Stroke
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 37,630
- 47,434
Hakuna umuhimu huo kwakweli maana yeye sio kiongozi wa uma. Yeye ni mwenza tu.Wao wanataka sheria zao sio hizo za Umma na nahisi wanataka ziitwe Sheria za wake wa Marais
Ukifanya hivyo unafungua mlango kwa wenza wa watumishi wengine nao kuhitaji mafao.
Mfano mke wa IGP, Mke wa CDF , mke wa DGIS, Mwenza wa kamisha na Magereza, Takukuru,Uhamiaji ,Zimamoto n.k. zote hizo ni nafasi za juu katika utumishi wa uma.
Kwa hali yetu ya kiuchumi hatuwezi kuhudumia watu wote hao.
Huo ni ufujaji wa fedha za wananchi. Watu waridhike tu na wanachopata kwenye maisha haya binadamu huwezi ukawa na kila kitu. Ni swala la kuridhika tu.
Mtu kama huridhiki hapo sasa kuna kitu kinaitwa tamaa.
Tamaa huzaa dhambi na malipo ya dhambi ni mauti.