Samaki, nyama, kuku na maharage kuliwa kama mboga ni dalilli ya umaskini?

Samaki, nyama, kuku na maharage kuliwa kama mboga ni dalilli ya umaskini?

Babu zetu wa kipindi gani? Babu zetu waliokuwa wawindaji na wala matunda ya porini?
Hizo Ng'ombe na mbuzi zilitoka wapi? Hizi bahari na Maziwa zilikua hazitoi Samaki, kwamba walikua hawatumii samaki? Huo ugali na wali vilitoka wapi?
 
Inaitwa Olympic breakfast inakuwa na mchanganyiko wa
  • Soseji
  • Mayai mawili ya kukaanga
  • Uyoga
  • Viazi vilivyokaangwa vikakauka vizuri ama chips
  • Nyanya kipande unaila ikiwa mbichi
  • Maharage yasiyokaangwa
  • steak ndogo ya kipande cha nyama sio mbaya sana
  • Mkate pia ukiweka slace mbili sio kesi.
 
Attachments

  • images (8).jpeg
    images (8).jpeg
    49.7 KB · Views: 5
Kwenye hoteli kubwa zote, na nyingi za kati menu ya chakula kikuu huwa ni samaki, kuku, nyama ya ng'ombe, mbuzi kitimoto na nyinginezo halafu ndio unachagua utakula na nini ikiwa ni ugali, wali, viazi n.k

Kwenye hizi hoteli bei ya chakula inapimwa kwa samaki, kuku na nyama kisha (wanga) ambao ni ugali, wali, ndizi, viazi n.k inakuwa nyongeza tu, ina maana hata usipokula wanga utalipa bei ile ile tu ya nyama, kuku au samaki. Kama wewe sio mla nyama bei itabadilika.

Sasa kwa mama ntilie inakuwa kinyume chake, chakula kikuu ni wanga ambao ni ugali, wali, ndizi n.k halafu nyama, kuku, samaki inakuwa kama nyongeza tu. Halafu huwezi kusema unataka kula nyama, kuku au samaki tu, ukitaka hivyo huwezi kuuziwa chakula na inaweza kuzua hata ugomvi!

Na nyumba nyingi za Watanzania ulaji ni kama huo wa mama ntilie, hii inaweza kumaanisha uduni wa maisha japo tunajigamba kuwa na chakula kingi.
Wrong totally wrong.
Kula samaki,kuku au nyama kama mboga ni tamaduni kwa vyakula vya Afrika na Asia.
Hiko sio kigezo cha umasikini.
Kuna nyumba zipo wali samaki kila mmoja na sato wake mzima na kama wali kuku kila mtu kuku robo na kama wali nyama kila mmoja bakuli la nyama limejaa.
Umepimia kizembe sana.
Japo suala la lishe bora linahusika.
Maana kilishe bora mtu mmoja hatakiwi kula zaidi ya nusu kilo kwa wiki kwa nyama nyekundu.
Kula kwa wingi labda samaki na nyama nyeupe(nyama za ndege mathalan kuku).
Japo Tanzania asilimia kubwa hatuli kilishe tunakula kushiba.
 
Kikubwa ule ushibe tumbo ndiiiiiiii mkuu maana ukifatiria habr za mlo kamili hii ni changamoto nyingine mtu huwezi mwambia eti ale matunda tu usiku kama ujataka ngumi apo usimwambie izo habr za kuamka akiwa na njaaa😂😂😂
 
kuna sehemu nilitaka kununuA nyama choma peke yake, nikaambiwa lazima ninunue na ugali
Hii imewahi kunitokea mkoa wa Mara wilaya ya Bunda, nilienda sehemu wanachoma nyama nikaagiza nyama nikashangaa njemba inakuja na ugali kwenye kijimfuko ugali una rangi sijui kahawia ile sijui nyekundu hata sikumbuki vizuri.
Nikamwambia sijaagiza ugali, akasema sasa unakulaje. Nikalipa nyama yake nikaenda sehemu ya chakula nikaachana na mambo ya kuchoma nyama.
 
