Samatta hatomaliza misimu miwili ndani ya Ligi Kuu ya Uingereza (EPL)

Najua nitashambuliwa kwasababu watanzania hatupendi kuambizana ukweli, hata uone mapungufu ya wazi kabisa tuko radhi tukayaseme pembeni au kukaa nayo kimya.

Kwanza nampongeza alipofika na apangacho Mungu lazima kitimie, inawezekana alipangiwa kufika hapo alipo, lakini pia kwenye maisha kuna suala na bahati, inawezekana kafika hapo kwa bahati aliyonayo ukiondoa juhudi na maarifa.

Twende kwenye hoja, ukiangalia Samatta aina yake ya ushambuliji utagundua ni mtu wa kutengenezewa kila kitu yani apikiwe, apakuliwe yeye aje kula tu, ligi ya EPL inataka uhangaikaji, utafutaji na sometimes hata kama wewe ni mshambuliaji basi ujue kujitengenezea pia. Ukiangalia magoli ya Samatta toka alipokua Genk utagundua ni mzuri sana kumalizia, yani yeye ni mipira ya kichwa, kama ni mguu basi ile one touch nyavuni, hakuna kujitengenezea wala kujitafutia.

Ndio maana tumeanza kusema ooh anabaniwa pasi, hakuna kitu kama hicho, angalia game zote mbili hakuna sehemu ametafuta, zote alikua na mtu anaezengea zengea golini, kibongo bongo tunaita kuibia [emoji1][emoji1]. Sasa kwa wenzetu hata wachezaj wenzie wanamchora tu ni rahisi kumuona aah jamaa anasubiri tumpelekee haya aendelee kusubiri, sasa sisi tunatafsiri kama wanambania

Lakini pia Samatta akisema aanze mashambulizi ya kujitengenezea utagundua anawahi sana kuchoka, hana pumzi na hapo ndio linakuja suala la kuongeza juhudi kwenye kijijengea pumzi, tusishangae akianza kutokea benchi round ya pili ikianza. Yote ya yote kijana anajituma anastahili pongezi.

Wenzetu wale hawakawii kukuuza kwa mkopo wakiona mambo sio mambo..
Jamaa ulisema kweli watu wakakuwakia kinoma
 
Ila Waingereza bana wana vimambo mambo vyao vya ubaguzi

Sasa yule Davis kamzidi nini Samatta? Angalau hata Samatta alifunga magoli mawili lile jamaa halijafunga kabisa afu juzi wameliongezea mkataba au kwasababu ni mtoto wa kwao ndomana wanakaa kimya
Sumatta hakutakiwa kwa sababu hakuwa mwenzao, wenye kunielewa watanielewa kwenye mpira kuna mambo mengi zaidi ya mpira, mpira ni sehemu mojawapo ambayo inatumika kurecruite kwenye mambo yetu yale, sasa wachezaji mpira wenzako wakikuona sio mwenzao ni ngumu kukupa ushirikiano, Samatta alizike na hapo alipofikia kuliko kujiunga nawo, maana huko hakuna mlango wa kutokea upo mlango wa kuingia tu.
 
Najua nitashambuliwa kwasababu watanzania hatupendi kuambizana ukweli, hata uone mapungufu ya wazi kabisa tuko radhi tukayaseme pembeni au kukaa nayo kimya.

Kwanza nampongeza alipofika na apangacho Mungu lazima kitimie, inawezekana alipangiwa kufika hapo alipo, lakini pia kwenye maisha kuna suala na bahati, inawezekana kafika hapo kwa bahati aliyonayo ukiondoa juhudi na maarifa.

Twende kwenye hoja, ukiangalia Samatta aina yake ya ushambuliji utagundua ni mtu wa kutengenezewa kila kitu yani apikiwe, apakuliwe yeye aje kula tu, ligi ya EPL inataka uhangaikaji, utafutaji na sometimes hata kama wewe ni mshambuliaji basi ujue kujitengenezea pia. Ukiangalia magoli ya Samatta toka alipokua Genk utagundua ni mzuri sana kumalizia, yani yeye ni mipira ya kichwa, kama ni mguu basi ile one touch nyavuni, hakuna kujitengenezea wala kujitafutia.

Ndio maana tumeanza kusema ooh anabaniwa pasi, hakuna kitu kama hicho, angalia game zote mbili hakuna sehemu ametafuta, zote alikua na mtu anaezengea zengea golini, kibongo bongo tunaita kuibia [emoji1][emoji1]. Sasa kwa wenzetu hata wachezaj wenzie wanamchora tu ni rahisi kumuona aah jamaa anasubiri tumpelekee haya aendelee kusubiri, sasa sisi tunatafsiri kama wanambania

Lakini pia Samatta akisema aanze mashambulizi ya kujitengenezea utagundua anawahi sana kuchoka, hana pumzi na hapo ndio linakuja suala la kuongeza juhudi kwenye kijijengea pumzi, tusishangae akianza kutokea benchi round ya pili ikianza. Yote ya yote kijana anajituma anastahili pongezi.

Wenzetu wale hawakawii kukuuza kwa mkopo wakiona mambo sio mambo..

Mzee kiona mbali
 
Hakuna mchezaji aliekuwa wa kuandaliwa mpira kama Ronaldo de Lima ila alitoboa vizuri sana!
Humjui R9 vizuri wewe!!! Ronaldo aliyekuwa na uwezo was kupangua backline nzima na kipa juu ama unamzungumzia delima yupi!! Na vijana wengi miaka hiyo tuliipenda Brazil kwa sababu ya uchezaji wa Rinaldo de Lima.
 
Back
Top Bottom