Salim nakupenda! Kwanini hukunivumilia na unajua nilikuwa mtoto, ukakimbilia kuoa?

Salim nakupenda! Kwanini hukunivumilia na unajua nilikuwa mtoto, ukakimbilia kuoa?

Usiseme hivo,,,

Kuomba ushaurii haina maana kwamba mimi ni Mtoto
Nimeomba kwasababu yamenikaba na nimeona nipate mawazo ya watu mbali mbali
Suala la kuolewa tena mke wa pili ni kubwa sana haswa ukizingatia mimi sio wa dini hiyo

Umri wangu sasa unaruhusu kuwa mke wa mtu
Lakini katika umri huu tena nakutana na hii changamoto unajua ni kwa namna gani navyochanganyikiwa

Na ukiangalia vigezo alivyonavyo mimi ndivyo ninavyovitamani kizuizi kikubwa ni dini,,

Sasa usiniseme hivo jamani nipe ushaurii utakao nifaa

Maana nipo njiapanda kama nataka kama sitaki
Hujajitaji mume bado
Ungekua na uhitaji kweli
Mngefunga ya bomani
Mana ye karidhia we ndio hutaki
Kuwa mke wa pili hutaki
Ndo mana nakuambi huyo Kijana hujampenda


Subiri waje wanaume waliowahi kupendwa wakueleze
Huwezi kataa mpa penzi mwanaume unampenda for years na bado ndoa hutaki
 
SALIM ananifaa sana yaani ingekuwa ni wa dini yangu ningepiga [emoji3581][emoji3581][emoji3581]

He deserve love
Kijana mzuri Sana namaanisha ana roho nzuri mno ndiyo hivyooo….[emoji849]
basi fanya kukamilisha maana tayari umeshafanya maamuzi lkn kama ni ushauri sisi tumetoa huko mbeleni utajua mwenyewe
 
Wewe ni mtu usiyejielewa,usiyejiamini na usiye na msimamo,watu kama wewe ni ngumu sana kuendelea,

Hakuna ushauri utakaoufuata humu,miaka itaenda na utajikuta huna ndoa,utakuja kutoa ushuhuda hapa JF.
 
Miaka 26 ni binti mdogo kuolewa mke wa pili? Kwa mwanamke hiyo ni miaka mingi sana ngoja afike 30 ndo atajua hajui.

Ataolewa na kibabu cha miaka 60 plus akishafika 30. Hiyo 26 tu bado hawezi kuolewa na kijana wa miaka 30 labda wa kuanzia 35 hadi 50.
Nakubali
 
Wewe ni mtu usiyejielewa,usiyejiamini na usiye na msimamo,watu kama wewe ni ngumu sana kuendelea,

Hakuna ushauri utakaoufuata humu,miaka itaenda na utajikuta huna ndoa,utakuja kutoa ushuhuda hapa JF.

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]aiseeee

Nipe ushaurii bhn nimekwama kijana mwenzio

Ila umenifanya nicheke kwa nguvu maana umeandika kwa hisia sana
 
Habari ndugu zangu,

Wakati nipo Mkoa X, nilikutana na huyu kijana nikiwa nimemaliza kidato cha sita kwenye mafunzo fulani fulani huko yeye akiwa tayari ameshaajiriwa ana kama miaka 5 kazini.

Nakumbuka tulikutana ofisini wakati mimi napeleka barua za kuomba ajira na yeye amefika kuripoti maana alikuja likizo. Yeye ndo alinikuta ofisini nikiwa namalizia malizia kupewa maelekezo, hatukusemeshana tuliangaliana tu kisha nikatoka nikamuacha ofisini na mimi kurudi home

Usiku wa siku hiyo nikapokea simu ni namba ngeni sauti ya kiume

“Samahani kwa kuiba namba yako bila Idhini yako, mimi ni yule kaka tulieonana ofisini nilikukuta ukiwa unaongea na mkuu”

“Mmh mbona sikukumbuki “ nilijifanya Kama simkumbuki lakini ukweli nilikuwa namkumbuka sana tu kwasababu alipoingia nilimuona na namna alivovaa alikuwa smart wa kuvutia kumtazama hivyo nilizuga tu

Basi alijielezea kwamba alivutiwa na mimi na kwakuwa nilikuwa nimeshaondoka hajui pa kunipata aliiba namba yangu kwenye daily ya mkuu wa ofisini maana niliambiwa niiandike kama kutatokea shida anijulishe

Kuanzia siku hiyo tulikuwa tunawasiliana sana na yule kaka (Tumwite Salim). Salim hakuwai kunitongoza mpk anaondoka likizo yake ilipoisha

Bahati nzuri tulikuwa tunakaa mkoa mmoja yeye alitangulia mimi nikafuata baadae na nakumbuka yeye ndo alinitumia nauli ya kurudi

Nilifika nyumbani mkoa aliopo yeye tukawa tunaendelea kuwasiliana akanitongoza akaniomba niwe mpenzi wake nikamwambia anipe muda wa kutafakari

Ukweli jibu nilikuwa nalo moyoni nilikuwa nimemkubalia ila kusema nikawa naogopa ,,unajua sababu ilikuwa ni nini??

