Same: Ajali yaua watu saba wa familia moja

Same: Ajali yaua watu saba wa familia moja

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2021
Posts
577
Reaction score
2,595
Watu saba wa Familia moja akiwemo Ofisa Uhamiaji wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), Sylvester Chambo na wanae wanne wamefariki dunia papohapo huku wengine wanane wakijeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na gari jingine Wilaya ya Same, Mkoani Kilimanjaro.

RPC wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema imetokea eneo la Saweni Wilaya ya Same, Mkoani Kilimanjaro.

Amesema gari lililoua Familia ya Watu 7 lenye usajili namba T.618 AWP aina ya Toyota Corola lilikuwa likitokea Mkoani Tanga kuelekea Moshi na kugongana uso kwa uso na gari T.515 DMV aina ya Volkswagen lililokuwa likitokea Moshi kwenda Dar es salaam na kusababisha majeruhi wanane.

"Chanzo cha ajali ni uzembe wa Dereva wa gari T.618 AWP Toyota Corola lililokuwa likiendeshwa na Ofisa Uhamiaji wa KIA kuhama upande wake wa kushoto wa Barabara na kuelekea upande wa kulia wa Barabara na kugongana uso kwa uso na gari T.515 DMV Voxywagen"

Chanzo: Millard Ayo
 
Wajaliwe pumziko jema.

Bado inahitajika elimu kubwa kwa jamii juu ya matumizi ya vyombo vya moto, inahitajika pia utulivu wa akili unapokua nyuma ya usukani wa gari.
 
Unabebaje watu 7 kwenye Corolla, halafu unaendesha kiboya, au ndio umeshachukuliwa na Monica Mrs UMUGHAKA?

Afisa Uhamiaji na Corrola namba A au mi ndio sielewi?
Ya Corolla kubeba watu 7 unaielewa? Halafu jamaa akaanza kuendeshea upande wa kulia, watu wote saba wanamshangilia tu, wala hamna wa kumkataza?
 
Mwanga mpaka Hedaru ni eneo hatari sana kwa mwendokasi na kuna baadhi ya maeneo yake yamewekwa kabisa vibao vya hadhari
BTW alitoka Tanga nyumbani ... Kuna baadhi ya maeneo siku ya kuondoka huagi kila mtu
True. Mambo ya kuaga ili upewe kuku wa bure ndio unajikuta umepewa kuku maalum wa kukupeperusha wewe na familia yako yote.
Jamaa alisafiri hadi na House girl

Hakuna check points huko, watu 7 ni wengi kwa Corolla
Watu8, usifanye masihara na nguvubya rushwa, buku tatu tu inamfanya njagu atulize mshono wa njaa
 
Back
Top Bottom