Sallam athibitisha Harmonize kujiondoa WCB

Sallam athibitisha Harmonize kujiondoa WCB

Harmonize ni lini aliuza mitumba Tandale? Hii ni fact ndogo ambayo inaondoa maana ya yote uliyoyaandika.

Nawashangaa sana mnaosema Harmonize kakosea kubadili management... Hivi nyie mnaijua WCB kuliko Harmonize?
Harmonize ni mtu wa ndani wa WCB, anajua mengi kuliko mtu yeyote nje ya WCB. Acheni kuleta siasa ktk masuala ya career za watu.
Huu uchambuzi wenu hauna maana yoyote maana tasnia ya muziki inahusisha mambo ya ndani ambayo hatuyajui tofauti na mpira unaochezwa hadharani ndio maana mtu unaweza kufanya uchambuzi ila sio muziki wetu uliobeba fitna za kila namna.

Mimi naona tumtakie heri kijana wetu, ameonesha uthubutu muacheni asonge mbele acheni hizi ramli zenu chonganishi.
Waambie mkuu naona inawachoma Sana konde kusepa!!!!
 
Wasanii wa TZ ambacho hawaelewi mpaka sasa hivi ni kwamba mziki wa kizazi hiki,muziki wa awamu hii hauhitaji uwe na KIPAJI peke ake kama anavyodhani HARMONIZE..mziki wa sasa hivi unahitaji KIPAJI + KIKI(pesa) ya kuufikisha kwenye PEAK.

Harmonize yawezekana amejiona kipaji anacho na Kiki anaweza...kwa haraka haraka tu Harmonize akiniambia ana kipaji cha kuimba kuliko hata DIAMOND naweza nikamkubalia 100% ila kamwe hawezi niambia ana uwezo wa KIKI za DIAMOND,ki ufupi diamond WCB ndio nyumba ya KIKI...

WCB wanapitwa vipaji na vijana wengi tu nnje ya WCB ila kinachofanya WCB ibaki on PEAK ni nyumba ya kiki yaan diamond ndio matofali,nguzo,mpk bati...kujitenga na DIAMOND utakua umebaki na KIPAJI ila KIKI huwezi tena,maisha ya KIKI anayaweza DIAMOND ndio mana anaweza maliza mwaka mzima hajatoa nyimbo ila Jina lake halikauki midomoni mwa watu.

Sasa HARMONIZE atambue tu kwamba ataondoka na KIPAJI chake ila KIKI kaziacha...akae akigundua hilo mwache ajidanganye na huyo mzungu wake..

Simuombei aanguke nataka atuthibitishie kua anaweza bila WCB.

Mkuu kwanini usimpe muda kabla ya kumuhukumu hataweza hizo kiki?
 
ukiona mtu halalamiki kwenye record lebel ujue terms and conditions katika makubaliano yao inatao favour kwa kila upande.

hii ni tofauti na aina ya mikataba yenu mnayoingia na wasanii huku bongo. mnawabana sana hawa vijana kwenye mikataba. mnalifanya hili kwa kuwa wengi wao hawajaenda shule.

na kwakuwa wengi wao ni zero brain academically, wanakuwa too excited na ile lifestyle ya kuishi kisuper star(kuvaa nguo nzuri, kuendesha gari, kudate na wadada maarufu wa mujini nk). huwa hawatilii maanani vipengele vya kwenye mkataba. wanakimbilia kusign kichwakichwa.

baada ya miaka kwenda mbele, baadae wanakuja kushtuka kuwa wanadhurumiwa, hawafaidiki na kazi zao. wanashtuka kuwa wanamtajirisha mtu au kikundi fulani cha watu wachache. inawezekana hiki ndio kilichomsukuma harmonize kuvunja mkataba na wasafi.
Sorry hiv inamaana hamjui kinachoendelea Kati ya Kanye west na Jay z mpaka mnamtolea mfano ..au tuko dunia tofauti![emoji51]
 
Hatimaye Meneja wa Wasfi Classic Baby (WCB), Sallam SK amekata mzizi wa fitna baada kuthibitisha Harmonize kaandika barua ya kuvunja mkataba na lebo ya WCB.

