Sallam SK,awatolea uvivu clouds media na Kusaga/Wametusamehe kwa kosa gani?

Sallam SK,awatolea uvivu clouds media na Kusaga/Wametusamehe kwa kosa gani?

Naona kwa makusudi kabisa unaamua kujiumiza kichwa kwa vitu vyepesi!!
Kama ni vyepesi basi jibu maswali yangu!
Haiwezekani hata siku moja mtu kama Salam na Fella wasiwe na chao pale Wasafi media never ever!
Tale tunajua a a Dizzim
 
babu tale hajawai kua na media ..hiyo dizzim online ni ya huyo salam..
😝😝😝😝😝😝😝😝 pole sana narudia pole sana.
Usiishi kwa kutegemea udaku utaingizwa chaka hadi ujute.
.
Tale hamiliki chochote Wasafi media na hata kwenye press mbalimbali akiulizwa swali la wasafi media anasema hausiki uulizwe uongozi wa wasafi media, Salam anakuja na kulitolea ufafanuzi.
Dizzim Tv na Fm sio za online tu zinafanya kazi hadi via satellites ila tangia Azam waitoe haijarejeshwa.
.
Next time usikurupuke
 
Wewe vipi!!!! acha kukurupuka,wewe unamwona chawa lakini Mondi anajua impact ya huyo chawa ktk biashara yake ya mziki ,pamoja na 4m4 yake.

Kwa hiyo haina mashiko sababu katoa Jay Z na si DOMO? Je angetoa huyo msanii unayemwita DOMO ingekuwa na mashiko? Hii katoa Jay Z,lkn kupitia mziki wake Diamond anaiishi hii kauli ya Jigga SIMPLE.

So tatizo sio aliyetoa,bali both of them Jigga ameitumia ktk biashara yake ya mziki na Mondi naye kakopi na kuiapply kwenye biashara yake ya mziki,sawa na kusema Jigga kam-inspire Mondi kupitia kauli yake SIMPLE.

"
Got beef with radio if I don't play they show
They don't play my hits, well, I don't give a shit,
so Rap mags try and use my black ass
So advertisers can give 'em more cash for ads"
-Jay Z (99 problems).
Mkumbushe huyo Clouds hawachezi ngoma za Diamond lakini matangazo ya makampuni mfano Pepsi aliyofanya Diamond wanayacheza mpaka kesho.
 
Sasa kama.mke wa kusaga ni shareholder wa wasafi media hapo kusaga unamtoa vipi? Maana yule mama wa kingazija ni mama wa nyumbani tu hiyo expossure ya hizo business hana..hapo pesa katoa kusaga na dili kachonga kusaga tu waache kuzingua
Unamjua vizuri lakini yule dada?!! Inasemekana Kusaga alisilimu kwa ili kufunga ndoa na yule dada!! Sasa hivi angekuwa ni mama wa nyumbani tu unadhani Joe angekubali kusilimu kwa ajili yake?! Mtu asiye na exposure na biashara unaamini angeibuka tu from nowhere na kuanza kui-manage Prime Time Promotions?!
 
Mkuu ivi unajua mke wa kusaga kwao wana pesa na yeye pesa ipo vizur 2 na anaweza kwenda sambambamba na kusaga kusema kuwa n mama wa nyumban 2 umetudanganya sana tena inabid umtake radhi

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa hiyo ni mama wa barabarani ....
alaf jitanue basi ukishasema kwao pesa wanazo manake ni za baba yake ama mama.... simply put wazazi.....
hapa inazungumziwa investment kwenye biashara ya radio na tv stations.....
kumbuka kila tajiri hawa matajiri wa kawaida wanawekeza kwenye biashara wanazozijua/ambazo wana uzoefu nazo.....
Jambo la pili watu wa Fair Competition hawakuachi....
Huwezi ukamiliki kampuni kubwa mbili,manake utakuwa ni threat kwa wafanyabiashara wengine uta create monopoly....
na ndio maana nadhani ikabidi amuweke mkewe......
lkn at the back stage lijamaa ndio litakuwa lina-control
 
