sinza pazuri
JF-Expert Member
- Aug 16, 2014
- 3,344
- 9,066
Sallam SK aka Mendez ambaye ni international manager wa Msanii namba moja Africa yani Diamond Platnumz ametoa pongezi jinsi Yanga inavyofanya vizuri kwenye kuwaongezea thamani kwenye chapa zao wachezaji wake au kwa lugha nyingine branding.
Sallam SK ambaye pia ni mdau mkubwa wa soka ambaye alishafanya hapo nyuma kazi ya kuwatafutia masoko nje ya nchi wachezaji wa kiafrica, ameendelea kusema kuwa mameneja wa wachezaji wa kitanzania wamelala usingizi wa pono.
Nakubaliana na Sallam aka Jorge Mendez Wa bongo, wachezaji wetu wengi hawana managers bali wana madalali.
Managers wa TZ utawaona kwenye kipindi cha usajili ndio maana ligi imekuwa kubwa wachezaji wamekuwa mastaa ila huwezi kuta mchezaji ana endorsement ya maana kama za kina Diamond, Zuchu, Mbosso, Rayvanny, Mobetto au Nandy.