Amesema kwa sasa wanasubiria kufanya taratibu za kisheria kuuvunja mkataba na karibuni watakuwa na kikao cha kukubaliana 'terms' ingawa Harmonize ameshaonyesha nia ya kukubaliana na 'terms' zote za kuvunja mkataba.

Sallam ameomba radhi kwa mwenendo uliokuwa unaonyeshwa na msanii huyo siku za karibuni lakini amewaomba mashabiki wa Wasafi waendelee kutoa ushirikiano kwa Harmonize kwani ajaondoka kwa ubaya.

Sallam amesema katika tamasha la Wasafi lililofanyika mjini Mwanza, Harmonize alitumia usafiri binafsi, kufanya baadhi ya mambo yaliyotoa tafsiri kuwa amejitenga.

Sallam amesema kwa sasa Harmonize moyo wake haupo Wasafi lakini ukweli ni kuwa bado ana mkataba na kundi hilo.

Kuhusu kujitenga na wenzake Sallam amesema, “Hili jambo si sawa kulingana na maudhui ya tamasha hilo. Maudhui ya Wasafi Festival ni umoja. Msanii akiamua kuacha kuambatana na wasanii wenzake ambao wapo pamoja katika tamasha ni kwenda kinyume.”

“Sisi katika tamasha letu hatupendi kutengeneza matabaka, tumeamua kuwa kitu kimoja, siyo kwamba Diamond, Rayvany hawakuwa na uwezo wa kutumia usafiri wao binafsi kama alivyofanya Harmonize” amesema Sallam.


Mtazamo wangu;

Harmonize anaenda kuwa historia kwenye muziki wa bongofleva uenda tukashangaa sana pale ambapo hatutasikia tena muziki wa kueleweka kutoka kwake na ukawa mwisho wake kisanaa.

Waliomshauri Hamo anapaswa kuwachukia maisha yake yote kama waliomshauri Mavoko.

Acha kujipa uganga ndugu kwani wcb ndo wanaomuimbia anaweza akatoka then akawa msanii mkubwa tu na kufanya yake yote matokeo ata diamond alikua kwenye management tofauti na akafanikiwa so hata yeye anapenda mafanikio makubwa pia
 
Wewe ni kati ya wasioujua muziki lakini una ujuaji mwingi ilhali huna ulijualo.
Unasema Lavalava sio msanii na nyimbo zake hazieleweki? Mimi sio shabiki wa hiyo WCB yenu ila Lavalava ndio msanii wangu bora pale WCB na hizo nyimbo zake unazosema huzielewi ndio nimejua hujui muziki.

Unathubutuje kusema mtu mwenye vibao vitamu kama Bora Tuachane, Utatulia, Go Gaga na wimbo wangu bora wa muda wote kwa Lavalava, Kilio sio msanii?
Wewe jamaa umejua kuniharibia asubuhi yangu!
Teh ... [emoji28]
 
Wasanii wa TZ ambacho hawaelewi mpaka sasa hivi ni kwamba mziki wa kizazi hiki,muziki wa awamu hii hauhitaji uwe na KIPAJI peke ake kama anavyodhani HARMONIZE..mziki wa sasa hivi unahitaji KIPAJI + KIKI(pesa) ya kuufikisha kwenye PEAK.

Harmonize yawezekana amejiona kipaji anacho na Kiki anaweza...kwa haraka haraka tu Harmonize akiniambia ana kipaji cha kuimba kuliko hata DIAMOND naweza nikamkubalia 100% ila kamwe hawezi niambia ana uwezo wa KIKI za DIAMOND,ki ufupi diamond WCB ndio nyumba ya KIKI...

