Ni Kweli kabisa nimecheki pia Mase alipokua anahojiwa kuhusu umafia wa puff daddy, Mase anakwambia mikataba mingi ni magumashi na wasanii weng kwasababu ya uchanga wao na elimu ndogo wanasaini vitu ambavyo hawavijui mwa mfano Mase mkataba wake na Bad boys ambayo waliingia 1996 umekuja kuisha 2020 kumbuka 50cent alitaka kumsajili Gunit ukashindikana kabisa mwishowe Mase amekua mlokole, pia nliona clip ya busta rhymes anakwambia label nyingi zina fake maisha halis ya wasanii kwa mfano utavalishwa cheni fake,watakupa gar za kifahar,nguo kali,utapangiwa nyumba kali lakn bila msanii kujua kuwa anakuja kukatwa kwenye malipo yake ya show au streams.
Pia nliona kisa cha kundi mashuhuri la TLC kuvunjika aisee nilijua unyama uko Tz tu kumbe hata america label zimeua na kufilisi wengi,TLC walikua wakipewa nguo,viatu,cheni,miwani,magari etc hapo weka na tiketi za ndege,gharama za show,gharama za hotel wakienda tour au show,gharama za photoshot,gharama za airtime promoshen etc sasa TLC walikuja shituka kwenye album kwa mfano imeingiza bilion 4 wao wako 4 wanashangaa kwenye akaunti inawekwa 100mil wakiuliza wanaambiwa makato ya label kundi likafa....ndo mana hata hapa kwetu angalia fela alichowafanyia TMK
YAMOTO BAND ni wizi na dhruma,Yamoto walijengewa nyumba kwenye kiwanja kimoja na nyumba zimeungana kama train ndo madogo wakahoj mbona wakina chege wamejengewa separate sie kiwanja kimoja tukae wote? Kundi likafa, angalia harmonize kawalipa wasafi kiasi gan cha pesa kujitoa? Rich mavoko mpaka leo akaunti yake ya youtube anaishikilia sallam.
Yes hata Snoop Doggy same thing. Anakwambia alishtuka siku anasimamsishwa na askari wa usalama barabarani, halafu askari anamwita Snoop Mr Suge (maana alikuwa chini ya label ya Suge Knight ya Death Row). Ndipo akaja kutambua kuwa hakuna anachomiliki, kuanzia magari, nyumba anayoishi na kila kitu kinamilikiwa na label ambayo mmiliki wake ni Suge Knight. Anakwambia hapo ndipo alipoamua kuchukua hatua.
Nilicheka T-Pain anakwambia label inakwambia label wanakwambia hatujali unafanya nini, isipokuwa chochote utakachoingiza tutakuwa wa kwanza kuchukua chetu.
Pia nikamskia Akon anakwambia alipouza hakimiliki zake alizokuwa nazo kwa Lady Gaga, that is when it turned into an investor. Pia kidogo amsign Drake, ila walipomleta kwake anasema Drake alikuwa kipindi hicho anaimba kama Eminem alimkataa coz alikuwa anasound kama Eminem.
Akon anasema Smack that, alikuwa anahitaji kufanya na Eminem, sasa jinsi ya kumpata ashajaribu kila njia kashindwa, akaenda LA akiwa club akakutana na jamaa akamwambia Eminem mshikaji wake, kesho atampeleka. Kweli kesho yake akampeleka studio kwa Eminem. Hapo Akon alikuwa na ngoma tayari ambayo alitaka afanye na Eminem, kufika Eminem akamsikilizisha ma beat kadhaa ila ilipofika ay Smack that akaikubali. Eminem akamwambia aingie booth jamaa akaingia akaweka mistari yake, kutoka anakuta eminem ashaondoka, akauliza jamaa vipi kaenda wapi, wakamwambia muda wake ushaisha huyo ashaondoka rudi kesho.
Kesho yake anafika studio saa sita, anaambiwa Eminem kaenda lunch. Baada ya muda akarudi, akamwambia ngoma yako tayari unataka kuisikiliza, kumwekea, anakuta kuna verse ya Eminem tayari. Jamaa anamuuliza, hii umefanya saa ngapi. Eminem akamwambia yeye Studio uwa hakeshi, anafanya kama kazi, anaingia saa mbili ikifika saa kumi anaondo anarudi nyumbani, yani ana ratiba, saa mbili anaingia, saa tatu anapata breakfast, saa sita anaenda lunch, saa kumi anaondoka anaenda home.
Akon anasema toka muda huo na yeye akaanza jifunza kuwa na ratiba siyo eti unakesha mara vibe limepanda studio.