Same: Ajali yaua watu saba wa familia moja

Same: Ajali yaua watu saba wa familia moja

Hakuna check points huko, watu 7 ni wengi kwa Corolla
nafikiri hiyo sio hoja ya kujadili hapa; KWANI hizo corolla zipo aina nyingi
Corola Spacio (new model) inabeba watu 7 (wakiwemo watoto wawili ) tena wote wamekaa Vizuri
TOYOTA WISH ina row mbili nyuma za kubeba watu watatu x 2; bado kule mbele kwa dereva.

Ni msiba mkubwa sana jamani; Mungu awape nguvu na uvumilivu!
 
nafikiri hiyo sio hoja ya kujadili hapa; KWANI hizo corolla zipo aina nyingi
Corola Spacio (new model) inabeba watu 7 (wakiwemo watoto wawili ) tena wote wamekaa Vizuri

TOYOTA WISH ina row mbili nyuma za kubeba watu watatu x 2; bado kule mbele kwa dereva.

Nafahamu kuwa model zote hizo umetaja ni familia moja ya Corolla...

Lakini unashindwa kuelewa kwamba kwa ilivyozoeleka ukitaja Corolla, je ni gari ipi inayokuwa inatambulishwa?

Je na hizo gari umetaja, huwa watu wanazitambua kwa majina ya Spacio na Wish au Corolla?

Amesema gari lililoua Familia ya Watu 7 lenye usajili namba T.618 AWP aina ya Toyota Corola
 
Poleni Sana ndugu jamaa na marafiki. Raha ya milele uwape e Bwana na mwanga wa milele uwaangazie wapumzike kwa amani.
 
Unabebaje watu 7 kwenye Corolla, halafu unaendesha kiboya, au ndio umeshachukuliwa na Monica Mrs UMUGHAKA?

Ya Corolla kubeba watu 7 unaielewa? Halafu jamaa akaanza kuendeshea upande wa kulia, watu wote saba wanamshangilia tu, wala hamna wa kumkataza?
Hapo kwenye kuendesha kulia nadhani alikuwa anaovateki ndiyo hamadi uso kwa uso na VW..
 
[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]Eheeeee Mungu wangu.
 
Nafahamu kuwa model zote hizo umetaja ni familia moja ya Corolla...

Lakini unashindwa kuelewa kwamba kwa ilivyozoeleka ukitaja Corolla, je ni gari ipi inayokuwa inatambulishwa?

Je na hizo gari umetaja, huwa watu wanazitambua kwa majina ya Spacio na Wish au Corolla?
Anazingua mtuu mkuu, hivi Toyota Wish huku kitaa tunaiita Toyota Corolla?? [emoji12]
 
Watu saba wa Familia moja akiwemo Ofisa Uhamiaji wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), Sylvester Chambo na wanae wanne wamefariki dunia papohapo huku wengine wanane wakijeruhiwa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na gari jingine Wilaya ya Same, Mkoani Kilimanjaro.

RPC wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema imetokea eneo la Saweni Wilaya ya Same, Mkoani Kilimanjaro.

Amesema gari lililoua Familia ya Watu 7 lenye usajili namba T.618 AWP aina ya Toyota Corola lilikuwa likitokea Mkoani Tanga kuelekea Moshi na kugongana uso kwa uso na gari T.515 DMV aina ya Volkswagen lililokuwa likitokea Moshi kwenda Dar es salaam na kusababisha majeruhi wanane.

"Chanzo cha ajali ni uzembe wa Dereva wa gari T.618 AWP Toyota Corola lililokuwa likiendeshwa na Ofisa Uhamiaji wa KIA kuhama upande wake wa kushoto wa Barabara na kuelekea upande wa kulia wa Barabara na kugongana uso kwa uso na gari T.515 DMV Voxywagen"

Chanzo: Millard Ayo
Wapumzike kwa amani

Najiuliza Corolla kubeba watu 7.... kwamba wawili mbele watano nyuma???
 
Back
Top Bottom