DINI hii ndio sababu ambayo iliniumiza akili sana kijana alikuwa muislam na mimi mkristo tena wale wenye msimamo mkali (Mama yangu ni mlokolee) baba ni muislam ila alishatangulia mbele za haki lakini sisi kwetu wote ni wakristo ukiachia upande wa baba

Mama yangu ni mtu mwenye msimamo sana anaweza hata kunilaani akisikia hivi

Turudi kwenye jibu nililompa

Nilikubali nikamwambia sawa lakini vipi kuhusu dini akasema tuache kwanza tutajua mbeleni basi nimekaa nae kama wiki hivi nikaona hapa haiwezekani hii dini itakuja kuharibu mbeleni huko nikamwambia naomba tuachane maana mimi siwezi kubaildili dini na wewe najua huwezi siwezi kumuumiza mama kwasababu ya mapenzi mama atanitenga

Salim Alinambia ameumia sana na nimemkosea sana basi tukabaki marafiki wakuchart
Tukaja kupotezana karibia miezi 9 nakumbuka siku amenitafuta akanambia “Mama mzungu naomba nikuoe hata ndoa ya serikali ama bomani nakupenda na naamini wewe unanifaa“

Kusema ukweli nilikataa na kipindi hiko nilikuwa bado msichana mdogo miaka kama 23 hivi
Wakati ananiambia hivo mimi nilikuwa nawaza harusi kubwa washiriki ndugu zangu wote na marafiki zangu niolewe kanisani kiufupi nilikuwa natamani ndoa ya kanisani yakuvaa shela

Salim alinikaushia tena akajaga kunitafuta baada ya miezi kama 5 akanikumbushia nikamwambia hapana nahisi alikuwa ananitega maana baadae akanambia mimi nimeamua kuoa kwasababu umri unaenda na kazi inayoifanya inabidi aoe ili apate mambo furani furani. Nikamwambia tu poa Mungu akutangulie kwenye ndoa yako upate mke mwema

Sauti ya mwisho nilioisikia kwake ni “daaah” Akakata simu

Salim nilipomjibu hivo nahisi alisusa ama kukasirika maana hakupatikana tena kwa namba zake zote nilizokuwa nazo
Nakumbuka mambo yote yanaendelea alishawahi kunipeleka kwa baadhi ya ndugu zake mama ake mdogo dada na mdogo wake walikuwa wananifahamu ila sikuwa na namba zao japo walipokuwa wanaishi nilipajua ila sikutaka kwenda

Miaka ikapita kama mitatu mwaka huu ndio nikashangaa namba ngeni Mimi Salim nimekukumbuka Leo ikabidi niweke lini yangu ya zamani nichukue namba yako nikutafute

Kwakweli nilifurahi maana nilimmis sana sanaa. Nikamuuliza kwanini Salim umenifanyia hivo miaka mingi sana unajua nilivokumis,, akanijibu niliona unanizingua sana nikaamua nisikutafute mpk ukue kwanza kiakili ndo nirudii maana unautoto mwingi Sanaa

Basi tukaongea vizuri tukawa tunachart nikakumbuaka alinambiaga anataka kuoa nikamuuliza kama ameoa
Salim akanambia ameoa 2020 na ana Mtoto mmoja

Kusema ukweli sikuamini alinitumia mpk picha na Mtoto wake ni mzuri Mtoto wake Sanaa,, niliumia kwasababu
Salim, nilikuwa nampenda kweli sana sema nilikuwa sina maamuzi niseme na utoto ulichangia hiyo kitu imeniuma sanaa

Salim amenambia ameumia sana kwa kunikosa alitamani niwe mke wake anasema anaishi na mwingine na moyo wake upo kwingine
Salim anasema anataka anioe mke wa pili maana dini inaruhusu , ananipenda sana hatamani kunikosa

Mimi mama mzungu Salim nampenda na ningetamani awe Mume wangu lakini kuwa mke wa pili roho inasita sana naogopa sana hasa swala la ushirikina nasikia wanarogana sana

Mimi sijazeeka hivyo mpk niolewe mke wa pili hata sijafika miaka 28 nawaza sana je mke wake atanikubali

Salim amesema Kama itashindikana ndoa ya kidin ipo ya serikali na kimila ilimradi nitambulike kuwa mimi ni mke wake.


Ushauri wenu
Huyu jamaa vigezo anavyo vyote yaani kama angekuwa mkristo ningekuwa sina haja ya kumfikiria wala kumkataa miaka hiyo nyuma
Maana ni kijana ambae anajiheshimu mstaarabu ana huruma sio kwangu tu nimeonaa hata tulipokuwa mafunzoni ni mtu anaeguswa sanaa juu ya wengine wale mnaosoma biblia mnamfahamu Korinerio basi Salim anafanana kabisa na huyo mwamba kwenye bible

Je nijitose tu kuwa mke wa pili ama nikomae na mkristo tufunge pingu za maisha Japo sijawahi kupata wa dini yangu ambae yupo seriously [emoji19]

Kuhusu hela anayo nyingi tu ya kututosha mimi na mke wake [emoji38]

NB: Mimi na Salim mpk leo hii Hatujawahi kufanya mchezo Mchafu yaani Salim hajaninyandua wala mimi sijanyanduliwa na Salim

Najua kuna watakao uliza umri wako sipo chini ya miaka 25 wala sipo juu ya miaka 28 nipo katikati hapo

Mnisamehe kwa uandishi
Sawa,ngoja tubeti kwanza,tuangalie mkeka wa leo umekaaje.

Tutarudi tukushauri
 
mpaka Salimu anakumbukwa,itakua ashapiga mzigo!
 
Mpe kwanza...usipompa utajuta mbeleni...

Nimeshajuta

Ila suala la kupewa nafikiri tufunge mjadala halipo
Kumpa maana ake nimekubali kuwa bi mdogo


Natamani miaka ingerudi nyuma huenda ningemkubali ningekuwa Bi mkubwa [emoji24][emoji24]
 
Back
Top Bottom