WCB wanapitwa vipaji na vijana wengi tu nnje ya WCB ila kinachofanya WCB ibaki on PEAK ni nyumba ya kiki yaan diamond ndio matofali,nguzo,mpk bati...kujitenga na DIAMOND utakua umebaki na KIPAJI ila KIKI huwezi tena,maisha ya KIKI anayaweza DIAMOND ndio mana anaweza maliza mwaka mzima hajatoa nyimbo ila Jina lake halikauki midomoni mwa watu.

Sasa HARMONIZE atambue tu kwamba ataondoka na KIPAJI chake ila KIKI kaziacha...akae akigundua hilo mwache ajidanganye na huyo mzungu wake..

Simuombei aanguke nataka atuthibitishie kua anaweza bila WCB.
Dah ila mondi ana kipaji cha kuimba mkuu

Huyu mmakonde ana miaka mingapi kwenye gemu tuanzie hapo

Mondi toka 2008 nadhan

Hajawahi shuka
 
Hiyo skylight band imefika level ya kimataifa? Huyo Seba kamfikisha msanii gani level ya kimataifa? Harmonize alikua amefika level ya kimataifa so tunategemea awe juu zaidi ya hapo, na hilo ndo tunalosubili.
Kabla ya Diamond mkubwa Fela na Salam waliwahi kumfikisha msanii gani level ya kimataifa??
 
Kabla ya Diamond mkubwa Fela na Salam waliwahi kumfikisha msanii gani level ya kimataifa??
Sallam alimfikisha AY level za juu mpaka kuwa msanii wa kwanza kupiga show MTV MAMA na kufanya collabo na wasanii kama Sean King stone,Psquare nk.
Sallam vilevile ni middle man kitambo na kama hujui yy ndio anaye meneji kazi zote za Wizkid EA na Sunday meneja wa Wizkid ana meneji kazi za Diamond West Africa,ili wasiingizwe mkenge na mapromota feki.
 
Dua la kuku........... kwani mtu akikua c anaondoka kwa wazazi wake mbona mmemuwekea kinyongo au lebo ndo inamtegemea yeye akiondoka kuna mkwaja utakata???
Kwa waliobaki wcb , hakuna tena mwenye uwezo wa kutunga nyimbo zenye ujumbe wa kugusa na kukonga nyoyo za wasikilizaji kama Harmonize.
 
Dah ila mondi ana kipaji cha kuimba mkuu

Huyu mmakonde ana miaka mingapi kwenye gemu tuanzie hapo

Mondi toka 2008 nadhan

Hajawahi shuka
Nime assume tu Harmonize akanilazimisha kua ana kipaji kuliko Mondi..sitom bishia ila kwasasa hivi mi akili yangu nafsi na roho inaelewa Hrmonize hamuwezi Mondi kwa chochote si Kipaji wala Kiki..Mondi ni level zingine akubali akatae.

Kuwa non stop masikion mwa watu from 2008 sio mchezo hata kama ni uchawi bhasi huo uchawi utakua wa Newyork
 
Mkuu acha kabisa kuna siku huyo rayvan kakosa hela ya mafuta kutoka kwake tabata mpaka Mbezi .. Wengi Wa mashabiki wanadanganywa na zile picha za Instagram tu ...


Watu hawawezi amini kuwa rich mavoko licha ya kutoa zile hitsong alikuwa hana hata mia mfukoni na akipata show hao utatu mtakatifu wanachukua cha kwao na Wcb kwa ujumla na kinachobaki ndio anapewa...


Kuna Dogo mmoja diamond alimchukua kutoka Sweden ndio kachukua nafasi ya Moses iyoyo kama dancer instructor Wa wcb, nimekutana nae face to face na anajuta kuingia wcb ... Huyo Dogo ndio kabuni dance styles kwenye nyimbo zote za wcb kuanzia mwaka Jana . nyegezi, tetema, inama n.k ...
Huoni haibu kuleta story za kutunga na ujuaji mbele ya watu waliokuzidi umri na maarifa ?
 
Back
Top Bottom