- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Wakuu nimekutana na hii video lakini ni kama kilichoandikwa ni tofauti na kinachozungumzwa.
- Tunachokijua
- Salome Makamba amewahi kuwa mbunge wa viti maalum na mwanachama wa Chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kabla ya kuhamia Chama cha mapinduzi (CCM) mara baada ya bunge kuvunjwa.
Madai
Kumekuwa na kipande cha video kinachosambaa katika mitandao ya kijamii ikwa na grafiki yenye kichwa kinachosomea "Waliotaka kushindana na wewe waliishia kutekwa" huku video hiyo ikimuonesha aliyekuwa mbunge wa viti Maalum, Salome Makamba akizungumza mbele ya mgombea Urais kupitia CCM, Samia Suluhu Hassan kwenye kampeni mkoani Simiyu.
Uhalisia wa madai hayo
Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck kupitia marejeo ya video halisi umebaini kuwa kichwa kilichoandikwa kwenye grafiki ni tofauti kilichozungumzwa na Salome Makamba.
Salome katika mazungumzo yake mbele ya mgombea wa Urais wa CCM alimfananisha mgombea huyo na ua la uwaridi huku akielezaa kuwa waliojaribu kwenda kinyume na ua hilo wameishia kwenye mikono ya sheria.
“Mhe. Rais wewe kama uwaridi unayo miba ambayo ni sheria nzuri, kanuni, taratibu, mila na desturi ambapo pale ulipotaka kuonesha waridi lako kwa kuweka 4R walipotaka kukuchokoza waliishia kwenye mikono ya sheria.
Wewe kama ua zuri ulipotaka kuweka demokrasoa na uwanja sawa wa siasa wale ndugu zangu niliokuwa nao walipotaka kukuchokoza uliwaambia watakutana na miiba kabla ya hamjaliharibu waridi, leo hii wapo kwenye mikono ya sheria wanalia wameonewa. Wewe ni ua zuri kwa Tanzania.” - Salome Makamba, Mbunge na Mwanachama wa zamani wa Chadema