Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Kwenye hoteli kubwa zote, na nyingi za kati menu ya chakula kikuu huwa ni samaki, kuku, nyama ya ng'ombe, mbuzi kitimoto na nyinginezo halafu ndio unachagua utakula na nini ikiwa ni ugali, wali, viazi n.k
Kwenye hizi hoteli bei ya chakula inapimwa kwa samaki, kuku na nyama kisha (wanga) ambao ni ugali, wali, ndizi, viazi n.k inakuwa nyongeza tu, ina maana hata usipokula wanga utalipa bei ile ile tu ya nyama, kuku au samaki. Kama wewe sio mla nyama bei itabadilika.
Sasa kwa mama ntilie inakuwa kinyume chake, chakula kikuu ni wanga ambao ni ugali, wali, ndizi n.k halafu nyama, kuku, samaki inakuwa kama nyongeza tu. Halafu huwezi kusema unataka kula nyama, kuku au samaki tu, ukitaka hivyo huwezi kuuziwa chakula na inaweza kuzua hata ugomvi!
Na nyumba nyingi za Watanzania ulaji ni kama huo wa mama ntilie, hii inaweza kumaanisha uduni wa maisha japo tunajigamba kuwa na chakula kingi.