kedekede
JF-Expert Member
- Aug 21, 2016
- 5,313
- 7,714
Tuna ni samaki wa kawaida na anapatikana bahari ya hindi.Kwa kiswahili anaitwa Jodari,Wapo ain mbili kuu hawa Tuna fish.Kuna weusi wakubwa Albacore na kuna wale wenye mkia na mabawa ya njano ambao wanitwa yellow fin Tuna.Japo yapo makundi mengine ila haya mawili ndiyo maarufu,na yote yapo Tanzania.Tuna anaweza kuwa kafupi ila kameshiba na kanaweza kufika kg 50 na kuendelea hasa hawa Albacore
Vituna vidogo ambavyo havikui sana vinaitwa sehewa kwa kiswahili.Nyama ya Tuna ni nyekundu na inatumika sana kwenye mapishi ya kuliwa wabichi.Tuna hatakiwi kuiva sana hata kama atapikwa.Tuna anatumika kwenye vyakula kama Carpaccio na shashimi huwa ni vyakula vibichi.Anatumika sana kwenye mapishi ya kijapan na ni ghali kwa sababu ya kuwa samaki ambao sio wengi.Hata hivyo hadi awe ghali hivyo inategemea amevuliwa kwa utaratibu upi.Ili awe ghali ni lazima nyama yake ibaki kuwa nyekundu.Wavuvi wa huko kwa wenzetu wako well equiped wakimvua tu samaki huyu anawekwa kwenye cooler box ambayo ina barafu hadi watakapo mpeleka kwa mnunuzi siku hiyo hiyo kabla hajaganda..Sisi wavuvi wanakaa hukooo weee hadi jioni samaki ameshabadilika Rangi.Hawezi kuwa na thamani hiyo hata mara moja.