Samaki wa kupaka (grilled fish with coconut sauce)

Samaki wa kupaka (grilled fish with coconut sauce)

Afu mi ili nifaidi napikaga sato mkubwa na kiugali kidogo japo ugali matonge mawili nakula
 
farkhina ahsante yani samaki napenda sana kwa wiki zaidi ya mara 3 lazima nile ila si wajua usela sina oven so nampika kama unavyosema ila simgril anakuwa mbichi na mtamu balaa.Watu wanashangaaga kwa nini mbichi afu hana shombo?ha ha ha mapishi mwaya.
Shem wako juzi kaniambia kanunua oven yani atanikoma mapishi na hivi apenda kula mapenzi yatazidi wallah atatangaza ndoa lol

Hahahaha umpikie mapishi yote lol....
Mie natafuta viwalo kabisa vya kuvaa siku ya harusi yako..😉😉😉😉
 
Last edited by a moderator:
farkhina ahsante yani samaki napenda sana kwa wiki zaidi ya mara 3 lazima nile ila si wajua usela sina oven so nampika kama unavyosema ila simgril anakuwa mbichi na mtamu balaa.Watu wanashangaaga kwa nini mbichi afu hana shombo?ha ha ha mapishi mwaya.
Shem wako juzi kaniambia kanunua oven yani atanikoma mapishi na hivi apenda kula mapenzi yatazidi wallah atatangaza ndoa lol
aki ya mama wadafa bwana mnatupatia sana kwenye menu..
 
Last edited by a moderator:
Huna haja ya kukuna nazi kwa raha zako......

yaani dia mie nimeenda sokoni nshanunua 3 napikia mojamoja chakula cha peke yangu nishanunua njegere za kesho,maharagwe ninayo ndani yaani kwa kweli bakhresa amesaidia sana.Karibu maini rost na spagheti natamani kuweka recipe ila nasikia uvivu nkiwa fresh nitarusha hewani.
 
Ahsante nlivokua na njaa saivi na kuzurura huku...leo nakuja kula huko lol
 
shukran farkhina.samaki wa mishkaki ni msosi niupendao sana ila sijui huwa mnapikaje.hapo juice ya Hanjal lazima ihusike

Ntaweka recipe yake....
Ni rahisi tu kupika
 
Mahitaji

1)Samaki mkubwa...
2)nyanya 2..
3)kitunguu thomu 1 teaspoon..
4)tangawizi 1 teaspoon
5)bizari ya njano kiasi
6)bizari ya pilau 1 teaspoon...
7)ndimu 2...
8)kitunguu maji 1..
9)chumvi kiasi
10)pilipili manga 1 teaspoon
11)pilipili mbuzi 1
12)tomato sauce
13)tui la nazi 1-1.5 kikombe...

Namna ya kutaarisha samaki

1)safisha vizuri samaki wako na umeweke alama kwa kisu ili viungo viingie ndani ya samaki..muache akolee viungo for 30minutes

2)weka samaki kwenye trey na umuunge kwa pilipili manga,chumvi,ndimu 1,bizari ya pilau,kitunguu saumu na tangawizi...

3)muweke kwenye oven moto kiasi ili awive vizuri....akiwiva upande mmoja mgeuze upande wa pili...

4)ukishawiva pande zote mbili weka samaki kwenye sahani.....

Namna ya kutaarisha sauce

1)saga nyanya,pilipili mbuzi na kitunguu maji weka maji kidogo sana au unaweza tumia tui badala ya maji..

2)weka tui jikoni,mimina mchanganyiko wako uliosaga,weka na bizari...koroga na wacha vichemke vizuri

3)weka tomato paste kiasi ili sauce iwe nzito nzito...

4)weka ndimu....acha ichemke kwa dakika 5 then epua

5)mimina sauce yako juu ya samaki ulimtaarisha kabla

Samaki wa kupaka (grilled chicken with coconut sauce) tayari kwa kuliwa...

Sasa best kama huna oven,unaweza kumkaanga???
 
Sasa best kama huna oven,unaweza kumkaanga???

Mpenzi kama una ile grill ya mkono ya kubanika samaki, ni vizuri sana ukamchoma na makaa kwenye seredani. Anakua very taste.

Na hayo ndo mapishi haswa ya kizamani. Sikuizi sema hatuna hayo maseredani ndo mana tunatumia ovens
 
Back
Top Bottom