Uchaguzi 2020 Salumu Mwalimu: Biashara zote za Serikali kubinafsishwa

Uchaguzi 2020 Salumu Mwalimu: Biashara zote za Serikali kubinafsishwa

Kuna huduma ambazo kwa asili ya unyeti wake ni vyema zitolewe na serikali kama usafiri wa treni na ndege, uzalishaji wa umeme, mifuko ya hifadhi ya jamii na usambazaji wa maji.

Ila kwa Tanzania hizo huduma kuwa mikononi mwa serikali imekuwa ni tatizo kubwa sana na mashirika husika yamekuwa yakigeuzwa kuwa sehemu ya watu kujitafutia utajiri.

Inatakiwa utaratibu mzuri uandaliwe utakaowezesha mashirika yanayotoa huduma hizo kufanya kazi bila kuhujumiwa na wakora kwani huduma hizo zinapotolewa na sekta binafsi gharama hua hazishikiki.

Lakini kwa hii sera ya Magufuli ya kutaka sasa serikali ifanye hata biashara ya kuuza mafuta, uwakala wa mizigo na ukandarasi ni ovyo kabisa na tunaipinga kwa nguvu zote kwani ktk dunia ya sasa serikali haipaswi kufanya biashara bali kuratibu na ukusanyaji kodi tu.
 
Kama hamjaelewa ulizeni mtaeleweshwa.. Upotoshaji hautawafikisha popote
Mwanasiasa maelezo atoayo hasa kwa Salum Mwalimu ni "self explanatory ", Salum Mwalimu ni muungwana hana hila na anaipenda Tanzania. Ana makuzi mazuri hapendi uongo! Bahati mbaya tu kaangukia kwenye mikono ya wenye hila. Ila kwa mapenzi yake kwa nchi yake na watanzania amelazimika kufunua hila za hao walio"mteka nyara" kisiasa. Kijana wa wetu watanzania Salum Mwalimu tumpongeze na kumsaidia kwa kila linalowezekana aweze kudhibiti hila za hao waliomteka " kisiasa" huko huko alipo. Ameanza vizuri sana kwa kufunua nia ovu ya hao wenye hila huko huko alipo. Na tunawatahadharisha hao wenye hila Salum asiguswe!

Mkuu, Mshana Jr, upo !? Nasikitika kwa kitendo ulichokifanya cha kumsusa " kijana wa Rondo" wa huko kusini mwa nchi yetu. Umeamua kuukimbilia " Msala" unaopita huku ukiuacha "Mbachao" umeinama kwa majonzi. Mkuu, umefanya vibaya nakulaumu.
====
Tuendelee na mjadala ulipo mezani. Ha ha ha aaaa!
 
Unajua maana ya alichosema yaani "Sera"
Neno sera si neno la kilatini kusema kuwa likitafsiriwa na watu mbali mbali wa lugha tofauti linaweza kuwa na maana iliyopotoshwa kutokana na utafsiri huo. Sera ni neno la kiswahili sanifu kabisa. Nawatahadharisha msimguse Salum Mwalimu kwa kuonyesha hila za hao mnaowafuata!!!
 
Mwandishi wa Gazeti la Mwananchi amemnukuu Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais Chadema akieleza sera ya Chama chao kuwa ni kubinafsisha biashara zote ili ziendeshwe na sekta binafsi. Amesema Serikali itabaki na jukumu la kutunga Sera tu.

My Take:
Nadhani upo umuhimu wa wataalamu kuwasaidia vyama vya siasa na wagombea mambo muhimu na yaliyotafitiwa ya kuyaongelea kwenye kampeni.
Acha afe kibudu ,hatusaidii huyo ,ni mzigo kwa taifa
 
Hatuwezi kufanya majaribio kwa nchi nzima. Watanzania ni waelewa sana!
====
Kwamba Tanesco itabinafsishwa, TTCL, ATCL, TRC, nakadhalika....! Vyote watapewa " wakwepuaji" wa chama cha Mbowe,Chadema! Maajabu hayeshi!

Chadema wataruhusu " sector" BINAFSI kuendesha biashara hizo sambamba na Serikali kwa SHERIA, TARATIBU, MIONGOZO na KANUNI zinazofanana.

Kama ni mitaji, Serikali itatoa kwa "Sector" zote kwa masharti yanayofanana.

Mfano:- ATCL, TTCL, VODA, FASTJET, PRECISION, TIGO na HALOTEL zitafanya BIASHARA katika UWANJA MMOJA, REFA MMOJA na SHERIA MOJA.
 
Neno sera si neno la kilatini kusema kuwa likitafsiriwa na watu mbali mbali wa lugha tofauti linaweza kuwa na maana iliyopotoshwa kutokana na utafsiri huo. Sera ni neno la kiswahili sanifu kabisa. Nawatahadharisha msimguse Salum Mwalimu kwa kuonyesha hila za hao mnaowafuata!!!
watamtenga
 
Mwandishi wa Gazeti la Mwananchi amemnukuu Mgombea Mwenza wa Kiti cha Urais Chadema akieleza sera ya Chama chao kuwa ni kubinafsisha biashara zote ili ziendeshwe na sekta binafsi. Amesema Serikali itabaki na jukumu la kutunga Sera tu.

My Take:
Nadhani upo umuhimu wa wataalamu kuwasaidia vyama vya siasa na wagombea mambo muhimu na yaliyotafitiwa ya kuyaongelea kwenye kampeni.
Certificate in journalism atajua kuendesha saccos tuu, nchi asahau.
 
1. MAGUFULI ALISEMA ANATAKA MATAJIRI WAISHI KAMA MASHETANI.

2MAGUFULI ALISEMA AKIWA RAIS WA TANZANIA WATANZANIA TUTALIMIA MENO.

Utakuwaje kiongozi wa Malaika kama unataka matajiri waishi kama mashetani.
Toka amekuwa rais ni mwananchi gani aliwahi kulimia meno? Muwe mnaelewa misemo siyo kukurupuka Kama Lissu.
 
Wanasiasa huwa mara nyingi wanaongea vitu katika mtazamo wa kisiasa na sio katika uhalisia Kuna vitu wanavozungumza havina uhalisia kabisa
Shida ndio hiyo tunadhani siasa ni uongo ! Mtu anakumbia vitambulisho ni Muhimu unashagilia , vitambulisho siyo lazima unashangilia , vitambulisho vinatumika kutoa mikopo unashangilia wakati havina jina,picha wala saini ya mmiliki .
 
Back
Top Bottom