😝😝😝😝😝😝😝😝 pole sana narudia pole sana.
Usiishi kwa kutegemea udaku utaingizwa chaka hadi ujute.
.
Tale hamiliki chochote Wasafi media na hata kwenye press mbalimbali akiulizwa swali la wasafi media anasema hausiki uulizwe uongozi wa wasafi media, Salam anakuja na kulitolea ufafanuzi.
Dizzim Tv na Fm sio za online tu zinafanya kazi hadi via satellites ila tangia Azam waitoe haijarejeshwa.
.
Next time usikurupuke
we jamaa umekula maharage ya wapi ..hivi umesoma vizuri nilichoandika..kweli walimu wanakazi sana mashuleni..
 
we jamaa umekula maharage ya wapi ..hivi umesoma vizuri nilichoandika..kweli walimu wanakazi sana mashuleni..
Ulisema hivi wewe
babu tale hajawai kua na media ..hiyo dizzim online ni ya huyo salam..
Nikasema hivi
pole sana narudia pole sana.
Usiishi kwa kutegemea udaku utaingizwa chaka hadi ujute.
.
Tale hamiliki chochote Wasafi media na hata kwenye press mbalimbali akiulizwa swali la wasafi media anasema hausiki uulizwe uongozi wa wasafi media, Salam anakuja na kulitolea ufafanuzi.
Dizzim Tv na Fm sio za online tu zinafanya kazi hadi via satellites ila tangia Azam waitoe haijarejeshwa.
.
Next time usikurupuke
Ambacho hujakielewa kipi? Unabisha Tale hamiliki Dizim mimi nasema anamiliki

Alafu hamna mboga ya maana kama maharage wewe, mnajifanya mmekwenda shule na kuelimika kumbe wapumbavu wakubwa!
.
FAIDA ZA MAHARAGE HIZI HAPA NITAJIE MBOGA YOYOTE INAYOWEZA KUFANYA HAYA
1. Hupunguza lehemu (cholesterol)
Moja kati ya vyakula vinavyopunguza lehemu mwilini ni maharage. Nyuzinyuzi zinazopatikana kwenye maharage hujishikiza na lehemu ziwapo tumboni na kuzuia lehemu zaidi kufyonzwa mwilini.

2. Huzuia saratani
Maharage ni chakula chenye madini ya manganese pamoja na vitamini K ambavyo vyote kwa pamoja huzuia kuharibika kwa seli kunakosababisha saratani.

3. Huboresha afya ya ubongo
Kemikali ya thiamine pamoja na vitamini K zinazopatikana kwenye maharage husaidia katika kuboresha afya ya ubongo.

4. Hutawala kiwango cha sukari mwilini
Maharage yana nyuzi nyuzi ambazo hupunguza kiwango cha metaboli cha wanga (carbohydrates) mwilini. Kwa kufanya hivi huwezesha kutawala kuongezeka kwa kiwango cha sukari hasa baada ya kula chakula.

Maharage pia yana protini ambayo husaidia kupunguza kiwango cha sukari mwilini.

5. Huongeza nguvu za mwili
Kuwepo kwa madini ya chuma pamoja na manganese kwenye maharage kunayafanya kuwa na nafasi kubwa katika kuongeza nguvu za mwili.

Madini haya ni muhimu sana katika kuuongezea na kuupa mwili nguvu.

6. Huimarisha mifupa
Madini ya calcium pamoja na manganese ni muhimu sana kwa ajili ya afya ya mifupa. Maharage ni chanzo kimojawapo kizuri cha madini haya.

7. Huboresha ngozi
Maharage husaidia michakato ya metaboli ya asidi ya amino, gluconeogenesis, neurotransmitter synthesis, histamine synthesis, asidi ya mafuta (fatty acids), lipids and hemoglobin synthesis kwenda vizuri.

