Just Distinctions
JF-Expert Member
- May 5, 2016
- 3,230
- 6,742
Salum Kikeke ni mmoja wa waandishi wa habari mahiri na wenye uwezo mkubwa wa kuhoji na kwa bahati nzuri kuwahi kwake kufanya kazi BBC kumesaidia kumpa jina.
Lakini baada ya kumfatilia jana katika mahojiano yake na Lissu mbona ghafla nimemuona ni mwandishi wa daraja la chini mno hawezi fikia viwango vya kina mzee Tido Mhando hata chembe! Kwa nini ameporomoka ghafla hivi?
Swali la nia ya kutaka kugombea Urais, Lissu kamjibu sahihi kabisa kikanuni ndani ya Chadema lakini Kikeke katakana kuwa mbona Mrema kaeleza hivi na vile na mbona Msigwa naye kasema vile!
Mtu yeyote makini atajua anachotafuta hapa ni kuonyesha kuna mgogoro wa kugombea ndani ya Chadema.
Hii siyo sifa njema (kutumika) kuhoji ili kutengeneza mtifuano nje ya mfumo.
Kikeke lazima ujitofautishe na watu kama Kitenge. Hao wanaweza kutumika kwa lolote hata kama litasababisha dhiki na vifo kwa wengine ili mradi wao wapate rasilimali za kuwatambia wengine. Hizo huwa za muda tuu. Au nawe umetamani maisha hayo.
Usikute umeshaingia kwenye mfumo! Ila if so, bye bye weledi.
View: https://www.youtube.com/live/e-IRCGgC0KQ?si=gPN9FJdhQfJf19dc
Uandishi wa habari ni kuuliza maswali ambayo watu wanayotaka kusiki, ambayo wangependa kusikia na yale ambayo hukutarajia kusikia
Sasa hukutaka aulize swali hilo aulize nini tena???
Pamoja na kuwa tunafatilia vyombo vya wenzetu huko nje lakini bado tunafumbia macho vingi vinavyoendelea ndani
Unakumbuka Lissu alivyofanyiwa mahojiano katika kipindi cha Hardtalk??
Si ajabu yaoe maswali angeuliza mwandishi wa bongo angeonekana katumwa au katumiwa ilhali ndio uandishi unavyotaka na kitu ambacho kibongo bongo hata Chief Odemba anafanya sana na haonekani kuwa na upande
Tuendelee kupiga kazi