PreGE2025 Salim Kikeke kutoka BBC Swahili hadi kuwa Chawa mkubwa wa Rais Samia

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Mama kashawashika waandishi wengi ili wamsaidie kuusagia kunguni upinzani.
 
Au wanamaanisha chawa ni yule anae kubali tu kwa sababu fulani za kimaslai yake binafsi bila kutazama ubaya wake au uzuri wake kwa mantiki🤔
 
Anaitafuta 70, anataka kustaafu vizuri - hela haijawahi kushidwa kitu, may be kumhuisha mwanadamu tu ndo imedunda mengine yoote inatelezaa
 
Kama ni rahisi hivyo basi na wewe kawe chawa wa mtu yeyote. Yaani Kikeke ulitaka aendelee kuwa mwajiriwa wa BBC ili kukufurahisha wewe usimuite chawa.

Pumbavu kabisa, ukute unaishi kwa shemeji hata hela ya bando unapewa na shemeji yako.
 
Lakini cha kuuchukia huo unaoitwa uchawa ni nini? Kama uchawa unaongeza influence kwenye jamii; kwa nini vyama vyote visiwe na mfumo huo au kubuni mfumo mwingine wenye kuleta influence badala ya kuwatukana hao wanaoitwa chawa?
 
Huyu ni mwandishi wa habari. Huenda huelewi taaluma hii ndo unaona ugeni. Mwambie Pascal Mayalla akudokezee kidogo kuhusu hii taaluma. Kikeke hajakosea popote kwa kufuata misingi ya taaluma yake. Mambo ulizeni wanaojua ili mufaidike.
 
Mimi leo nikimuelewa na kumkubali Samia na kuanza kampeni za siasa kwa sababu naamini kabisa Samia ndiye mtu sahihi, na CCM ndicho chama sahihi, bila uchawa, mtanitenganishaje na machawa?
Totally Chawa pro max
 
Kwa kweli neno CHAWA linapora utashi wa wengine kufanya maamuzi ya kuchagua
 
Kauli zako na matendo yako ndio muamuzi wa kutofautisha baina ya uchawa na political support.

Huwezi kupayuka kama hayawani mama anaupiga mwingi, kitumbua cha mama halafu tuseme una support kisiasa. Hapo unakuwa ni chawa punguani.

Support ya kisiasa huambata na facts na justifications. Sio kusifia mama kaleta mvua.
 
Inamana Samia hamuoni mzee wa propaganda chafu mitandaoni mzee , wanasheria asio msomi, aliye garagazwa vibaya na Kura moja Kawe Pascal Mayalla??Duh!!
 
Uchawa kwa sasa ndio ajira inayolipa zaidi TZ
 
Kikeke katoka mbele kuja kupigishana kelele za uchawa na wamatumbi. Smh
 
Kwa kweli neno CHAWA linapora utashi wa wengine kufanya maamuzi ya kuchagua
Exactly.

Bado mpaka sasa sijapewa jibu la tunawezaje kumtenganisha chawa na mtu anayetumia haki zake za kikatiba na kibinadamu tu kuchagua siasa anazozitaka kifalsafa bila uchawa.
 
Mkuu,

Kwani mtu hawezi ku support kijinga bila kuwa chawa?

Yani mtu aliyezoea ushabiki wa Simba na Yanga, hana elimu, hajui hoja, anataka ku support CCM, ni haki yake, hawezi ku support kijingajinga bila ya kuwa chawa?

Aki support kijingajinga tu tayari ni chawa?

Chawa ni nani? Definition ya chawa ni nini?
 
Kuna ushabiki (huu unaweza hata kuwa wakijinga) Shabiki hatarajii ujira/fidia kutoka kwa kile/yule anaeshabikia. Anaweza kukosa uelewa wa anachoshabikia lakini kwa mapenzi yake akashabikia na pengine hata kutetea upuuzi bila ya kutarajia any form of compensation/gain.

Uchawa ni ile hali ya kuhalalisha upumbavu ambao hata haulalishiki ili tu uonekane bora mbele ya yule unaemhalilishia kwa muktadha wa kutarajia labda utavuna kitu kama fidia/ujira.

Chawa kifasihi ni mdudu mdogo mnyonya damu anaeishi kwenye mwili wa binadamu/mnyama.

Kwa sasa wehu wanaoweka rehani utu wao kwa kusifia hata visivyosifika kwa matumaini ya some sort of monetary/political gain huitwa chawa.

Kwa lugha nyepesi chawa ni mpuuzi aliekuwa radhi kuweka utu wake rehani kwa kusifia/ku support blindly ili tu apate manufaa.

Panapokuwa na matarajio ya kufaidika kwa ku support automatically unatoka kwenye ushabiki na kuwa LICHAWA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…