Sallam athibitisha Harmonize kujiondoa WCB

Nampongeza sana,ndivyo inavyotakiwa kwa mpambanaji yeyote.Cha muhimu ni kujipanga tu.Unakuta mtu ameajiriwa tangu abalehe hadi uzeeni...yeye kuita wenzake boss tu.Inatakiwa ifike mahali na wewe ujisimamie mwenyewe uwe CEO kwenye kampuni yako.Nampa pongezi sana na si ajabu akafika mbali zaidi,cha muhimu ni mkakati aliojiwekea.
 
Wasanii wa TZ ambacho hawaelewi mpaka sasa hivi ni kwamba mziki wa kizazi hiki,muziki wa awamu hii hauhitaji uwe na KIPAJI peke ake kama anavyodhani HARMONIZE..mziki wa sasa hivi unahitaji KIPAJI + KIKI(pesa) ya kuufikisha kwenye PEAK.

Harmonize yawezekana amejiona kipaji anacho na Kiki anaweza...kwa haraka haraka tu Harmonize akiniambia ana kipaji cha kuimba kuliko hata DIAMOND naweza nikamkubalia 100% ila kamwe hawezi niambia ana uwezo wa KIKI za DIAMOND,ki ufupi diamond WCB ndio nyumba ya KIKI...

WCB wanapitwa vipaji na vijana wengi tu nnje ya WCB ila kinachofanya WCB ibaki on PEAK ni nyumba ya kiki yaan diamond ndio matofali,nguzo,mpk bati...kujitenga na DIAMOND utakua umebaki na KIPAJI ila KIKI huwezi tena,maisha ya KIKI anayaweza DIAMOND ndio mana anaweza maliza mwaka mzima hajatoa nyimbo ila Jina lake halikauki midomoni mwa watu.

Sasa HARMONIZE atambue tu kwamba ataondoka na KIPAJI chake ila KIKI kaziacha...akae akigundua hilo mwache ajidanganye na huyo mzungu wake..

Simuombei aanguke nataka atuthibitishie kua anaweza bila WCB.
 
Mbona "Skylight Band" inafanya vizuri? Seba sio meneja mmbaya ni miongoni mwa wadau wakubwa wa huu mziki! Harmonize akikomaa ataendelea kuwa juu!
Seba fitna ya muziki anaijua since anatangaza njia panda clouds fm
 
Hapo kwenye RED naunga mkono kwa 100%! Si kuanzisha label bali label zenye nguvu zitakazotoa wasanii wengi watoa hits na kufanya tasnia yetu kuwa competitive!!! So, Harmonize kama amejipanga sawa sawa na kutaka kuanzisha label yenye nguvu kweli kweli, ya kuweza kushindana na hata kuizidi WCB, itakuwa poa sana lakini kama anatoka kwa hoja tu kwamba hataki kuwa chini ya mtu kwavile yeye ni mkubwa, basi atafeli, kwa sababu hiyo siyo hoja ya msingi hasa ukizangatia hata wasanii wakubwa wa mbele tu na wenyewe wapo chini ya label!! Hoja nyingine labda kama anaona maslahi anayopata ni madogo na anadhani huko aendako atapata maslahi makubwa zaidi, nayo ni hoja ya msingi manake yeye hafanyi muziki kama burudani bali biashara!!
 
Lavalava hamna kitu bhn naww...n lebel tu inambeba yule muimba kaswida
 
Hivi ile lebo ya wcb mmiliki si dayamondi?
 
Kwahiyo ata dayamondi unaweza kuta hana kitu kabisa??
 
kweli mzee..wcb ndo ilikua kila kitu kwake sasa amenyea kambi atakua kama mavoko

halafu mbaya media zingine pia haziivi sa cjui nae atafungu radio na tv
So long as ataondoka kwa njia muafaka, Wasafi hawataacha kupiga ngoma zake! Ni ngumu kwa Wasafi kupiga ngoma za Mavoko kwa sababu Mavoko alitoa tuhuma za kunyonywa!! Sasa mtu kama huyo lazima uwe na tahadhali ili kesho na kesho kutwa asije tena akasema Wasafi wanapiga ngoma zangu bila kunilipa!!! Harmonize hawezi kufika huko! Harmonize angependa sana kuondoka WCB lakini bado akiwa na ties na WCB kwa sababu anafahamu potential yake! Na hata kuhusu hizo media ambazo hawaivi; kimsingi "mgomvi" wa hizo media sio Harmonize bali Diamond! Na media za Bongo zilivyo za ajabu, utaona sasa watakavyoanza kumchangamkia Harmonize kama namna ya ku-deal na Diamond! Usishngane ndani ya wiki 2 zijazo baada ya kila kitu kuwa sawa, ukakuta jina la Harmonize linakuzwa pale Clouds kuliko msanii mwingine yeyote!! Hata hivyo, itakuwa ni upepo tu! Kama upepo wa EFM kwa Ruby enzi Ruby anaingia kwenye conflict na Clouds!!
 
Hivi ile lebo ya wcb mmiliki si dayamondi?
Hata kama angekuwa anaimiliki WCB kwa 100%, bado share ya showz lazima iende kwa mameneja wake! Mtoa hoja hakumaanisha mapato ya label ya WCB bali mapato ya shows za Diamond kama msanii, ambae nae yupo managed na hao mameneja watatu!!! Ukiona akina Tale wanaenda na familia zao Ulaya, hayo ni matokeo ya mgao wanaopata kutoka kwenye shows za Diamond!!
 
Kasumba tuliyonayo waswahili kondeboy Ana explore new ventures na opportunities hakina sababu ya kumbana WCB.

Tunahitaji wanamuziki wakubwa Kama nchi za wenzetu . Hongera Sana Harmonenga kwa kuchanja mbuga inshaalah mola akuwekee wepesi.

#Achawoga Kondegang kesho la mtu moko
# Jembejembe tunakuamini usimtose kijana wetu

#Independentisgrowth
 
Mbona "Skylight Band" inafanya vizuri? Seba sio meneja mmbaya ni miongoni mwa wadau wakubwa wa huu mziki! Harmonize akikomaa ataendelea kuwa juu!
Seba fitna ya muziki anaijua since anatangaza njia panda clouds fm
Hiyo skylight band imefika level ya kimataifa? Huyo Seba kamfikisha msanii gani level ya kimataifa? Harmonize alikua amefika level ya kimataifa so tunategemea awe juu zaidi ya hapo, na hilo ndo tunalosubili.
 
Mbona mwishoni umeoeta uchawi mkuu.
Come on mentality gani hio,unadhani dunia ingekua na mentality hio Leo kungekua na jamiiforum?
Haswaa kaanza vzr huko mwisho sasa kaleta uchawi wake kwani Mbona inaonesha km imewauma Sana mmakonde kuondoka na wkt mnajinasibu kaondoka kiustaarabu?
 
Wabongo ni wanafiki tu.

Kipindi kile wasanii wakiachana na CMG au THT tunaambiwa wamejitambua na blah blah kibao ila huyo jamaa kutoka WCB imekuwa nongwa Why?
Sindano imewaingia kinoma hii sindano ni ya kutibia ng'ombe jooh yaani wameumia kinomaa ndo maana wanaweweseka mara oooooh atapotea utazani wao ndo sir God
 
Kwani WCB mama yake mkuu Mbona munaumia Sana?
 
Sasa mkuu, mbona hakushikiwa mtutu kumwaga wino kwenye huo mkataba, si alikubali yeye mwenyewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…