Ikumbukwe kuwa hivi vyote vina nafasi kubwa katika kuboresha afya ya ngozi.

8. Huboresha afya ya moyo
Aina nyingi za maharage zina vitamini B9 (folate au folic acid) ambayo ni muhimu kwa ajili ya afya ya misuli ya moyo.

9. Huboresha afya ya macho
Madini ya zinc yanayopatikana kwenye maharage ni muhimu sana kwa ajili ya afya ya macho. Hivyo ulaji wa maharage mara kwa mara utaboresha afya ya macho yako.

10. Huboresha uwezo wa kumbukumbu
Kama nilivyotangulia kusema kuwa maharage huboresha afya ya ubongo, uwezo wa kumbukumbu huboreshwa pia kupitia ulaji wa maharage.

Vitamini B1 inayopatikana kwenye aina mbalimbali za maharage hukabili ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu (Alzheimer’s na dementia).

11. Huondoa sumu mwilini
Vyakula vingi vya viwandani huhifadhiwa kwa kutumia vihifadhi vyenye sulphites; Sulphites inapozidi mwilini ni sumu. Hivyo basi kemikali ya molybdenum inayopatikana kwenye maharage inasaidia kuondoa sumu ya sulphites mwilini.

Soma pia: Njia 12 za Kuondoa Sumu Mwilini

12. Hukabili shinikizo la damu
Kama tulivyoeleza kwenye makala nyingine, potassium, magnesium pamaoja na protini husaidia sana kukabili shinikizo la juu la damu. Maharage hukabili shinikizo la damu kwa kuwa ni chanzo kizuri cha potassium, magnesium pamoja na protini.

13. Hupunguza uzito
Vyakula kama maharage vina nyuzinyuzi zinazokuwezesha usihisi njaa mapema, hivyo kuepuka kula mara kwa mara na kusababisha kuongeza uzito wako.

Ikumbukwe pia maharage ni chakula ambacho kina kiwango kidogo cha mafuta (fat), hivyo hakisababishi uzito mkubwa wa mwili.

14. Husaidia kutibu tatizo la kutokupata choo
Kama nilivyoeleza kwenye hoja zilizopita, maharage ni chakula chenye nyuzinyuzi kwa wingi; ikumbukwe kuwa vyakula vyenye nyuzinyuzi ni tiba bora ya tatizo la kutokupata choo.

15. Husafisha tumbo
Wakati baadhi ya watu wakiyachukulia maharage kama kitu kinachovuruga tumbo, maharage yana nafasi kubwa kwenye afya ya tumbo.

Utafiti uliofanyika ulibaini kuwa kula maharage kwa kiasi cha kutosha kutasafisha tumbo lako na kukukinga na maradhi ya saratani ya utumbo (colon cancer).

16. Husaidia kukabili maradhi ya asthma
Utafiti uliofanyika ulibaini kuwa kuna uhusiano kati ya upungufu wa madini ya magnesium na kutokea kwa maradhi ya asthma. Kutokana na maharage kuwa na kiwango kizuri cha madini ya magnesium, basi yanaweza kuwa na mchango mkubwa katika kukabili maradhi haya.

17. Huboresha na kukomaza seli nyekundu za damu
Virutubisho vilivyoko kwenye maharage husaidia katika maendeleo na ukomavu wa seli nyekundu za damu.

18. Huzuia kuzeeka mapema
Kuzeeka mapema? Ndiyo, kutokana na maharage kuwa na kemikali zinazozuia kuchakaa kwa seli za mwili, yanaweza kuwa na mchango mkubwa katika kuzuia kuzeeka mapema.

19. Huboresha afya ya kucha na nywele
Biotin, madini ya chuma pamoja na protini vinavyopatikana kwenye maharage vina nafasi kubwa katika kukupa kucha imara pamoja na nywele zenye afya njema.[/QUOTE]
 
Back
Top Bottom