ana clear mizigo ya METL ambayo inamuingizia billion of money! Leo useme kuwa anampindua godfather wake?! Stupid nonsense!!

Hivi vilabu vya Simba na yanga vina mashabiki wengi ambao wengi ni masikini tu! Tafuta taarifa za za mabank ambayo yamefanya project hivi karibuni na hivi vilabu ndio utapata jibu! Hakuna biashara ya maana serious investa anaweza kufanya na wapenzi wa hivi vilabu, hakuna investa wa maana atakuja kuweka pesa! Hayo mengine ni propaganda tu!

Muulize gsm biashara ya nguo ni wapenzi wangapi wa yanga wenye cards za benki zenye discount wanaoenda kununua biashara kwake!

Ingekuwa kuna mashabiki wenye hela kwenye hivi vilabu gsm asingekomaa kuuza jezi! Angekuwa sponsor tu na biashara angeiona!
Ila kwakua wengi ni apeche alolo kama wewe ambao mnataka mdhamini awanunulie tiketi muingie uwanjani bure! Mlipiwe safari kwenda kushangilia timu bure! Kuna la maana hapo! Kuna mtu serious hatajitokeza kuweka pesa ya maana?

Ndio maana jamaa anauza jezi angalau asitoke patupu.

Nimekujibu kukutoa tongotongo tu! Najua kunielewa ni ngumu maana sijui hata kama una GPA! Au ndio wale wenye chuki na ndalichako.

Elewa Mtu kama MO anafanya kwa passion tu! Na labda kwa jicho la uko for future!!
Simbasc ingekuwa na faida hao uliowataja kwenye ndoto zako sijui dangote na Mzee Salim hawana haja ya kufanya short cuts unazojitungia wangeita wawakilishi wa MO wanamuwekea pesa mezani wananunua hisa zake biashara inakuwa imeishia! Hio ndio business ya dunia! Kwakuwa wewe upo kwa mtogole uko unauza Madera huwezi kuelewa chochote!
Kwaheri ngoja mimi nibebe box kwa Biden uku.
Ukweli mchungu huu
 
View attachment 2966280

Moto unawaka SSC! Ni vita kubwa!
Klabu ya Simba ipo katika kipindi kigumu cha vita inayozidi kukomaa kila uchwao baina ya Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi ya Simba Salim Abdallah Muhene ‘Try Again’ dhidi ya ‘Rais wa heshima’ wa Simba Mohamed ‘Mo’ Dewj.

Wawili hao walianza kukosa maelewano baada ya Mo Dewj kuhamisha makazi yake nchini ambapo taarifa za uhakika ni kwamba anaishi Dubai hadi hivi sasa.

Baada ya Mo Dewj kuhamisha makazi uwekezaji wake Simba ulisuasua, ikitaarifiwa kumuachia mzigo mkubwa wa uendeshaji timu Try Again ambao ulimuelemea!

Try Again alijitahidi kadiri ya uwezo wake baada ya ‘tajiri’ kujitenga ‘kiaiana’, akihaha huku na huko kutafuta namna ya kuinusuru Klabu ya Simba ambayo kwa msimu wa tatu sasa mfululizo imekuwa na matokeo ya kusuasua. Jitihada zake hizo zikionekana kuzaa matunda kwa kiasi kisichoendana na kipindi ambacho muwekezaji alikuwa ameshikilia usukani.

Try Again adhamiria mapinduzi, amlenga Said Salim Bakhressa!
Baada ya Try again ‘kususiwa’ timu na muwekezaji Mo Dewj, Try Again aliona uwezekano wa kupindua meza, na kama ilivyo ada ya wafanyabiashara wakubwa kuwa na jicho angavu la udhia, S.S Bakhressa hakusita kupenyeza rupia!

