Salma Kikwete ataka Sheria ya Stahiki za wake wa Viongozi Wakuu

Salma Kikwete ataka Sheria ya Stahiki za wake wa Viongozi Wakuu

Good point. Kwanini iwe kwa tabaka la juu tu? wakati tabaka la chini ndio lina maisha magumu zaidi.

Wajifunze kupigania maslahi ya wengi. Ikiwezekana Wabunge wote waishi maisha,kupata mishahara ya walimu, polisi, machinga, mama ntilie kwa miezi mitatu kabla ya kwenda bungeni. Watajifunza uhalisia wa maisha.
 
Hakuna umuhimu huo kwakweli maana yeye sio kiongozi wa uma. Yeye ni mwenza tu.

Ukifanya hivyo unafungua mlango kwa wenza wa watumishi wengine nao kuhitaji mafao.

Mfano mke wa IGP, Mke wa CDF , mke wa DGIS, Mwenza wa kamisha na Magereza, Takukuru,Uhamiaji ,Zimamoto n.k. zote hizo ni nafasi za juu katika utumishi wa uma.

Kwa hali yetu ya kiuchumi hatuwezi kuhudumia watu wote hao.

Huo ni ufujaji wa fedha za wananchi. Watu waridhike tu na wanachopata kwenye maisha haya binadamu huwezi ukawa na kila kitu. Ni swala la kuridhika tu.

Mtu kama huridhiki hapo sasa kuna kitu kinaitwa tamaa.

Tamaa huzaa dhambi na malipo ya dhambi ni mauti.
 
Kiinua mgongo cha viongozi wastaafu huwa kinajumuisha na familia zao!! It’s assumed their wife’s cater for their families full time!!

Mke wa Kikwete anatakiwa aelimishwe!
Yeye Salma mafao yake yameunganishwa na mafao anayopata mumewe hivyo asitubebeshe Mzigo mwingine; hata hivyo yeye anapata mara mbili hivi sasa kule kwa mumewe na bungeni!! Atosheke na anachopata.
Sdhani kama anakuelewa
 
Hii Nchi ya ajabu sana yani Kijana Anakaa CHUO miaka 3 au 4 hadi Mi 5 akisoma anatoka pale anaambiwa na SERIKALI aji AJIRI Leo Mke wa Rais amekua na Mme wake 10 Years kwenye position yenye Fursa kibao za kufanya na za kumwingizia Mamilion ya Hela ila anataka Serikali imuandalie Mazingira mazuri ya yeye kama mke baada ya Mme wake kuacha Urais wapewe Posho hii inaingia akilini kweli?🤔
 
Du anataka bunge lijadili na kutunga sheria kwa watu kama watano hivi?
Mama Salma anajisahau sana.
Na watu wa jimbo lake wanafaidika vipi?.
Mfadhili mmoja nchini Kenya aliwahi kusema, watu wanakula na kufsidi misaada na hatimaye kuvimbiwa na kutapikia viatu vya wafadhili.
Naona hii ndio picha naiona ya mama Salma.
 
Habari!
Hii taarifa imenipata nikaona niilete kama ilivyo.

My Take: Yani wanataka kila kitu serikali iwaandalie yani hadi Future yao kweli?

Mbunge wa Mchinga (CCM), Salma Kikwete ameishauri Serikali kutengeneza utaratibu ama sheria ya kuwahakikishia stahiki zao wake na wenza wa viongozi wa juu, akiwemo Rais, mara baada ya wenzi wao kuchaguliwa kushika nafasi hizo.

Mbunge huyo ambaye ni mke wa Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete ameyasema hayo leo Ijumaa Aprili 22,2022 Bungeni Jijini Dodoma wakati akichangia katika makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora mwaka 2022/2023.

Amesema wake wa viongozi akiwemo rais, makamu wa rais na Waziri Mkuu mara baada ya wenza wao kushika nafasi hizo wanatakiwa kustaafu na kuendelea na shughuli nyingine.

Amesema kitendo hicho kinamaanisha kuwa utaalamu wake unatoweka.

“Ukiwiwa sana unaweza kusema hebu nianzishe Ngo (mashirika yasiyo ya kiserikali) lakini hata ukianzisha hakuna mtu anayeku suport ni wewe mwenyewe uhangaike ili kuhakikisha unapata raslimali ili uweze kuendesha Ngo,”amesema.

Ameomba Serikali kutengeneza utaratibu wa kisheria ambao mke wa kiongozi anapomaliza muda wake ajue ni nini anachotakiwa kukifanya.

“Ni imani yangu mtatengeneza utaratibu ama sheria inayomuhusu mke wa Rais ama wenza nini bada ya hapo kiendelee kufanyika ni jambo muhimu sana na si kwangu bali ni kwa vizazi vijavyo kujua haki zao,”amesema.

Chanzo: MWANANCHI
Huyu ingekuwa ameolewa na maskini angemtesa sana.
 
Tumbo la mwanadamu ni kama Bahar kila sku linaitaji kulishwa na halijai likaacha
 
Back
Top Bottom