Sambusa za nyama na juice ya matunda

Mwachiluwi

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2022
Posts
25,258
Reaction score
48,589
Leo tujifunze hii kitu sambusa za nyama

MAHITAJI
Unga wa ngano
Nyama
Hoho
Karoti
Chumvi
Mafuta

Kwanza chemsha nyama yako kisha isage vizuri
Then chukua ngano weka mafuta na chumvi anza kukanda mimi natengeneza za kula mwenyewe so nilitumia unga nusu


Baada ya hapo ngano yako ulio kanda ipumue kidogo kisha kata na utengeneze madonge kama ya chapati

Baada ya hapo anza kusukuma moja moja iwe kama chapati hakikisha isiwe nzito

Baada ya hapo andaa sahani pembeni weka unga kwenye sahani kisha weka chapati yako kwenye sahani

Na ukiwa unaweka unazibebanisha juu yake unapaka mafut kama ivyo ili ukija babua inakuwa ni vyepesi kuzitoa

Ukimaliza hapo chukua kidogo mimi nilichukua kama chapati tatu zikiwa zimebebana nikazisukuma tena

Baada ya hapo unakata kwa njia ya msalaba kama hivi

Baada ya hapo unaenda kubabua

Weka pole pole ukimaliza kubabua njoo uziachanishe kama hivi
Baada ya hapo nikachukua nyama nilio isaga na kuikaanga nilichanganya pilipili karot na hoho

Baada ya hapo chukua sasa vipande vyako na ulivyo achanisha kunja kama hivi na uweke nyama kidogo tu usijaze mpaka juu

Na kunja vizur hakikisha hakuna pembe ya sambusa inayo weza fanya mafuta yaingie ndani

Kisha zikaange kwenye mafuta yalio chemka ili zisinyonye mafuta na ziwe za kawahawia

Zilikuwa mzuri sana

Juice mnajua kusaga nitawapa mahitaji tu
Embe moja
Nanasi moja
Passion matatu

 

Attachments

  • RPReplay_Final1739448856.mov
    4.5 MB
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…