Vita kubwa iliyopo hivi sasa ni Try Again aliyeko kwenye mikakati thabiti ya kumpindua Mo Dewj kama muwekezaji kisha nafasi hiyo apewe muwekezaji asiye na ‘mbambamba’ S.S. Bakhressa, huku Mo Dewj nae akiwa katika mipango ya kujidhatiti kushikilia nafasi yake hiyo adhimu ambayo huitumia mara nyingi kama kielelezo cha mali zake (SSC)

Serikali yakoleza vita!
Hivi karibuni, Serikali imetoa agizo la kuanzishwa upya kwa mchakato wa undeshwaji wa kisasa kwa klabu ya Simba. Kama mtakumbuka vyema mchakato huo ulioanza miaka kadhaa nyuma, haukuwahi kukamilika.

Serikali imetoa agizo hilo baada ya kujidhihirisha kuwa mchakato wa awali ulikuwa na makosa mengi, hivyo ulikuwa batili ukikosa uhalali.

Agizo hilo limekuwa chachu kwa Try Again na timu yake, kwani endapo ukifanikiwa kuanza kuna uwezekano mkubwa wa S.S. Bakhressa na wawekezaji wengine kujitokeza na kushika hatamu katika mgawanyo wa hisa, huku ikielezwa kwamba Mo Dewj atarudishiwa fedha zake alizolipia katika mchakato wa awali uliohuishwa ambako alijitwalia hisa 49% za umiliki wa klabu ya Simba.

Mo Dewj atupa shilingi mechi ya Yanga!
Hii ni tahadhari kwa Klabu ya Yanga, Hersi na wenzio kama hamjaipata nawapa hii…

Mo Dewj amejipanga kuitumia mechi ya tarehe 20/04/2024 dhidi ya Yanga kama turufu yake ndani ya Simba.

Mo Dewj ambaye inaarifiwa ametenga fungu ‘nono’ kuhakikisha Simba inashinda mechi hiyo, amejipanga sawia na mkakati wake huo ambao tayari ameshaanza utekelezaji.

Mkakati huu wa Mo ni kwamba endapo Simba ikishinda mechi hiyo, atafanikiwa kurudisha imani na mapenzi kwa mashabiki, hivyo kutumia hilo kama zengwe la kuwang’oa Try Again na Mangungu pale Simba.

Kila mmoja ana mpango kazi!
Try Again ambaye hapo awali alitumia ‘janja janja’ kuwang’oa aliyekuwa CEO wa Klabu bibie Barbara na Rweyemamu ambaye alikuwa meneja wa timu kwa ‘kuwachonganisha’ na muewekezaji Mo Dewj, anahaha kulinda maslahi yake kwani endapo Mo Dewj akishinda vita hii (Kwa Simba kushinda dhidi ya Yanga) amepanga kuwarejesha Barbara, Rweyemamu ambaye hivi sasa yupo Kikosi B na aliyekuwa Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi ambaye alijiengua Mkwabi.

Try Again ambaye wameungana na Mangungu kumuhujumu Mo Dewj, nao hawako nyuma. Wanatumia turufu yao ya ‘ujanja wa mjini’ kuhakikisha Mo Dewj anang’oka Simba kwa namna yoyote!

Inaarifiwa hata agizo la kuanza upya kwa mchakato wa uendeshaji wa kisasa wa timu umechagizwa na ‘connection’ za Try Again pamoja na S.S.B na mpaka hivi sasa mpango wao ‘umetiki’.

Je, nani ataibuka mshindi katika vita hii? Ni ‘watoto wa mjini’ Salim Abdallah, Try again au tajiri Mo Dewj?

Ni mimi na chanzo changu nyeti,

Nifah.

Pia soma
- Tetesi: - Simba imepasuka. Kuna Simba ya Try Again na Simba ya Mo, Kila upande unauroga upande mwingine

Kama Mo atarudishiwa pesa zake na yeye arudishe pesa ambazo amekuwa akibenefits na SSC pamoja na matangazo yake
 
Hahahahah,sasa try again kawekwa pale na mo,afu yeye apambane kumtoa mo.??dah
 
Back
Top Bottom