Inaitwa Olympic breakfast inakuwa na mchanganyiko wa
  • Soseji
  • Mayai mawili ya kukaanga
  • Uyoga
  • Viazi vilivyokaangwa vikakauka vizuri ama chips
  • Nyanya kipande unaila ikiwa mbichi
  • Maharage yasiyokaangwa
  • steak ndogo ya kipande cha nyama sio mbaya sana
  • Mkate pia ukiweka slace mbili sio kesi.
Hiyo kwa mtzed wa kawaida kuipata daily ngumu
Halafu Kuna wale wa kula viporo washibe ndi ndi ndi
Hawa hawataiweza hii
 
sasa mura sisi huku tarime tunagonga kichuri kwa ugali wa muhogo/mtama
 
Kwenye hoteli kubwa zote, na nyingi za kati menu ya chakula kikuu huwa ni samaki, kuku, nyama ya ng'ombe, mbuzi kitimoto na nyinginezo halafu ndio unachagua utakula na nini ikiwa ni ugali, wali, viazi n.k

Kwenye hizi hoteli bei ya chakula inapimwa kwa samaki, kuku na nyama kisha (wanga) ambao ni ugali, wali, ndizi, viazi n.k inakuwa nyongeza tu, ina maana hata usipokula wanga utalipa bei ile ile tu ya nyama, kuku au samaki. Kama wewe sio mla nyama bei itabadilika.

Sasa kwa mama ntilie inakuwa kinyume chake, chakula kikuu ni wanga ambao ni ugali, wali, ndizi n.k halafu nyama, kuku, samaki inakuwa kama nyongeza tu. Halafu huwezi kusema unataka kula nyama, kuku au samaki tu, ukitaka hivyo huwezi kuuziwa chakula na inaweza kuzua hata ugomvi!

Na nyumba nyingi za Watanzania ulaji ni kama huo wa mama ntilie, hii inaweza kumaanisha uduni wa maisha japo tunajigamba kuwa na chakula kingi.
Unataka watu wakufe?
 
Kitendo cha kuwa na jamii yenye chakula alafu kuna kitu kinaitwa mboga ni dalili ya umaskini. Yaani mfano Scotland au Northern England kama sisahau wao chakula common cha asili ni chips samaki. Ulaya Mashariki nchi nyingi wanakula siagi, viazi na kushushia wine kidogo wale watu wa chini wasioishi kisasa. Wachina wanakula wali hata supu yake ipo wakichanganya na makorokoro mengine, wanapenda kitimoto pia.

Wote hao hakuna anayesema wali na mboga ya kitimoto, chips na mboga ya samaki. Bongo ukisema chakula imezoeleka ni kama wali, ndizi na ugali then ndio utaje mboga gani ipo. Kule ukisema chakula hautaji tena mboga, yani nyama, ngano, samaki, wali, matunda, maziwa, wine na mbogamboga vyote ni vyakula. Hawachukui bonge la ugali na maharage kibakuli kidogo wakasema ni mboga. Wanaweza kula samaki mkubwa na kachapati kamoja, huku ukifanya hivyo unakuwa "umejitoa out" au mroho au wakishua.
 
Tunashiba makapi mkuu, ukweli mchungu huo. Inawezekana 80% ya chakula tinachokula kinaishia chooni as hakina nutrients muhimu kwa miili yetu, ndio maana kuna watu wanaenda chooni hata mara tatu kwa siku.
Mkuu ukila vizuri ndio unaenda chooni mara nyingi, ulaji mbaya wa kufakamia wanga kama ugali, wali na chapati kwa wingi huku inayoitwa mboga ikiwa kidogo ndio huwafanya watu waende chooni mara chache sana au hata kupata constipation kabisa.
 
Hiyo kwa mtzed wa kawaida kuipata daily ngumu
Halafu Kuna wale wa kula viporo washibe ndi ndi ndi
Hawa hawataiweza hii
Viporo vinapunguza gharama sana, wali maharage ya jana inapashwa watoto wanakula, badala ya kununua mikate sijui maandazi..hayo ndio maisha ya mtanzania wa kawaida

Kifupi sisi tunakula kujaza tumbo, sio kupata lishe/mlo kamili.
 
Inaitwa Olympic breakfast inakuwa na mchanganyiko wa
  • Soseji
  • Mayai mawili ya kukaanga
  • Uyoga
  • Viazi vilivyokaangwa vikakauka vizuri ama chips
  • Nyanya kipande unaila ikiwa mbichi
  • Maharage yasiyokaangwa
  • steak ndogo ya kipande cha nyama sio mbaya sana
  • Mkate pia ukiweka slace mbili sio kesi.
Hii ndio breakast sasa, hizo nyingine ni chai tu.
 
Hii imewahi kunitokea mkoa wa Mara wilaya ya Bunda, nilienda sehemu wanachoma nyama nikaagiza nyama nikashangaa njemba inakuja na ugali kwenye kijimfuko ugali una rangi sijui kahawia ile sijui nyekundu hata sikumbuki vizuri.
Nikamwambia sijaagiza ugali, akasema sasa unakulaje. Nikalipa nyama yake nikaenda sehemu ya chakula nikaachana na mambo ya kuchoma nyama.
Hiyo njemba maisha yake yote inajua ugali ndio chakula, nyama ni mboga tu. Wewe kutaka nyama bila ugali ilikuwa kama surprise
 
Back
Top Bottom