Salum Hamdun: Hakuna miundombinu ya reli Kilimanjaro iliyoharibiwa

Siungi mkono ubabe wowote lakini pia siungi mkono kusemana hovyo humu JF. Hapa ni mahali pa ma GT sio wambeya. Umeandika na weye kiumbeya ka huyo Sabaya alivyo kurupuka bila kuwaza. Acheni ugomvi tukae pamoja tuijenge nchi
 
Huyu mheshimiwa tangu amnyang'anye bwana mzee ofisi aligeuka kuwa shetani.
 
Hii ni kweli, si rushwa ya pesa tu hata ngono, kama mnamkumbuka yule mfanya biashara Sabaya alienda hotelini kulazimisha kulala na msanii Nandi !! Yule mfanya biashara mpaka ameikimbia nchi kwa sababu ya huyu mjinga Sabaya. Kwa bahati mbaya hata mamlaka za uteuzi nao ni wajinga wote wamekutana hakuna hatua itachukuliwa dhidi yake. Aibu sana kwa taifa
 
Hakuna chochote hapo, ni vita tu hiyo. Hakuna mwizi mjinga kiasi cha kudai milioni 2 kila mwezi na wakati hajashikilia chochote cha kutishia mtu. Ndio yaleyale ukitaka kuleta maendeleo, unaambiwa una mabomu ya nyuklia, unahatarisha dunia.
 
Siungi mkono ubabe wowote lakini pia siungi mkono kusemana hovyo humu JF. Hapa ni mahali pa ma GT sio wambeya. Umeandika na weye kiumbeya ka huyo Sabaya alivyo kurupuka bila kuwaza. Acheni ugomvi tukae pamoja tuijenge nchi
Nilidhani unapinga taarifa , kumbe unataka tumlinde Sabaya ! hilo halitawezekana
 
Huyu ni choko tu hamna madhara kwa wajanja,dc anaomba rushwa kwa kila mtu iwe hai mpka arusha mjini.ogopa tapeli sugu wa mtaani apewe ajira serikalini ni utapeli kila siku.
Kiboko yake ni cathbert swai wa asante tours alimvua boksa mchana kweupe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu DC ana matatizo.. Sijui Mh. Rais haoni matatizo yake au?? Hili sio tukio la kwanza la huyu jamaa. Yapo mengi ya aibu lakini hatuoni akichukuliwa hatua
Wengine wanakuwepoga si kwa sababu ya ukuu wa wilaya Bali kutimiza kile walicho tume,
 
Nashangaa wanatumbuliwa watu waaminifu kama Kangi halafu watu wapuuzi kama Naneya wanaachwa ofisini
 
Mwenzenu anataka ukuu wa mkoa, hizo timbwili zote ni kutafuta sifa, kwasababu alisifiwa hatosita kusema lolote kutafuta sifa.
 
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro limesema, hakuna hujuma wala uharibufu wa miundo mbinu ya Reli katika eneo la Kijiji cha Rundugai wilaya ya Hai, kama ilivyoelezwa na Mkuu wa wilaya hiyo ,Lengai Ole Sabaya
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro ,Kamishna Msaidizi wa Polisi ,Salum Hamdun, amesema kuwa baada ya DC kutoa tuhuma hizo na kuagiza wafanyabiashara wawili wa Mabasi ya Abiria, kujisalimisha polisi, walitii agizo hilo na baada ya kutoa maelezo walitoka kwa dhamana.

"Uchunguzi wa awali umebaini kuwa hakuna miundombinu ya Reli iliyoharibiwa au kuhujumiwa katika himaya hii kwa maana ya kipande cha kutoka Moshi kuelekea Arusha, ambapo mpaka sasa kimeshakarabatiwa kwa Kilomita 23 na kazi inaendelea" amesema RPC Kilimanjaro.

January 19, 2020, Mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya, akiwa katika kijiji cha Rundugai akikagua ukarabati wa Reli, alitoa agizo kwa wafanyabiashara wawili wa mabasi ya Lim Safari na Machame Safari ambao ni Rodrick Uronu na Clemence Mbowe, kujisalimisha katika kituo cha Polisi cha Bomang'ombe kwa tuhuma za kuunda genge la uhalifu ili kuathiri usafiri wa Treni ya abiria kati ya Dar es Salaam ,Moshi na Arusha.


Source EATV
 
Shirika la reli ndio lilitakiwa kutoa tamko sio RPC
 
Moderator kichwa cha habari kiwe RPC wa Kilimanjaro badala ya Hamdun , wengine wanaweza kudhani huyo hamdun labda ni msela tu kaamua kujitokeza jf , hii habari ni kubwa sana , sijawahi kuona DC muongo kwa kiwango cha hatari kama huyu kwa kadri ya kumbukumbu zangu
 
Kama RPC ameshakanusha, nini kitakachofuata? Bwana Sabaya ataendelea kuachwa huru ili amsakame Mbowe mwingine? Je kuitwa Mbowe ni "abomination" kiasi ambacho unastahili kuwa "condemned"?

Je ni halali kutafuta utukufu wa duniani "at the expense of reputation" za watu ambao wamechukua muda mrefu kuzijenga? Je bwana Sabaya ana "Diplomatic Immunity???
 
Hivi Shamba la Mbowe mboga hazikubaki akazing'oe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…