YEHODAYA
JF-Expert Member
- Aug 9, 2015
- 36,902
- 52,001
Nchi gani hiyo mbona hujatajaKatika nchi ya wapumbavu kila kitu kinawezekana
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nchi gani hiyo mbona hujatajaKatika nchi ya wapumbavu kila kitu kinawezekana
Huenda atakayefuata yaani awamu ya 7 naye hatokaa sana atapita kama wenzake huku wa awamu ya 6 akiendelea kufaidi pensionWhy odd number?
Naunga mkono hoja
Huyu Mama Super Sana
Msikilize hapa
View: https://youtu.be/-UXoc_m0ZKo?si=wDKW5lNYBlXH1sV8
View: https://youtu.be/2TPWGMc9Wh8?si=mgWZbmfj1wlhrCU1
View: https://youtu.be/iQRndfSdiHE?si=BBfwvbf49QEq0Vij
View: https://youtu.be/UBMGVaYrxSQ?si=_8R4POUECeiOjil4
P
Mkuu ruaharuaha , she is super for the contents, umesikiliza contents au umeishia kukodolea shavu dodo na ile baby face?.Super? sababu amekupa interview sio, ni sawa pia unavyomsifia Makamba sababu wanakupa interview.
Unalipwa kiasi gani kutetea huu ujinga? Wewe ni objective, serious journalist?
Sahihi vingine hata hutavifaidi .mtu awaye yeyote hata apewe bilioni kwa mwezi mifisadi mingi na mikwapua pesa za wanyonge au za umma au kuonea wanyonge kwa rushwa nk au kula kodi za walalahoi inaunwa kuanzia visukari na migonjwa kibao na haiwezi kula chakula kitamu chenye sukari,chumvi au mafuta ,nyama nzuri red meat nk Mwenyezi Mungu kawavizia kawatenda kitu kibaya na mamilioni na mabilioni yao chakula tu chenye chumvi,mafuta au sukari hakipandi wakati lofa anaweza bugia chumvi au sukari kavu bila kuunga mboga yuko fresh tu au chakula aweza kula chenye mafuta kibao na yuko fresh tuKifafanuacho wafu mbele ya Mungu, si cheo kikubwa, si daraja , si sifa
matendo mema yataufungua mlango wa mbingu.
ukija duniani unatafuta , unatumia, unaviacha
Mungu hapa ndipo alicheza hasa, huondoki na chochotee
Mkuu ruaharuaha , she is super for the contents, umesikiliza contents au umeishia kukodolea shavu dodo na ile baby face?.
Mimi ni mwandishi wa kujitegemea kwa kujitolea, silipwi na yeyote, uandishi na utangazaji naufanya bure kabisa just for the love of it!.
P
Sahihi ulichosemaHahaha, Shavu tena! Nazungumzia hii topic ya mleta mada Jaji mfawidhi.
Contents mmezungumzia mambo mengi mengine hadi kuhusu uhusiano wao. Sisi hayatuhusu.
Maoni yako ni yapi kuhusu hii topic? Jikite kwenye muswada wake.
Salma Kikwete ambaye ni Mwalimu Mstaafu wa Oystrbay Primary, Mbunge huko Mtwara na pia Mmiliki. wa WAMA -NGO ya Kitajiri:
Wenza ni :
1. Maria Nyerere.
2. Siti Mwinyi.
3 Anna Mkapa.
4. Salma Kikwete
5. Janeth Magufuli
Bunge lijalo , kama atatokea kiongozi mwengine basi ipendekezwe na watoto wa wastaafu wapewe mafao, baba zao na mama zao wametumikia nchi, wametumia muda mwingi kufikiria taidfa na kuliongoza taifa.
Kifungu kipya cha 13 ambapo makamu wa rais anapofariki akiwa madarakani, au baada ya kustaafu (kabla hajalipwa mafao yake), wategemezi wake (dependants) watalipwa kiasi cha fedha sawa na mshahara wote wa makamu wa rais alioupokea wakati akiwa madarakani. Mfano, kama makamu wa rais alikaa madarakani kwa miaka 10, akalipwa TZS 2B kama mshahara, basi wategemezi wake watalipwa kiasi hiko cha TZS 2B kama pension. Ifahamike, kwa mujibu wa sheria hii, neno "dependants" limefafanuliwa kwenye kifungu cha 4, na maana yake ni mke au wake, mume, watoto (ambao walikuwa ni tegemezi kwa marehemu), pamoja na wazazi wa marehemu (wategemezi).
Badiliko la JEDWALI la sheria hii linalotaja nyongeza ya mafao ya viongozi.
1. Rais mstaafu ameongezewa idadi ya magari kutoka magari 2, sasa atapata magari 3 yasiyopungua uzito wa tani 3 (yaani hawezi pewa Corola, bali ni gari kubwa kama V8 ,vxr nk, ambapo atapewa magari mapya kila baada ya miaka 5.
2. Rais mstaafu ameongezewa idadi ya madereva toka 2 na sasa atapewa 3.
3. Sheria ya sasa inataja gharama za mazishi kwa rais mstaafu tu, nyongeza iliyowekwa ni gharama ya mazishi kwa mwenza wake. Yaani kama rais mstaafu atafiwa na mke/mume wake, basi Serikali itagharamia mazishi hayo.
4. Makamu wa Rais mstaafu ameongezewa idadi ya magari kutoka gari 1, sasa atapata magari 2 yasiyopungua uzito wa tani 3 ambapo atapewa magari mapya kila baada ya miaka 5.
