Kufuata jistoria, je? Ni Wamaasai wameingilia hifadhi ya wanyama au wanyama waliwakuta Wamaasai pale?
Mbona hili jambo limeshikiliwa kidedea leo?
Hapa kuna siri kubwa. Kama kipindi cha mtawala fulani walijenga kwenye njia ya Tembo!! Kwanini tusiamini hata sasa kuna mtawala ana taka eneo???
Naanza kuamini kuwa hili sakata la Ngorongoro lina yaliyojificha nyuma ya pazia.
Kwanza kabisa, tukubali lipo tatizo la Uhifadhi Ngorongoro.
Tena tatizo kubwa.
Tatizo lenyewe ni Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.
Siyo Wafugaji wa Kimasai.
Nguvu ya rushwa inahamishia tatizo kwa Wafugaji, badala ya kulielekeza kwa Mamlaka ya Hifadhi.
Kwa nini?
Mbuga inayoingiza takriban Shs. Bilioni 150 kila mwaka, kwa nini wenyeji wa mbuga hiyo waishi kwa mashaka?
Wenyeji wa Hifadhi hiyo ni Wafugaji na Wanyamapori.
Kwa nini ishindikane kuboresha mazingira wakati kila mwaka pesa nyingi zinapatikana?
Let us focus on the corruption and inefficiencies of Ngorongoro Conservation Authority.
Kelele zote hizi zinaelekezwa kwa Wafugaji na rushwa inayotolewa na Viongozi wa Mamlaka.
Ambao wametoa Vibali haramu vya Ujenzi ndani ya Hifadhi.
Watanzania, tufumbueni macho tuone uhalisia.