Samata mishahara ya milioni 400 kwa mwezi iko wapi? Hatuoni maendeleo

Samata mishahara ya milioni 400 kwa mwezi iko wapi? Hatuoni maendeleo

ubarinolutu

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2012
Posts
2,424
Reaction score
4,954
IMG_7803.jpeg


Najiuliza hili swali nashindwa kupata jibu, kati ya wachezaji waliopata mafanikio makubwa na muda wote toka Tanzania iumbwe na Toka kabla makubaliano ya bandari hayajafanyika ni Mbwana Samata, amecheza vilabu vinginna vikubwa , lakini Nina swali dogo.

Mbwana alivofika ulaya alikuwa akipokea mshahara mkubwa na marupu rupu nje ya mshahara, kwa mshahara wake tu alikuwa akilipwa kwa mwezi takribani milioni 450 za Kitanzania, ukitoka Kodi na matakataka mengine anabaki na kama milioni 350 hapo nje ya marupu rupu.

Tunaomjua karibu Samata tunashindwa kuelewa kuwa zaidi ya nyumba ya Kigamboni hatujaona amefanya chochote cha maana na chakueleweka na ndio anafikia mwisho wake. Tofauti na wenzie kina Adebayor, Mane, ambao wameweka alama lakini wamefanya uwekezaji mkubwa sana.

Kama Samata ameshindwa kumanage funds alizopata na anazopata, basi Watanzania inabidi tujiangalie na tujiterekebishe. Katika hili hatuwezi kumlaumu Wema Sepetu, wala Irene Uwoya kwakuwa Samata alikuwa si mtu wa hizo mambo.

Natoa hoja.
 
Usiwadharau watu, wala usiwakebehi, wala usiwafanyie dhihaka, kwani haujui vipi itakuwa hali yako kesho.
Kuwa makini, leo usiwe ni katika watukanaji, kesho ukawa ni miongoni mwa waliopewa mtihani.

Tuhifadhini ndimi zetu.

Ijumaa Mubarak
 
Samata ametokea Mbagala na sie tunaoishi uswahili tunajua maana halisi ya Husda

ana haki ya kuwa na faragha kwny maisha binafsi

kwanini una hamu ya kujua mafanikio yake badala ya kujua changamoto zake ili zikupe funzo namna ya kujikwamua utoke hapo ulipo
 
Umejibiwa na wengi kwamba mtu atumiavyo pesa zake ni suala binafsi.

Na pia ujue sio uwekezaji wote huonekana na umma. Kuna mambo kama hatifungani, mifuko ya unit trusts, hisa, nk mtu anaweza kuweka kitita akajua mwenyewe.
 
Back
Top Bottom