5. Makamu wa Rais mstaafu ameongezewa idadi ya madereva toka 1 na sasa atapewa madereva 2.
6. Makamu wa Rais atajengewa nyumba ya kifahari. Ikumbukwe, kwa sheria ya sasa, ni Rais mstaafu pekee ndiye anajengewa nyumba.
7. Sheria ya sasa inataja gharama za mazishi kwa Makamu wa Rais mstaafu tu, nyongeza iliyowekwa ni gharama ya mazishi kwa mwenza wake. Yaani kama Makamu wa Rais mstaafu atafiwa na mke/mume wake, basi Serikali itagharamia mazishi hayo.
8. Makamu wa Rais atapewa ulinzi yeye binafsi,na wana familia wake kama mke/mume na watoto. Ulinzi huu utatolewa na Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) kutokana na mabadiliko ya sheria ya TISS ya hivi karibuni.
9. Waziri Mkuu mstaafu ameongezewa idadi ya magari kutoka gari 1, sasa atapata magari 2 yasiyopungua uzito wa tani 3 ambapo atapewa magari mapya kila baada ya miaka 5.
10. Warizi Mkuu mstaafu ameongezewa idadi ya madereva toka 1 na sasa atapewa madereva 2.
11. Waziri Mkuu mstaafu atajengewa nyumba ya kifahari. Ikumbukwe, kwa sheria ya sasa, ni Rais mstaafu pekee ndiye anajengewa nyumba.
12. Sheria ya sasa inataja gharama za mazishi kwa Waziri Mkuu mstaafu tu, nyongeza iliyowekwa ni gharama ya mazishi kwa mwenza wake atakapofariki.
13. Waziri Mkuu atapewa ulinzi yeye binafsi,na wana familia wake kama mke/mume na watoto. Ulinzi huu utatolewa na Idara ya Usalama wa Taifa (TISS) kutokana na mabadiliko ya sheria ya TISS ya hivi karibuni.
14. Mjane wa Rais mstaafu, kwa sheria ya sasa anapata 40% ya mshahara wa rais aliye madarakani kila mwezi kama "maintenance allowance", asilimia hii imepanda sasa atalipwa 60%.
15. Sheria ya sasa inatoa gharama za matibabu kwa mjane wa Rais mstaafu kwenye hospitali za ndani ya nchi tu, lakini badiliko la sheria mpya, atalipiwa na Serikali matibabu ya hospitali za nje ya nchi pia.
16. Mjane wa Rais mstaafu ameongezewa huduma za gari toka gari moja mpaka magari mawili, na dereva 2 kufanya shughuli zake za kila siku. Serikali inalipia gharama za mafuta pia. Magari haya yatakuwa yanabadilishwa kila baada ya miaka 5. Pia, ameongezewa mpishi, mfua nguo na mtunza bustani. Atapata ulinzi wa TISS.
17. Mjane wa Makamu wa Rais, anapata stahiki kama za mjane wa rais isipokuwa tofauti yake ni moja, yeye atapata gari moja la Serikali na dereva mmoja.
18. Mjane wa Waziri Mkuu mstaafu anapata stahiki za ziada kama mjane wa Makamu wa Rais, isipokuwa gari analotumia la Serikali litakuwa linabadilishwa kila baada ya miaka 7.
19. Hili ni badiliko linalohusu Waziri, Naibu Waziri na Mwanasheria Mkuu wa Serikali wastaafu ambapo watapata ziada ya mafao yao: wind-up allowance, Diplomatic passport kwao na wenza wao, gari moja ambalo atapewa jipya kila baada ya miaka 5, Ulinzi wa TISS, Msaidizi mmoja, Bima ya Afya bure yeye na mwenza wake, Matumizi ya VIP lounge.
20. Hii ni nyongeza kwa Spika wa Bunge kwenye mafao yake: gari moja, Bima ya Afya yake binafsi, matumizi ya VIP lounge, pia anapata stahiki nyingine kama LITA 70 za mafuta kwa wiki.
NOTE: Pongezi kwa Wenza, walikuwa wanaishi kimaskini Sana !
View: https://www.youtube.com/watch?v=fYGKoLzTWRg
View attachment 2814342
Mungu hataniwi hata Siku moja na sio mtani wa yeyote duniani na hatarqjii kuwa mtani wa yeyote kodi za wanyonge ziheshimiweHongera Salma Kikwete bado watoto wenu waongezwe humooo.....umewasahau....low IQ sana na milelee
Hakika. Tunawajibika kupambania haki.Hata ubaguzi wa South Africa ulikuwa kisheria... Ni wananchi wanatakiwa wakatae Sheria za kuwanufaisha watawala kama ilivyokuwa kwa weusi waafrika kusini.
Ndio, wake wanatambuliwa wanne, kwa wenye imani ya Kiislamu, kwa wakristu ni mke mmoja kama una suria huyo utamhusumia kwa fedha za posho za safari.Hakika. Tunawajibika kupambania haki.
Kitu kingine, kwa wenye wake wawili kama mwinyi na ghalibu bilal sijui wake wote wawili watalipwa!
Tag Salima Babu Seya ......atakujibuuMungu hataniwi hata Siku sio mtani wa yeyote duniani na hatarqjii kuwa mtani wa yeyote kodi za wanyonge ziheshimiwe
Sio kisa tu mtu ana mamlaka anatakodi zote ziende kwake na familia yake
Mungu ana tabia ya upole lakini pia ni mkali na mkorofi kwa wakorofi waonea kodi za wanyonge kisa tu wana position juu