Same: Ajali yaua watu saba wa familia moja

Same: Ajali yaua watu saba wa familia moja

Watu saba wa Familia moja akiwemo Ofisa Uhamiaji wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), Sylvester Chambo na wanae wanne wamefariki dunia papohapo huku wengine wanane wakijeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na gari jingine Wilaya ya Same, Mkoani Kilimanjaro.

RPC wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema imetokea eneo la Saweni Wilaya ya Same, Mkoani Kilimanjaro.

Amesema gari lililoua Familia ya Watu 7 lenye usajili namba T.618 AWP aina ya Toyota Corola lilikuwa likitokea Mkoani Tanga kuelekea Moshi na kugongana uso kwa uso na gari T.515 DMV aina ya Volkswagen lililokuwa likitokea Moshi kwenda Dar es salaam na kusababisha majeruhi wanane.

"Chanzo cha ajali ni uzembe wa Dereva wa gari T.618 AWP Toyota Corola lililokuwa likiendeshwa na Ofisa Uhamiaji wa KIA kuhama upande wake wa kushoto wa Barabara na kuelekea upande wa kulia wa Barabara na kugongana uso kwa uso na gari T.515 DMV Voxywagen"

Chanzo: Millard Ayo
Alilewa huyo, halafu haya mambo ya kusafiri pamoja familia ni hatari sana,,

R.I.P
 
Too painful,fikiria baba na watoto wake wanne,wanapoteza maisha kwa wakati mmoja!,hizi taarifa zikimfikia mke wa jamaa,daaa sipati picha dada wa watu alikuwa na hari gani!!
Inauma Sana Sana, ni majonzi kabisa
 
IMG-20221012-WA0013.jpg

Hii ndo gari iliyopata Ajali
 
Wafiwa wote poleni sana Mungu awape nguvu na akawe faraja kwenu.

Marehemu wote wapumzike kwa amani.
 
Overtaking ndio chanzo cha ajali alikuwa anasababu gani ya kuwai mwisho wa siku kasababisha umauti wa watu 7.
Zaidi ya 70% ya ajali kwenye hii nchi chanzo ni wrong overtaking. Mtu hajaona mita mia mbele anaovertake tu.
Labda kwa sababu ya uzito, gari ikayumba na kuingia kulia. RIP kwa familia.
Uzito hauwezi kusababisha gari iyumbe, hata kama alikua amebeba vibonge.
 
Watu saba wa Familia moja akiwemo Ofisa Uhamiaji wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), Sylvester Chambo na wanae wanne wamefariki dunia papohapo huku wengine wanane wakijeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na gari jingine Wilaya ya Same, Mkoani Kilimanjaro.

RPC wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema imetokea eneo la Saweni Wilaya ya Same, Mkoani Kilimanjaro.

Amesema gari lililoua Familia ya Watu 7 lenye usajili namba T.618 AWP aina ya Toyota Corola lilikuwa likitokea Mkoani Tanga kuelekea Moshi na kugongana uso kwa uso na gari T.515 DMV aina ya Volkswagen lililokuwa likitokea Moshi kwenda Dar es salaam na kusababisha majeruhi wanane.

"Chanzo cha ajali ni uzembe wa Dereva wa gari T.618 AWP Toyota Corola lililokuwa likiendeshwa na Ofisa Uhamiaji wa KIA kuhama upande wake wa kushoto wa Barabara na kuelekea upande wa kulia wa Barabara na kugongana uso kwa uso na gari T.515 DMV Voxywagen"

Chanzo: Millard Ayo
corola imebeba watu saba? mhhhh. Wapumzike kwa amani, sote ni waja WAKE
 
Mwanga mpaka Hedaru ni eneo hatari sana kwa mwendokasi na kuna baadhi ya maeneo yake yamewekwa kabisa vibao vya hadhari. BTW alitoka Tanga nyumbani. Kuna baadhi ya maeneo siku ya kuondoka huagi kila mtu
Eti Bro Mshana ... mwanaume kulala kwa wakwee na kugegedana huwa inaleta madhara wakati wa safari?

Je ni kweli watu wa kaskazini wana imani mbaya pale familia inaposafiri katika gari/basi moja kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine hasa msimu wa sikukuu ama kuwapo na shughuli ya kifamilia sherehe/msiba?

nakubaliana nawe sio kila ndugu/jirani wa kumwaga
 
Back
Top Bottom